Kuongezeka kwa Hati zenye shaka na hati mbaya za ukaguzi kwa mwaka 2019/20

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ripoti za Ukaguzi za mwaka 2019/20 zinaonesha kuongezeka kwa Hati Zenye Shaka na Hati Mbaya zilizotolewa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Miradi ya Maendeleo. Mwenendo wa Hati zilizotolewa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa a Miradi ya Maendeleo ni kama ifuatavyo;

Hati za Ukaguzi Zilizotolewa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa, kati ya Halmashauri 185 zilizokaguliwa, Halmashauri 124 sawa na asilimia 67 zilipata Hati Zinazoridhisha, Halmashauri 53 sawa a asilimia 29 zilipata Hati Zenye Shaka na Halmashauri 8 sawa a asilimia 4 zilipata Hati Mbaya. Hati zinazoridhisha zimeshuka kwa asilimia 28 kutoka asilimia 95 mwaka 2018/19 hadi asilimia 67 mwaka 2019/20.

Hati Zenye Shaka zimekuwa zikiongezeka kwa miaka mitatu mfululizo kutoka asilimia 4 mwaka 2017/18, asilimia 5 mwaka 2018/19 hadi kufikia asilimia 29 mwaka 2019/20.

Halmashauri zilizopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Wilaya za Shinyanga, Singida, Itigi, Igunga, Sikonge, Urambo na Momba.

Hati Zenye Shaka na Hati Mbaya zilitolewa kutokana na mapungufu mbalimbali ikiwemo, mabadiliko ya kiasi kilichoripotiwa katika hesabu za mwaka 2018/19 bila maelezo, taarifa za fedha kuripoti kiasi zaidi au pungufu bila maelezo, kukosekana kwa nyaraka za matumizi pamoja na ufafanuzi wa matumizi, kutokuzingatiwa kwa Sheria ya ununuzi wa umma pamoja na tatizo la uandaaji wa hesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa ya uandaaji wa hesabu katika sekta ya umma (IPSASS).

Vilevile, ripoti ya CAG inaonesha mapungufu katika mifumo ya usimamizi wa ndani ikiwa ni pamoja na Wakaguzi wa Ndani kutokukagua hesabu za mwisho za Halmashauri 54 kabla ya kuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya ukaguzi. Hi ni kinyume na Memoranda ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa 14(4) (d). Aidha, kumekuwepo wa viashiria ya rushwa, kutokamilika kwa miradi pamoja na kutotumika kwa miradi iliyokamilika.

WAJIBU INSTITUTE
 
Hao waliopewa hati chafu au zenye mashaka hawajui mbinu za kimedani. Aliyekua mkurugenzi Tanga jiji anakula hela na akijamtu anatulizwa. Anajua kununua watu yule mzee. Hata wanaopambana na rushwa yeye alishawaweka mfukoni.
Waandishi wa habari Tanga walinunuliwa jumla hakuna mwanahabari Tanga jiji
Miradi inayotakiwa kuzinduliwa na mwenge kama alishapiga,mwenge hauendi.
Hao waliopewa hati chafu labda hawajatumia rasilimali fedha vizuri
 
Back
Top Bottom