Kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini kunatokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia na siyo kosa la serikali ya Rais Samia

Unapoondoa kodi lazima uwe na mbadala wa mapato ya kodi hiyo kwa haraka ili nchi iendelee kujiendesha

Kuondoa kodi siyo kitu rahisi kama unavyofikiria, huo siyo ushauri rafiki na haiwezekan
Iviii zile kodi za miamala za simu zilizokuwa imposed ni kodi ipi ilifutwa ilii izo za miamala ya simu iwe mmbadalaa
 
Hiyo bei ya Agosti 2020 na siyo March 2021
Una matatizo yoyote? Nauliza hili swali ili nijue kwanza
Mwezi August 2020 bei ilikua 1832

Screenshot_20220406-125118_1.jpg
 
Bei ya mafuta ni 2700-3000


Hiyo 3400 labda wanakouza kwa madumu huko vijijini au migodini ambako wanajiamulia bei
Kigoma bei halali ni 3093, na ndio Bei ya juu nchi nzima

Unapaswa kusema ni kati ya 2700-3100

Hizi bei zimetolewa na ewura Wala huna haja ya kukaza mishipa
 
chapati moja 500,kitumbua na andazi 300,chai 400, unga kilo1300 kweli vita ya urusi kiboko
 
Kwani hawa Marais wanaopambana na changamoto ya mafuta kupanda bei ni kosa lao?🐒🐒🐒
7UID.jpeg
IMG_20220402_184504_432.jpg
IMG_20220404_100611_745.jpg
AARD4K.jpeg
 
Bei ya mafuta ni 2700-3000


Hiyo 3400 labda wanakouza kwa madumu huko vijijini au migodini ambako wanajiamulia bei
Unaongea kama juha. Kwahiyo siku hizi kuna bei za migodini na za mikoani? Ujinga wa nchii hii mpk kuwe na mbadala wa sifiasifia
 
Unaongea kama juha. Kwahiyo siku hizi kuna bei za migodini na za mikoani? Ujinga wa nchii hii mpk kuwe na mbadala wa sifiasifia
Bei elekezi ni kwa ajili vituo vilivyosajiliwa kuuza mafuta. Yanayouzwa kwenye madumu yanauzwa kinyume na utaratibu
 
KUONGEZEKA KWA BEI YA MAFUTA YA PETROL NA DIESEL KUMESABABISHWA NA ONGEZEKO LA BEI KTK SOKO LA DUNIA NA SIYO KOSA LA RAIS SAMIA.

Hapo jana serikali imetangaza bei mpya ya mafuta ya bei ya petroli na diesel ambapo kwa hapa Tanzania bei inatarajiwa kuanzia leo kuwa kati ya sh 2700-3000

Kuna watu wengi hutumia mwanya wa ongezeko la bei ya mafuta kuwa ni uzembe wa Rais Samia na wengine wamekwenda mbali kwa kusema kuwa angekuwepo Magufuli (R.I.P) BEI ISINGEPANDA; Huu ni upotoshaji na uchonganishi usiokuwa na tija kwa Taifa letu. Rais Magufuli amefanya kazi kubwa sana ktk nchi yetu lakini siyo sahihi kusema angekuwepo yeye bei ya mafuta isingekuwa kubwa ilihali kiuhalisia bei ya mafuta haijapanda ktk soko la ndani baki ktk soko la dunia ambapo kwa namna yoyote athari za bei lazima uzipate kwa kuwa sisi siyo wazalishaji wa mafuta hayo

Linapokuja suala la mabadiliko ya bei ya mafuta ktk soko la dunia bei hiyo hubadilika ktk nchi zote na tunaoumia hasa ni nchi ambazo hazizalishi mafuta ikiwemo Tanzania.

Bahati nzuri ktk ukanda wa Afrika Mashariki licha ya bei ya mafuta kupanda ktk soko la dunia lakini bei yetu ni nafuu kuliko nchi zingine za afrika mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kwa wale wanaoamini kuwa Magufuli angekuwepo bei ya mafuta isingepanda naomba niwakumbushe kidogo.

Kipind Magufuli anaapishwa 2015, TZ bei ya petroli ilikuwa 1900-2000/litre ambapo bei ya mafuta duniani ilikiwa ni $40 kwa pipa.

Mpaka anafariki 2021, aliacha mafuta yakiuzwa 2400-2500/-. Leo hii pipa la mafuta katiķa soko la dunia ni hadi $140 na Tanzania yakiuzwa kati ya 2700-3000 kwa lita.

Ikumbukwe kuwa bei imeongezeka karibu mara mbili ya bei ya mwaka 2020 na karibu mara tatu ya bei ya mwaka 2015 lakini serikali imejitahidi kudhibiti mfumuko wa bei ya mafuta.

Uwezo wa serikali yetu ni kudhibiti mfumuko wa soko la ndani liendane na soko la dunia lakini si rahisi kudhibiti bei tofauti na ile inayouzwa ktk soko la dunia

Aidha tunaweza kulaumu tu kama bei ya mafuta nchini ikiwa kubwa kuliko nchi zingine au kuliko ktk soko la dunia.

Njia pekee ya kuweza kukabiliana na makali ya bei ni kwa serikali kutoa fedha ya ruzuku kwa wafanyabiashara ili kuuza bei rafiki (mfumo huu ni wa gharama ambao unategemeana na bajeti na uwezo wa serikali kifedha)

Tumeshuhudia nchini Kenya kwamba siyo tu bei imepanda lakini wenzetu wana uhaba wa mafuta kiasi cha kufanya kuwe na foleni ktk vtuo vya mafuta.

Hapa chini nimeweka bei za mafuta ktk nchi mbalimbali mpaka kufikia jana ambayo kimsingi bado inaonesha kuwa bei ya Tanzania ni nafuu kulinganisha na nchi zingine Afrika Mashariki.

Mimi binafsi ninaamini serikali haipendi wananchi wake wateseke hivyo wanaendelea kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wetu ili kuona namna bora ya kuhakikisha ongezeko hii la bei halituathiri kwa kiasi kikubwa.

Tuendelee kushikamana na serikali ktk kipindi hiki kigumu lakini tusisahau kushauri namna bora zaidi badala ya kupotosha au kuchonganisha.

Kwa mtizamano wangu ni wakati sasa serikali kuwekeza zaidi ktk gas badala ya mafuta ya petrol na diesel ili tupunguze kasi ya utegemezi wa nishati.

View attachment 2177633

Hapa chini ni bei ya mafuta ktk nchi mbalimbali hadi kufikia jana kabla ya bei mpya za leo ikionesha kuwa licha ya bei ya mafuta kupanda lakini bei yetu ni nafuu kuliko nchi zingine zingine Afrika Mashariki.
View attachment 2177634

View attachment 2177700
Wakati wa mlipuko wa covid 19 bei ya mafuta kwenye soko la dunia iliteremka hadi kufikia dola 20 kwa pipa kwani watu wengi walikuwa lockdown na uzalishaji viwandani ulikuwa umesimama kwa kiasi kikubwa. Lakini hapa kwetu bei ya mafuta iliendelea kupanda. Ilifika hadi watu wa Mbeya kununua mafuta hayo toka Zambia kwani kule bei iliteremka sana licha ya mafuta yao kupitia DSM.

Serikali yetu ina aina ya tozo zaidi ya kumi kwenye bidhaa hii ya mafuta kama ilivyokuwa kwenye bidhaa za kilimo hususani kahawa. Na kila mwaka wa bajeti, serikali huwa inaongeza aina ya tozo kwenye bidhaa hii ya mafuta.

Vita ya Russia vs Ukraine imepelekea nchi za Amerika na za ulaya kususa (sanction) kununua mafuta toka Russia ili kumbana mruso kiuchumi ashindwe vita. Russia ni mzalishaji mkubwa duniani. Theluthi moja ya mafuta yote duniani hutoka Russia. Ususaji huu umepelekea nchi ya Saudi Arabia (top producer) na zile za OPEC kuendelea kupandisha bei za mafuta yao ili kujinufaisha na mzozo huu. Leo pipa linauzwa kwa dola 150. Na bado litaendelea kupanda. Si ajabu ndani ya wiki mbili zijazo likafika dola 300. Hatujui vita hiyo itachukua muda gani kwisha na hali kurejea tulikotoka. Lakini mafuta toka Russia yameendelea kupungua bei hadi sasa kufikia dola 30 kwa pipa.

Hivyo kama hatutajipanga vizuri kila kitu kitavurugika. Mfumuko mkubwa wa bei utatokea. Uchumi wa nchi utasinyaa sana. Thamani ya pesa yetu itateremka sana. Makusanyo ya kodi yataporomoka kwani uchumi utakuwa umesinyaa. Maamuzi aliyofanya Makamba ya kuagiza mafuta haya ya bei ya dola 150 kwa pipa la crude oil (refined oil ni zaidi ya dola 230) kwa mkupuo wa kututosheleza miezi 3 hadi Juni 2022? si sahihi hata kidogo. Kwani kama bei ya soko la dunia itateremka hadi kufikia dola 80 kwa pipa mwezi May 2022, itakuwa imekula kwetu. Na kuna dalili kubwa wa mzozo huu wa Russia vs Ukraine kuisha hivi karibuni.

Mapendekezo makini ya kukabiliana na tatizo hili ni kama ifuatavyo:
1. Kupunguza kwa kiwango kikubwa cha idadi ya tozo za serikali katika bidhaa hii hadi zibakie aina ya tozo sisizozidi tatu kama tulivyofanya kwa kahawa ili kulinda uchumi wa nchi yetu.

2. Kubana sana matumizi ya serikali yasiyo ya lazima hususani washa, semina na safari za ndani ya nchi na nje ya nchi.

3. Kuiga mfano uliooneshwa na nchi za India na China, wa kununua mafuta haya kutoka Russia ambayo yameteremka bei hadi kufikia dola 30 kwa pipa baada ya sanctions.
 
Rais lege lege hawezi kusanya kodi kutoka vyanzo vigumu. Badala yake hukusanya kodi Kupitia vyanzo laini kama hivi vya mafuta.

RIP JPM
 
Back
Top Bottom