Kuongeza wigo wa kodi na makusanyo: Serikali ibuni vyanzo vipya na Mkurugenzi Mkuu wa TRA na waajiriwa wapya wa TRA waajiriwe kwa mikataba

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Binafsi naamini watu wenye kipato nchi hii na wanaoweza kulipa kodi ni wengi tu ila kinacholosekana ni ubunifu wa vyanzo vya mapato pamoja na watumishi wa TRA kutotaka kukimbizana na watu kukusanya kodi bali wanataka zaidi kukusanya kodi zisizo na usumbufu/changamoto kama PAYE, VAT na nyinginezo.

Ili kutafuta tatizo hili, napendekeza mikakati/njia mbili ambapo moja ni ya muda mfupi na nyingine ni ya muda mrefu.

Mkakati wa Muda Mrefu

Katika eneo hili, nashauri serikali ibadili Sheria waaajiriwa wote wa TRA kuanzia Mkurugenzi Mkuu na watumishi wengine wote wa TRA waajiriwe kwa mikataba ambayo itakuwa renewable based on performance.

Tukiwa na ajira za aina hii kwa taasisi sensitive kwa uchumi nchi kama hii TRA,nina hakika wafanyakazi wa TRA kuanzia Mkurugenzi wao watajituma zaidi na malengo ya ukusanyaji kodi yatayowekwa yatatimia kwa asilimia kubwa tu

Mishahara minono kwa wafanyakazi wa TRA sio suluhisho pekee linaloweza ku-motivate watumishi wa TRA kujituma zaidi bali tunapaswa kuangalia na njia zingine zinazoweza kuwafanya wawajibike zaidi likiwemo hili swala la ajira za mikataba.

Mkakati wa Muda Mfupi

Hapa nashauri serikali iwaruhusu TRA waajiri vijana wataoksanya kodi kwa mikataba ya muda mfupi na vijana hawa walipwe kwa commission kulingana na wanachokusanya.

Vijana hawa, hasa waliosomea mambo ya kodi, wanaoweza kutumika kukusanya zile kodi ambazo zinahitaji ufutiliaji wa karibu kama kodi za majengo, kodi zinazotokana na nyumba za kupangisha, n.k.

TRA itakuwa na jukumu la kuwawezesha vijana hawa kwa kuwapa vitendea kazi kama magari, mashine za kukusanyia kodi, askari kwa maana ya ulinzi na hata kuwapa semina za muda mfupi kwa lengo wa kuwajengea uwezo.

Naamini, tukifanya kazi mapendekezo haya kwa kuyaboresha n.k, licha ya kutoa ajira za muda mfupi kwa vijana, tutwaweza pia kuongeza mapato ya nchi na zaidi tutakuwa tumeongeza wigo wa kodi na hivyo kuna uwezekano wa kupunguza hata PAYE na kodi zingine kama VAT kwani asilimia kubwa zaidi ya watanzania sasa watakuwa wanaolipwa kodi na si kama ilivyo hivi sasa ambapo ni watanzania wachache tu ndio wanaobeba mzigo wa kulipa kodi.

Kwa jinsi deni la Taifa lilivyoongezeka huku serikali ikiwa na miradi ya matrilioni ya kuikamilisha, swala la kuongeza mapato ya nchi linapaswa kuwa ni kipaumbele namba moja kwa nchi tupende, tusipende vinginevyo huko mbeleni kuna mambo yanaweza kukwama na hata nchi kutokopesheka tena.
 
"Vijana walipwe kwa commission kulingana na wanachokusanya" mjomba kukusanya kodi sio sawa na kuuza bidhaa mtaani, hao vijana watalazimisha kuwakamua watu matokeo yake turudi enzi za mwendazake.
 
"Vijana walipwe kwa commission kulingana na wanachokusanya" mjomba kukusanya kodi sio sawa na kuuza bidhaa mtaani, hao vijana watalazimisha kuwakamua watu matokeo yake turudi enzi za mwendazake.
Kwani si wanakusanya kulingana na sheria na sio kwa wao kuja na kodi zao.

Elewa kodi kama kodi za majengo zinahitaji ufuatiliaji wa karibu hivyo ukiwalipa kwa commission, watajituma zaidi na kukusanya zaidi hata kama ni kwa kuzunguka mitaani siku nzima.

Watanzania tunatumia sehemu ndogo sana ya akili zetu na muda wetu kubuni vitu vinavyoweza kuwa suluhu ya matatizo yetu na tunatumia sehemu kubwa ya akili na muda watu kulalamika, kunung'unika na kujilaumu na pia kujadili matukio.

Hali hii ni moja ya sababu kwanini sisi ni watu wa kuiga tu vitu kutoka kwa wenzetu badala na sisi tubuni vyetu na wenzetu waige.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom