kuongeza mikoa mipya ni kuongeza matumizi ya serikali hawa wakuu wana kazi gani hasa?

harakat

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Messages
2,901
Points
2,000

harakat

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2011
2,901 2,000
Tanzania imeongeza mikoa mipya minne kwenye orodha ya mikoa yake ambayo ni
Simiyu,Geita,Katavi na Njombe.Kuongezwa kwa mikoa hii inamaana kuwa hapa pataitajika
mkuu wa mkoaa ,gari yake ,walinzi ,ofisi na vitu vingine Tija yao iko wapi?
Mi ninafikiri kwamba serikali ingefikiria kupunguza matumizi yake badala ya kuongeza kupitia
mambo kama haya...
 

clet 8

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
1,109
Points
1,500

clet 8

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
1,109 1,500
''Mwenye shibe siku zote huwa hamjui mwenye njaa'' Nchi inakabiliwa na matatizo lukuki halafu tunaongeza watu wa kuwalipa posho na marupurupu! Wanfunzi wanakoswa mikopo elimu ya juu, watoto wanakoswa dawa hospitali pamoja na kina mama, Nchi haina umeme wa uhakika, Nchi haina maji safi na salama kwa watu wake, wanafunzi hawana madawati na vitabu katikashule zetu.Hii ni ajabu! watawala wetu hawana utamaduni wa vipaumbele. Ingekuw jambo la busara watawala wetu wangerekebisha hizo kasoro katika maeneo hayo kwa kuboresha hayo machache niliyotaja halafu wakatuteulia hao ma-Dc&RC. Kusema kweli hawa wteule kazi zao huwa hazionekani!
 

sweya

New Member
Joined
Sep 15, 2011
Messages
3
Points
0

sweya

New Member
Joined Sep 15, 2011
3 0
me naona jk sasa aende uhamisho kwani yeye hatangazi kuna tatizo wapi nchi hii ,kafanya nini kuta2a hilo tatizo bali kwenye sherehe utasikia kawapisha mabalozi kawateua wakuu fulani na sasa wakuu wa mikoa hebu chuja mwenyewe Engneer sitelah manyanya mbunge wa viti malumu tena kamuteua kuwa mkuu wa mkoa hivi wa2 wengine hawapo au kunanini jamaniiiii a nimechoka nisaidieni wadau.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,008
Points
1,225

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,008 1,225
Tatizo ni kuwa tumeshindwa kuyaendeleza kwa ufanisi maeneo ya sasa ya kiutawala. Badala ya kuangalia kiini cha tatizo, wao wanadhani kuwa tatizo ni ukubwa wa maeneo hayo na ndio maana wanaona suluhisho ni kuyagawa. Wasichokifahamu ni kuwa kwa watendaji hawa tullio nao, tunapogawa mikoa au wilaya tunagawa matatizo na kuzidi kuyasambaza kwa kasi zaidi
 

kidjula

Member
Joined
Sep 13, 2010
Messages
8
Points
20

kidjula

Member
Joined Sep 13, 2010
8 20
acheni majungu, sasa kama mikoa haitaongezwa mnategemea k2 gan? mm nimeshahaidiwa kitengo flan nyeti katika mkoa flan mpya, acheni hizo, nikipata ndo mikoa mipya isianzishwe. vuteni subra jamani
 

Forum statistics

Threads 1,378,675
Members 525,139
Posts 33,720,338
Top