Kuongeza majimbo ya uchaguzi kuna tija gani kwa taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuongeza majimbo ya uchaguzi kuna tija gani kwa taifa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, Jan 26, 2010.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na fikra ndani ya tume ya uchaguzi kuwa kuna mpango wa kuongeza majimbo ya uchaguzi kwenye uchaguzi ujao. Hii inathibitisha kuwa ni jinsi gani watunga sera wanavyoona umuhimu wa kulinda masilahi binafsi badala ya yale ya Taifa. Hivi unapoongeza mbunge mmoja umejiuliza maswali haya kwanza?
  1. Nini kazi ya mbunge katika jimbo?

  2. Je wabunge waliopo wamefanikishaje kazi hii?

  3. Gharama za kumhudumia mbunge mmoja kwa miaka mitano kuanzia Posho, Mshahara na matibabu ni kiasi gani?

  4. Je Kiasi hiki kina faida gani kwa jimbo lake yaani cost-benefit ni kipi kikubwa?

  5.Tofauti gani iliyopatikana kutokana na kuongeza wabunge na watawala kama kugawa mikoa na wilaya kwa maendeleo ya wananchi wa sehemu hizo?

  6. Hivi tukiwa na wabunge wachache (Tuseme kila wilaya moja mbunge mmoja) mwenye uwezo wa kusimamia serikali na kutoa mawazo huru juu ya maendeleo ya nchi kuna hasara gani?

  7. Je hatuoni kuwa hizi pesa tunazowalipa wabunge ambao mchango wao ni sifuri zaidi kusbiri kupitisha miswada ya Kiingereza (wakati wengi wao lugha hii hawaijui) wasiyoijua na wala kuisoma wengine hawasomi zingeweza kuboresha huduma za jamii kama mahospitali, maji na barabara?

  8. Je kama mchezo ni kuongeza idadi ya wabunge ili kupunguza misuguano ndani ya CCM kati ya wabunge waliopo na wanaowania kuchukua nafasi hizo, hatuoni kuwa baada ya miaka mitano ingine ugomvi utazuka tena na kuongeza, kuongeza kuongeza mpaka wana-CCM wote karibu Milioni nne (kama wasemavyo wao) wakawa wabunge nchi itakuwa na uwezo wa kuwahudumia?.

   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi nilikuwa Tanzania mwaka jana baada ya miaka kumi na mbili ugaibuni. Niliondoka Tanzania baada ya kumaliza form six kama vijana wengi wa miaka ile ya mwishi ya 90,s hivyo niliondoka kijana na nilirudi mtu mzima. Mimi kwa mwangalio wangu nimegundua kuwa Watanzania wameendelea sana na wamejitahidi kwa kina namna na nimefurahi kuona huo mwamko, kila mtu anajaribu kufanya kazi kwa bidii na hakuna lawama kwa watu kwa watu. Tatizo kubwa Tanzania ni serikali! vitu ambavyo serikali inatakiwa kuvifanya haifanyi mfano. mipango ya barabara, umeme, maji na maji safi, elimu ya msingi na sekondari, mipango ya miji, rushwa ya hali ya juu kwenye vibali vya kina aina, ushuru usiokuwa na mpangilio. n.k. Tatizo lingine ni kwamba hakuna mpangilio mzuri wa uongozi serikali ni kubwa lakini haina mipangilio mizuri mfano. ni vigumu kujua ni sehemu gani ya kuchukua vyeti vya vizazi na vifo kuna sehemu zaidi ya tatu hivi wilayani, mkoani na makao makuu!!!. Kilicho nishangaza ni pale ambapo kijana mmoja aliamua akalipe kodi kwasababu hajawaona walipa kodi kwa miaka miwili na waka omba rushwa ili aweze kulipa kodi ambayo hata serikali ilikuwa haijui kama inatakiwa kulipa. Serikali vilevile kumeongezeka ubinafsi kila mfanyakazi serikalini anafikiria anakula vipi rushwa kuanzia mapolisi, wanasiasa, walimu, madaktari, na wizara zote. Mimi nimesikitishwa sana na serikali ya Tanzania na sikuona malalamiko yeyote kutoka kwa watu. Swala la mwisho ni siasa magazeti ya Tanzania kwa sasa hayaandiki habari za msingi kama umeme, elimu, au vibali vya viwanja bali ni siasa ambazo kwa mara nyingi si za maendeleo bali majungu na madongo.
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kamundu, nakubaliana na wewe kabisa kuwa UKUBWA wa serikali ni njia mojawapo ya kudumaza huduma za jamii. Sababu kubwa ni kuwa na "mlolongo mrefu wa maamuzi-long chain of command (bureaucracy) - na hii ndiyo chanzo cha rushwa" ili mtu apate short cut ya kupata huduma.

  Tunaweza sema kuwa serikali ni mwajiri mkuu kwa nchi yetu ambayo kiuchumi bado ipo nyuma, lakini ule mtazamo wa kuona kumpatia mtu nafasi nzuri ya kuangalia rasilimali (custodian off public resources) ni kumpatia ulaji ndiyo unachofanya wanasiasa kuona njia pekee za kulipa fadhila ni kumpatia mtu cheo hata kama hakitakuwa na tija kwa taifa. Kwa nini tusi-focus zaidi kwenye kuajiri watendaji yaani nguvu kazi manesi wa kutosha, madaktari, walimu walio bora watafiti na hawa kuwalipa vizuri ili waweze kudeliver badala ya kuongeza wasimamizi (Wabunge, wakuu wa wilaya n.k) ambao nao hata hawajui wanasimamia nini zaidi ya kubeba propaganda za Chama na kuvaa mashati kijani tu?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hukuona malalamiko kutoka kwa watu???? Ni Tanzania gani unayozungumzia????? Ubinafsi, rushwa halafu hakuna malalamiko sijui.

  Tanzania tumeendelea, hebu tuambie kivipi??? Kila mtu anafanya kazi kwa bidii, inawezekana maana wauza vocha wengi, madereva wa bajaji, pikipiki za kubeba abiria, baiskeli za kubeba abiria, madalali wa nyumba na viwanja wanaokaa vijiweni, wapiga debe wa daladala hizo ni kazi kweli.

  Hebu rudi utembee nenda vijijini ujionee. At the bottom line hakuna haja ya kuongeza majimbo ni kutafutiana ulaji tu
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni biashara ya watu na njia ya ccm kutawala zaidi kwani vyama vya upinzani ni vichanga kwahivo kupambana katika majimbo mengi inakuwa ngumu (they will stretch very thin na kushindwa zaidi)

  Pia ni mbinu inayotumika ukzidiwa, kuita majeshi

  hakuna katika hao wanaotaka majimbo ambao wanajua mzigo wetu na maana ya uchumi wala upeo wa kugundua maendeleo sio idaid ya wabunge nbali ni efficiency ya wabunge na utawala uliopo madarakani

  tunaweza kabisa kuwa na wabunge 80 na tukashinda umasikini

  mfano ni mtu kama magufuli anaweza kuwa mbunge hata wa majimbo kumi na bado akawa on top of issues na unaweza ukawa na ngeleja 200 bila hata tija
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa nimekuelewa lakini biashara ni lazima iwe na faida na kwa CCM kama chama cha siasa kinachopigania ridhaa ya wananchi, faida ingekuwa ni kuwaletea maendeleo na kuboresha hali zao kiuchumi, Kwa style hii ndiyo tusime CCM ni chama cha biashara yaani ni kwa wanachama kujifaidisha wenyewe lakini je mbona wapo karibu 4Millioni? au tunadanganywa maana nao wangedai gawio(dividend).

  Hapa tupo ukurasa mmoja, kuwa "ukubwa wa pua si wingi wa kamasi", umefikia wakati sasa hivi ndani ya CCM wenyewe waangaliane kuwa si wote wanaotaka uongozi ndani ya chama na serikali ni watu efficient, ningeshauri JK kama mwenyekiti wa CCM, Rais wa nchi na mtunga sera mkuu akaachana na ile dhana ya "Ukitaka kula sharti uliwe" yaani mtu akitoa nguvu na mali kumsaidia mtu kuingia mdarakani basi ni lazima apewe kula kwa kuwa kishaliwa huyu. Tutoe dhana ya kula iwe ni dhana ya kuliwa tu basi yaani ukitaka kuongoza lazima tukupime kwa matokeo ya uongozi wako siyo uwezo wako wa kupiga domo.

  Kwi kwi kwi! Mkuu hapa umeniacha hoi but mfano wako upo hai kabisa, yaani watu kama akina Sophia Simba and the like ni mzigo kwa Taifa kwani resources imput taifa inazoingiza kwa hawa(Mshahara +marupurupu+ulinzi) ni kubwa mno with zero output. Kwenye production plant tunasema efficiency ni zero yaani output/input= 0.
   
 7. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuongeza majimbo kwa kupunguza ukubwa wa jimbo mimi sioni mantiki, kwa mtazamo wangu kila wilaya au halmashauri ya wilaya ingekuwa na mbunge mmoja tu. Unajua haya mambo ya kuwa na wabunge lukuki ni gharama sana na ni fujo tu maana haina tija yoyote kwa sisi wananchi.

  Mbaya sana siku hizi ubunge umekuwa kama ajira kwa wabunge, na wananchi wanadhani mbunge ndiye anayetakiwa ''kuleta'' maendeleo au kutoa msaada kwa wapiga kura.

  Kutokana na mitazamo hii na mazoea haya wabunge wamekuwa wakihitajiwa kuwa na fedha nyingi sana ili kuweza kutimiza matarajio ya wapiga kura. Serikali nayo bahati mbaya imekuwa na mtazamo huo potofu ndo maana wakaanzisha mfuko wa maendeleo wa jimbo- hivyo kukoleza dhana nzima ya kuwa mbunge ndiye mleta maendeleo. Mtazamo huu potofu ndio chanzo cha rushwa katika uchaguzi na ufisadi pia.

  Kuna haja ya kubadili mfumo wa ubunge ili kazi ya msingi ya mbunge ( Bunge) ijulikane kuwa ni kutunga sheria za nchi na iwe kazi ambayo haina maslahi mengi kama ilivyo sasa, yaani mbunge alipwe kuhudhuria vikao basi asiwe mjumbe wa bodi, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, waziri n.k. Ikifanyika hvyo ubunge hautakuwa dili kubwa sana kama ilivyo sasa bali itakuwa kazi ya wito zaidi kuliko maslahi.

  BTW, jimbo la Mh. Hawa Ghasia lazima litagawanywa tu, kwasababu kuna upande mmoja wenye wapiga kura wengi hawamtaki kabisa huyu mama hivyo akigombea lazima atapigwa chini. Mkakati alioufanya ni kuhakikisha jimbo linagawanya na yeye anagombea upande ule anaokubalika, ule upande asiokubalika ameandaa mgombea moja ambaye alikuwa mtumishi wa elimu huko Dodoma kamhamishia hapa Mtwara. Jamaa kila wakati yupo kwenye kampeni na anakubalika sana. Hivyo anapiga kampeni kote kote kwa mama na kwake.
   
 8. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  kwa Tanganyika mahesabu rahisi wabunge wa kuchaguliwa na wananchi moja kwa moja = 40,000,000/ 206,130 (40m population Tanganyika; 206,130 idadi ya wapiga kura kila jimbo) tukigawa 40,000,000 kwa 206,130= wabunge 194 maximum.

  Upande wa Zanzibar huko inabidi special formula, maana idadi ya Wazanzibari 1,400,000.

  Hivyo idadi ya jumla ya wabunge(Tanganyika + Zanzibar) wakuchaguliwa inatakiwa iwe pungufu ya idadi ya sasa ambayo Bunge la Muungano lina wabunge 323.
   
Loading...