kuongeza majimbo ni demokrasia ama ufisadi mwingine

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Tume ya uchaguzi imesema ina nia ya kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi -- Ukumbi wa Bunge una uwezo wa kuchukua wabunge wengine 23 kutoka idadi ya 323 na kulifanya Bunge letu tukufu kuwa na wabunge 326.

Hapa TZ tupo milioni 40 na wabunge ni hao 326 --- Jaji Mark Bomani anahoji Marekani ina watu milioni 300 lakini idadi ya wabunge ni 425, Angalia India anasema ina raia bilioni moja lakini wabunge ni 542.

Je tunachokifanya hapa ni kuonesha demokrasia ama matumiz mabaya ya rasilimali maana ukiangalia uwiano inachekesha pamoja na umaskini wetu.

Hivi ni majimbo mangapi ambayo yameomba kuongezwa kupitia vikao vya halsmahasuiri za wilaya na haya yataongeza kiasi gani cha fedha katika uchaguzi na uendeshaji wa bunge. Naombeni Nondo
 
Jibu unalo!
 
Demokrasia ya kwetu ni matumizi makubwa ya pesa za wavuja jasho pasi kujali shida zinazowakabili kwa mantiki hiyo ili kuongeza matumizi ni lazima tu ongeze majimbo
 
Tume ya uchaguzi imesema ina nia ya kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi -- Ukumbi wa Bunge una uwezo wa kuchukua wabunge wengine 23 kutoka idadi ya 323 na kulifanya Bunge letu tukufu kuwa na wabunge 326.

Hapa TZ tupo milioni 40 na wabunge ni hao 326 --- Jaji Mark Bomani anahoji Marekani ina watu milioni 300 lakini idadi ya wabunge ni 425, Angalia India anasema ina raia bilioni moja lakini wabunge ni 542.

Je tunachokifanya hapa ni kuonesha demokrasia ama matumiz mabaya ya rasilimali maana ukiangalia uwiano inachekesha pamoja na umaskini wetu.

Hivi ni majimbo mangapi ambayo yameomba kuongezwa kupitia vikao vya halsmahasuiri za wilaya na haya yataongeza kiasi gani cha fedha katika uchaguzi na uendeshaji wa bunge. Naombeni Nondo
Huu ni ufisadi mwingine. Hakuna haja ya kuongeza majimbo.
Mwisho kila familia itaomba kuwa na wawakilishi bungeni na kama bunge lenyewe ni hili! hakuna haja kabisa.
Badala ya kuhangaika kuongeza majimbo kwa nini tume isishughulikie hukumu ya mahama kuu ya mgombea binafsi?
Jamani hizi tume mwisho wake zitatuletea maafa! Nisingependa maafa kama ya Kenya yatokee hapa maana mwanzo wa mvua ni mawingu.
 
Hivi manakumbuka kuwa lile jengo jipya lilijenga kwa sababu la zamani lilikuwa alitoshi, wabunge walikuwa wanatarajiwa kuongezeka ndio wakajenga jipya?

Usishangae mwakani wakajenga jingine kwani majimbo yameongezeka.

Hivi wanatumia vigezo gani? wacha nikatafute hivyo vigezo nikivipata navileta na uchambuzi wake.
 
Ukweli nikwamba wa Tz tunapigwa sana na hawa wanasiasa sasa wameanza kuitana ilikutumaliza sisi sasa hakuna mantiki ya kuongeza majimbo wandugu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom