Kuongea kiingereza mbele ya wasiojua kiingereza sio usomi au ujanja ni utumwa

Salathiel m.

Senior Member
Mar 12, 2011
185
41
Kuna watu wanatabia ya kuongea kizungu au wanachanganya changanya kiswahil na kizungu ili tu waonekane wajanja au wasomi au tu kupenda sifa. anaona ataonekana mshamba akiongea kiswahili moja kwa 1,kumbe ni ujinga mtupu wenzetu wachina wakienda nchi yoyote hua wanaongea lugha yao nyie mnawaona kama awajasoma,kujua kizungu sio usomi kuna nchi watu wake wanatumia kiingereza bado utakuta wanakabiliwa na tatizo la watu kutojua kusoma na kuandika. HUO NI UTUMWA KUSHOBOKEA LUGHA YA WATU,JE ELIMU YAKO IMEKUKOMBOA AU NDO IMEKUFANYA UWE MJINGA?

Nawakilisha.
 
yule jamaa aliyekuwa naibu waziri wa tanesco sijui malima ndiyo zake,utakuta yupo kijijini kwa watanzania wasiojua lolote kuhusu kingereza lakini utasikia akimwaga kiinglishi huku akinyanyua mavidole yake yaliyojaa mipete mikubwa mikubwa,,ovyo kabisa mkuu
 
Niujinga tu,wanasumbua na vizungu vyao vya inglishi kozi, ndo maana kwene nafasi za kugombea ubunge wa afrika mash walijinyeanyea sana walipokua wanajinadi kwa kiinglishi lakin uwakute nje wanajifanya kuchanganya changanya
 
Kama walengwa wanakuelewa sidhani kama kuna shida, ugumu huja pale unapochanganya lugha kwenye kadamnasi itumiayo lugha ya aina moja tu.
 
Kuna watu wanatabia ya kuongea kizungu au wanachanganya changanya kiswahil na kizungu ili tu waonekane wajanja au wasomi au tu kupenda sifa. anaona ataonekana mshamba akiongea kiswahili moja kwa 1,kumbe ni ujinga mtupu wenzetu wachina wakienda nchi yoyote hua wanaongea lugha yao nyie mnawaona kama awajasoma,kujua kizungu sio usomi kuna nchi watu wake wanatumia kiingereza bado utakuta wanakabiliwa na tatizo la watu kutojua kusoma na kuandika. HUO NI UTUMWA KUSHOBOKEA LUGHA YA WATU,JE ELIMU YAKO IMEKUKOMBOA AU NDO IMEKUFANYA UWE MJINGA?

Nawakilisha.

Ujumbe Mzuri sana,UNAWAKILISHA WAPI?
 
Na wengi wao wa tabia hiyo wakiambiwa waongee kuzungu mojakwamoja hawawezi...yaani hata hawawezi kazi kutubwatukia tu...
Kuna watu wanatabia ya kuongea kizungu au wanachanganya changanya kiswahil na kizungu ili tu waonekane wajanja au wasomi au tu kupenda sifa. anaona ataonekana mshamba akiongea kiswahili moja kwa 1,kumbe ni ujinga mtupu wenzetu wachina wakienda nchi yoyote hua wanaongea lugha yao nyie mnawaona kama awajasoma,kujua kizungu sio usomi kuna nchi watu wake wanatumia kiingereza bado utakuta wanakabiliwa na tatizo la watu kutojua kusoma na kuandika. HUO NI UTUMWA KUSHOBOKEA LUGHA YA WATU,JE ELIMU YAKO IMEKUKOMBOA AU NDO IMEKUFANYA UWE MJINGA?

Nawakilisha.
 
Ila kuongea kiarabu ndio ujanja? salamalekum, bismillah, alhamndulilahi, kwani haya maneno hayana mbadala wake kwa kiswahili?

yani apa swala ni kuleta lugha ya kigeni tofauti na lugha yako ya asili haijalishi ni kiarabu,kijapani au kifaransa!
 
Niujinga tu,wanasumbua na vizungu vyao vya inglishi kozi, ndo maana kwene nafasi za kugombea ubunge wa afrika mash walijinyeanyea sana walipokua wanajinadi kwa kiinglishi lakin uwakute nje wanajifanya kuchanganya changanya

Sasa wewe unawasema watu wengine wakati huo huo unafanya kosa lile lile! Ni kweli hampendi watu wachanganye kiingereza na kiswahili au ni wivu wenu tu wa kotojua kiingereza!
 
Unachozungumza ni kweli lakini unapaswa kufahamu kuwa dunia hivi sasa ni kijiji na athari zake moja wapo ni hiyo.
Wachina ambao lugha yao haina hata chembe cha uingereza hivi sasa imeanza kuingiliwa na lugha za kigeni kutokana na wototo wao ambao sasa ni wakubwa wanaathiri lugha.
Hata hapa nchini wacha kutumia lugha mchanyiko lakini kiswahili fasaha huzungumzwa na wachache sana lugha za kimjinini/mitaani zimeingia kwenye anga za radio magazeti na ni vigumu kudhibiti kutokana na kukubaliwa na vijana wengi.
vilevile ufahamu kwa wale ambao wametumia muda wa miaka mingi kukaa madarasani mchanganyiko wa lugha huja bila kutarajiwa.
Hivyo kama unataka kuanzisha kampeni tuanze na kuzungumza na kuandika kiswahili sanifu
 
Sasa wewe unawasema watu wengine wakati huo huo unafanya kosa lile lile! Ni kweli hampendi watu wachanganye kiingereza na kiswahili au ni wivu wenu tu wa kotojua kiingereza!

kuweka ayo maneno ambayo we unaona nimechanganya lugha ni kuweka msisitizo ili nyie mnaojifanya mnajua kizungu muelewe,ivi kwa kichwa chako kilivo na akili fupi ka maisha ya funza unaamini kua kuna mtu anaona wivu wa wewe kujua kizungu,kizungu chenyewe unachodai unajua cha ugoko kimejaa ukakasi!

samahani kama nimekuudhi.
 
Kuna watu wanatabia ya kuongea kizungu au wanachanganya changanya kiswahil na kizungu ili tu waonekane wajanja au wasomi au tu kupenda sifa. anaona ataonekana mshamba akiongea kiswahili moja kwa 1,kumbe ni ujinga mtupu wenzetu wachina wakienda nchi yoyote hua wanaongea lugha yao nyie mnawaona kama awajasoma,kujua kizungu sio usomi kuna nchi watu wake wanatumia kiingereza bado utakuta wanakabiliwa na tatizo la watu kutojua kusoma na kuandika. HUO NI UTUMWA KUSHOBOKEA LUGHA YA WATU,JE ELIMU YAKO IMEKUKOMBOA AU NDO IMEKUFANYA UWE MJINGA?

Nawakilisha.

Hii ni kazi kuliko kwenda kazini!
 
kuweka ayo maneno ambayo we unaona nimechanganya lugha ni kuweka msisitizo ili nyie mnaojifanya mnajua kizungu muelewe,ivi kwa kichwa chako kilivo na akili fupi ka maisha ya funza unaamini kua kuna mtu anaona wivu wa wewe kujua kizungu,kizungu chenyewe unachodai unajua cha ugoko kimejaa ukakasi!

samahani kama nimekuudhi.
Hata kiswahili kinakushinda neno ayo ndiyo nini? sasa kama lugha yetu ya kiswahili inatushinda lugha za wenzetu tutaziwezaje????
Ninadhani kwanza tuanze humu jamvini kwa kutumia kiswahili sanifu.
 
code mixing hakuna mtu ambaye anaweza kuongea kiswahili mwanzo mwisho bila kuchanganya kingereza awe anajua kingereza au hajui yani lazima uweke maneno ya kingereza tu.
Ila tatizo kaa pale mlimani city uone hasa mabinti utadhani hawajui kiswahili ni kingereza kwa kwenda mbele.
 
kuweka ayo maneno ambayo we unaona nimechanganya lugha ni kuweka msisitizo ili nyie mnaojifanya mnajua kizungu muelewe,ivi kwa kichwa chako kilivo na akili fupi ka maisha ya funza unaamini kua kuna mtu anaona wivu wa wewe kujua kizungu,kizungu chenyewe unachodai unajua cha ugoko kimejaa ukakasi!

samahani kama nimekuudhi.
Kuna kitu kama chuki hapa!!mchanganyiko na wivu+hasira, mbonsafo mwoli.
 
Kisha tuendelee na mtandao wetu huu!!jamii nimeielewa ila hiyo FORUM ndio bado!!eh sorry nimekosea tena,ngoja nikanywe guinness kwanza ohoo samaanini wajameni!ile pombe nyeusi!sjui inaitwaga beer au bia,hivi ni soksi au sox?skirt au sketi?lorry au lori?naenda car wash,niende klabu,nikachukue namba(au number)mi ntakuwa nakosea tu mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom