Kuondolewa kwa pesa za kufanyia mtihani wa taifa kidato cha nne

mark mayalla

Member
Oct 3, 2010
7
6
Hivi kweli kuna humuimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kulipia pesa za kufanyia mtihani wao wa kuhitimu? serikali inataka mwanafanzi wa kidato cha nne kulipia 35,000/= kama pesa ambayo itamuwezesha kufanya mtihani wake wa kidato cha nne. embu tu jaribu kuvuta taswira mtanzania huyu ni yule anayepokea mshaara wa kima cha chini kwa mwezi yaani 60,000/= kwa mwezi. ukitoa gharama za chakula na bill ndogo ndogo za hapo nyumbani tutakuja kukuta pesa hii haimtoshelezi mzazi huyu kumlipia mwanafunzi hela ya kufanyia mtihani.

wakaona haitoshi ata kuongeza riba ya shilingi 15,000/= kwa mwezi kwa wale wasiofikisha pesa hizo mapema. sasa tunakuja kuona ni wanafunzi wengi wenye uwezo mzuri ambao watashindwa kufanya mtihani kwa ajili ya pesa hizo.. kwani serikali haiwezi kumudu kitengo cha elimu ata wanafunzi wakafanya mtihani wao bure? wanaweza wakasema serikali haina hela lakini hiyo hiyo serekali ambayo haina hela imeweza kuongeza posho za wabunge na kuwawekea wabunge mafuta ya zaidi ya 35,000/= kwa siku katika magari yao ya millioni mia mbili lakini wakashindwa kuondoa ela ya kufanyia mtihani yaani 35,000/= kwa mwaka.

kwa mimi binafsi naamini serekali inaweza kuziondoa fedha izo kama mkazo wa kampeni za kuondoa pesa hizo ukiimarika. maana pesa hizo zinawanufaisha watu wachache na kuangamiza wanafunzi wengi wa kidato cha nne ambao wangeweza kulisaidia taifa na kukuza uchumi wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom