Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,129
- 18,743
Nadhani Chadema wanajua wazi kwamba Lowasa alihamia Chadema si kwa kuwa alikubaliana na sera za Chadema dhidi ya CCM, bali kwa kuwa aliona nafasi ya kuwa raisi wa Tanzania kupitia Chadema. Na Chadema (au Mbowe) hawakumkubali Lowasa kwa kuwa walimpenda, bali walimwona kama tiketi yao ya kushika uongozi wa nchi. Kumbuka wakati fulani JK alitishia kuhamia Chadema kama Mkapa asingempitisha kuwa mgombea uraisi wa CCM mwaka 1995. Kwa hiyo hili linaeleweka.
Lowasa "alishindwa" na Magufuli katika uchaguzi mkuu uliopita. Lakini Lowasa alionyesha kila dalili ya kutaka tena kuwa mgombea wa Chadema kwenyeuchaguzi mkuu ujao. Watu kama kina Lissu na wengineo hawakuwa tayari kuruhusu Lowasa apewe tiketi ya Chadema safari hii. Mbowe aliambiwa tulikukubalia kwa shingo upande uchaguzi uliopita, safari hii hatutaki.
Kisha akaingia LIssu. Jaribio la kumuua kama lilikuwa na lengo la kummaliza, sasa limempaisha kisiasa, ndani na nje ya nchi. Lissu sasa anatambua kwamba it is now or never kushindana na Magufuli uchaguzi ujao, na wengi wanakubaliana nae. YUpo Sumaye, lakini watu wanamwambia wazi nyota inayowaka kwa sasa ni Lissu.
Ndipo Lowasa alipotambua hana lake tena Chadema. Atafanya nini? Atakuwa nani? New kid on the block ni LIssu. Akaona ni bora arudi CCM ambako angalau ataheshimika na kna kuenziwa kama Waziri Mkuu mstaafu, heshima ambayo hakuipata kikamili alipokuwa Chadema.
Nimejifunza jambo moja kuhusiana na siasa za CCM. Hakuna mpinzani mbaya, bali wote ni watu wazuri na wenye hekima na wenye mawazo mazuri sana. Ubaya wao ni kwamba wako upinzani. Wakirudi CCM ghafla wanabadilika na kuwa watu safi wanaotakiwa kuheshimiwa sana. Yale matusi, kebehi na kashfa zote wanazofanyiwa wakiwa upinzani ni siasa tu, sio ukweli.
Kwa hiyo sasa njia ni nyeupe kwa Lissu. Magufuli jiandae. Na ukweli ni kwamba CCM wasipoangalia, na wasipotumia bao la mkono, Lissu anaweza kuwashangaza watu.