Kuondoa weusi katikati ya mapaja na kwapa

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,105
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,105 2,000

KUONDOA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA NA KWAPA

Leo wapendwa nataka kuongelea jambo ambalo linasumbua sana wanawake sio kwamba wanaume wao hawana bali hawalichukulii kiundani sana kama sisi wanawake linavyotusumbua, weusi katikati ya mapaja najuwa wanawake hapa wenye tatizo hili wamesema kweli kabisa..

Weusi huo wanawake tunao sana kwasababu ya jasho katikati ya mapaja maana kutwa yanagusana kwa kuvaa sana skirts na vitu vingine vingi vinavyofanya mapaja kuwa meusi labda hata mimi sivijui utafanyaje kama na wewe mapaja yako yapo hivyo..utatumia mafuta ya nazi

Ndio mafuta ya nazi ndio dawa ya kusafisha huo weusi ukishaoga asubuhi, mchana na jioni unayapaka kwenye mapaja ndani ya mwezi bila kuacha hata siku moja utaona huo weusi wote unapotea kabisa.
Kama hukulijuwa lako hilo beba na baba mpe na mkeo pia ukirudi nyumbani

NJIA 3 ZA ASILI ZA KUONDOA WEUSI KATIKA MAPAJA NA MAKWAPA.
Inner thighs/mapaja ya ndani na makwapa hutokea weusi kutokana na msuguano wa ngozi kwasababu ya mapaja kugusana, hata ngozi iliyokauka pia inaleta weusi katika ngozi.
Hivyo nimekuletea njia natural ya kuondoa weusi huo bila kutumia madawa makali.

1. TUMIA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU.
Mafuta ya nazi yanatumikakulainisha ngozi lakini unaweza kutumia pia katika kuondoa weusi ukichanyanya na ndimu..fata step hizi::
Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu nusu
Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama unafanya massage kwa dakika 15.
Kisha osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.

2. TUMIA MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU.
Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi katika mapaja na makwapa, fuata step hizi::
Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko kimoja cha sukari.
Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari ipotee.
Acha ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.

3. GANDA LA CHUNGWA NA ASALI
Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia unaondoa weusi. Fuata step hizi::

Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali
Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15
Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.
 
Joseverest

Joseverest

Verified Member
Joined
Sep 25, 2013
Messages
42,776
Points
2,000
Joseverest

Joseverest

Verified Member
Joined Sep 25, 2013
42,776 2,000
Wahusika watakuja...umewapa somo zuri
 
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Messages
13,486
Points
2,000
Adharusi

Adharusi

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2012
13,486 2,000
Je na ule weusi wa kwenye kinena, unaondolewa na nini maana unafanana na katika kwapa, Mi nilizani sababu ya kunyoa
 
culture gal

culture gal

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2017
Messages
6,924
Points
2,000
culture gal

culture gal

JF-Expert Member
Joined May 24, 2017
6,924 2,000
Nadhani ni Limao sio ndimu....

Lakini pia mtu anaweza kuchukua BAKING SODA na LIMAO akasugulia sehemu husika kama makwapani, mapajani, kwenyw vidole vya mikono na miguu.
baada ya kunawa akapaka Mafuta ya nazi.

Kiazi mviringo pia kinaondoa weusi akikate tu kipande na kuanza kusugua hata wale wenye madoa ya chunusi inawahusu hii.

Acha kutumia yale ma deodorant (sijui kama nimepatia spelling. lol) na pafyum kali zenye alcohol huleta sanaaaaa weusi.

Good Luck.
 
mwamgongo

mwamgongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
481
Points
500
mwamgongo

mwamgongo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
481 500
Mafuta ya Nazi kwa weusi ni nouma sana hii.
 
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Messages
10,495
Points
2,000
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2014
10,495 2,000
Hivi ndimu ni tofauti na limao?
 
Word

Word

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2016
Messages
1,413
Points
2,000
Word

Word

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2016
1,413 2,000
Aiseee hii haihusu yale mauweusi kwenye mashavu ya ndevu aiseee????
 
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
33,609
Points
2,000
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
33,609 2,000
ila ujue kuna wengine ngozi zao ni ngumu hata uloweke kwenye mafuta ya nazi au malimao, shida iko palepale.....
 
V

Veronica Peter

New Member
Joined
Sep 25, 2018
Messages
1
Points
20
V

Veronica Peter

New Member
Joined Sep 25, 2018
1 20
Asanteh saana maana hli ttzo ni la wanawake weng daah
 
mapipando

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
2,819
Points
2,000
mapipando

mapipando

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
2,819 2,000
Kuna wengine weusi umezidi kiasi kwamba ukiona tu mshedede unanywea nywiiiiii halafu unaonekana huna nguvu za kiume shubaaaaaamit.
 

Forum statistics

Threads 1,326,733
Members 509,585
Posts 32,232,777
Top