Kuondoa mzizi wa fitna waziri Lukuvi tupimie viwanja kwenye hizi heka 1,500 za Kigamboni

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,451
29,128
Heshima yako Waziri,

Sitaki kuingilia sana kwenye Mchakato wa Ubatilishwaji wa Ugawaji wa Heka 1,500 alizotoa Bwana yule wa Azimio Estate sababu yaliyotokea yanajulikana tayari hivyo tugange yajayo.

Mi Ushauri au ombi langu kwako Mh. Waziri mwenye dhamana ya Ardhi yetu ni kutupimia viwanja lile eneo. Nimejaribu kupiga hesabu kadhaa nikaona kama ukipima viwanja palem basi angalau kaya 7,000 zinaweza kupata eneo safi kabisa lililopimwa na serikali kukawa hakuna longo longo.

Heka 1,500 x Sqm 4046.86/heka = Sqm 6,070,290 jumla ziko pale. (Ref how big is an acre in meter - Tafuta na Google)

Sasa tufanye katika hizi Sqm 6,070,290 zilizoko pale, tunatoa miundombinu ya Barabara, Makaburi, Open Space, Market, etc ambayo ni kama 20% hivi, so itabaki Sqm 4,856,232 kwa ajili ya viwanja tu,

Kawaida viwanja hua vina ukubwa mbali mbali, kuanzia Sqm 400 labda na kuendelea lakini for the purpose of calculation here, tutumie kiwakilishi cha Sqm 700 kwa kila kiwanja kama average. Katika zile Sqm 4,856,232 zilizobaki ukigawa kwa Sqm 700 ya kila kiwanja kimoja unapata Viwanja 7,000 kwa kukadiria.

Huu utakua mradi mkubwa, sawa na ule wa Kibada au Gezaulole, na pia kwa serikali itakua ni chanzo kingine cha mapato kwa serikali. Pia itaondoa figisu figisu za eneo lile ambalo tayari limeanza kunyemelewa na matapeli. Nimeonelea mradi wa Vinja sababu Mkoa Mzima wa Dar es Salaam una uhaba mkubwa viwanja lakini Wilaya Mpya ya Kigamboni ndio yenye maeneo mengi makubwa yaliyoko wazi.

Ushauri wangu ni huo tu Mh. Waziri.
 
Tatizo bwana Azimio anazo zaidi ya hizo 1500 hapo. Inabidi arudishe zote kwanza. Sio kujisafisha kwa kumgawia Bashite kidunchu ili nyingine ziwe halali
 
Back
Top Bottom