Kuondoa matumizi ya nguvu na gharama kuua Upinzani nchini, Bunge litengeneze Sheria hizi

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,520
17,426
1. Vyama vyote vya siasa ni mali ya serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo Nchi ina jukumu la kuvilea, kuvilinda na kuvipa nafasi ya kushiriki kazi za kimaendeleo ya nchi kwa ujumla.

2. Baraza la usalama na Deep state Viwe na jukumu la kuweka mfumo wa uongozi wa kila chama na uteuzi wa viongozi kwenye kila chama kabla ya kupigiwa kura na wananchi kwa kuzingatia uzalendo na uwajibikaji wa wateuliwa ili kuepuka mapandikizi na viongozi wasio wazalendo.

3. Iwepo Tume huru ya uchaguzi ili kufanya Demokrasia halisi ambayo itatamalaki nchini Bila hofu ya watawala kwa kuwa wateuliwa kugombea wamekidhi vigezo vya uzalendo kutokana na mchujo uliofanyika kuwapata kutoka namba 2 hapo juu.

4. Raisi aliye madarakani awe chini ya uangallizi wa Baraza la usalama wa taifa na Deep state na sio kua top wa kila kitu. Itasaidia kudhibiti madaraka yake hata kuondolewa madarakani kama atakiuka sheria na maono ya Taifa letu ili kuleta mamlaka ya kumwajibisha Rais aliepo madarakani kuepuka migogoro na kuvuruga umoja wa kitaifa.

Angalau haya yakifanyika yataepusha jeshi letu kutumika ovyo kutishia uhai wa vyama vingine na harakati za siasa nchini kama ilivyo sasa hivi!
 
Kwani wale polisi wamarekani wanaoheshimu maoni ya watu wengine bila kuegama kwenye chama dola wanaendeshwa na katiba ipi?
 
Haya niliyoyaandika hapa yakiwekwa kwenye katiba mpya nakwambia Tanzania itakua nchi bora kabisa Duniani tena Bora ya kuigwa ya mfano!!
 
Kwani wale polisi wamarekani wanaoheshimu maoni ya watu wengine bila kuegama kwenye chama dola wanaendeshwa na katiba ipi?
Kuna ustaarab zamani ukiitwa wa Panzi,wenzetu wastaarabu wanajali Katiba yao na imeandikwa kuzingatia mahitaji ya jamii zao na kila moja anaishimu ila wastaarabu wa panzi wanakuambia wananchi hawahitaji katiba mpya bali maji,barabara na zahanati/hospitali.Wanalazimisha kuwa katiba mbadala wake ni huduma za kijamii.Aibu yetu.
 
1. Vyama vyote vya siasa ni mali ya serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo Nchi ina jukumu la kuvilea, kuvilinda na kuvipa nafasi ya kushiriki kazi za kimaendeleo ya nchi kwa ujumla.

2. Baraza la usalama na Deep state Viwe na jukumu la kuweka mfumo wa uongozi wa kila chama na uteuzi wa viongozi kwenye kila chama kabla ya kupigiwa kura na wananchi kwa kuzingatia uzalendo na uwajibikaji wa wateuliwa ili kuepuka mapandikizi na viongozi wasio wazalendo.

3. Iwepo Tume huru ya uchaguzi ili kufanya Demokrasia halisi ambayo itatamalaki nchini Bila hofu ya watawala kwa kuwa wateuliwa kugombea wamekidhi vigezo vya uzalendo kutokana na mchujo uliofanyika kuwapata kutoka namba 2 hapo juu.

4. Raisi aliye madarakani awe chini ya uangallizi wa Baraza la usalama wa taifa na Deep state na sio kua top wa kila kitu. Itasaidia kudhibiti madaraka yake hata kuondolewa madarakani kama atakiuka sheria na maono ya Taifa letu ili kuleta mamlaka ya kumwajibisha Rais aliepo madarakani kuepuka migogoro na kuvuruga umoja wa kitaifa.

Angalau haya yakifanyika yataepusha jeshi letu kutumika ovyo kutishia uhai wa vyama vingine na harakati za siasa nchini kama ilivyo sasa hivi!
Kuua upinzani sio rahisi labda kuua vyama vya upinzani
 
Back
Top Bottom