Utaratibu wa kufuata ili kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mazungumzo binafsi

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,627
3,570
Wadau nimeandaa safari ya kwenda kuonana na Rais JMT hata nahitaji nikaonane naye ana kwa ana nifanye naye mazungumzo kama raia wa kawaida kijana mpenda maendeleo.

Watu wengi sana wamekuwa wakienda Ikulu lakini hao ni wale wenye channel.

Je, kwa mimi nisiye na channel ama kujuana na yoyote mkubwa nifanyaje?

Msaada wadau nipo serious.
 
Hana matatizo omba apointimenti na ueleze unayotaka kwenda kuongelea
 
Watu wengine bwana,,hapa tu una kitete,,unajua kabla hujaonana nae,lazima uhojiwe na wale watu mule karibia wote ni tiss,jipange kisha kaombe appointment kwa katibu wake yeyote,,,
 
Vaa bullet proof ya tindikali, na pia uwe bubu ukionana naye kwani ukiongea kwa hasira kuna uwezekano mkubwa ukapotea hapa duniani.
 
fanya appointment kwangu. wasiliana na mim kama unataka kumuona. ni pm.ila uwe tayari kujibu maswali yote vizuri kabla atujakupa vibali
 
Wadau nimeandaa safari ya kwenda kuonana na rais lakin sio kama mjomba(mpoto) hata nahitaji nikaonane naye ana kwa ana nifanye naye mazungumzo kama raia wa kawaida kijana mpenda maebdeleo.

Watu wengi sana wamekuwa wakienda ikulu lakini hao ni wale wenye channel je kwa mimi nisiye na channel ama kujuana na yoyote mkubwa nifanyaje? Msaada wadau nipo serious.

NINGEFANIKIWA KUMUONA RAIS NINGEMUELEZA HUU UOZO WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE:
[h=2]Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Kigamboni kinafilisika?[/h]Kwa sasa Wafanyakazi wametangaziwa na Uongozi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kupitia wakuu wa idara kuwa kuanzia mwezi wa saba 2013 waanze kufunga mikanda maana mishahara wa mwezi wa saba utatoka tarehe za mwezi wa nane. Pia pesa za nyumba, usafiri, likizo na posho ya saa za ziada haitakuwepo hadi ada za wanafunzi ipatikane mwezi wa kumi 2013. Pia pesa za kusimamia na kusahihisha mitihani na kusimamia utafiti kwa wanafunzi hawajalipwa walimu. Haieleweki kilichotokea maana fedha hizi zinatakiwa ziwe zimewekwa kwenye bajeti ya mwaka husika. Mkuu wa Chuo Dr. Magoti yuko bize kumalizia nyumba yake huko Bunju ili ahame kutoka nyumba yake ya Kigamboni atakapo maliza mkataba wake wa mwisho mwezi wa desemba 2013.

Shilingi milioni 680 za mapato ya ndani ya Chuo zimetumika kukarabati nyumba ya mtu binafsi huko Zanzibar kwa ajili ya hosteli ya wanafunzi. Matumizi haya mabovu ya fedha za walipa kodi ndio moja ya sababu ya Chuo kufilisika. Bodi ya Chuo imefichwa ukweli huo na hata kamati ya huduma za jamii ya Bunge ilipotembela Tawi la Chuo Zanzibar na kugundua ubovu wa kuvuja kwa jengo lililojengwa kwa mamilioni ya shilingi walifichwa ukweli wa ukarabati wa nyumba hiyo ya mtu binafsi kuifanya hosteli. Jengo lile bovu lililozinduliwa hata baada ya Kamati ya Bunge kuzuia uzinduzi wake ambapo ililalamikiwa Bungeni, hata ile asilimia 10 inayobakizwa hadi baada ya mradi kwisha kumbe nayo ilishalipwa lakini imefanywa siri kwa Uongozi wa Chuo bila Bodi ya Chuo wala Kamati ya Bunge kujulishwa ukweli. Kiburi hiki cha Uongozi wa Chuo hiki haijulikana kinatokana na nini maana imeshasemwa sana lakini hawasikii la mtu hata wanawadharau wawakilishi wa wananchi. Inasikitisha kweli kwa jeuri hii ya viongozi hawa wasio na aibu kwa jeuri yao ya kuwahonga kila wanaochunguza maovu yao.


BAADHI YA MALALAMIKO YA NYUMA NI KAMA IFUATAVYO:

USIACHE KUISOMA YOTE:
DK: MAGOTI MKUU WA CHUO CHA NYERRE NA BWANA LWAMBANO NI MAFISA


WANAKIUA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE SASA KIMEKUWA CHUO CHA KUMSAHAU NYRERRE. RAIS KIKWETE ALIKOSEA KUMPA MKATABA MAGOTI BAADA YA KUSTAAFU ALIPEWA MKATABA WA MIAKA 5, AKAMALIZA AKAPEWA WA MIKA 2 KWAKUWA NI KADA... WA CCM DIKTETA.

TAARIFA AMBAYO IMETUMWA NA WAFANYAKAZI WA CHUO KWA WAZIRI MKUU PINDA, POLISI NA TAKUKURU MPAKA SASA HAIJAFANYA CHOCHOTE.

Mzee aliongezewa mkataba Ijumaa,jumamosi ujenzi wa hosteli uliokuwa umekwama chuoni ukaanza,tupo walimu tunaodai madeni tunaambiwa pesa hakuna ila kuna pesa ya kumwagilia miti dawa MILIONS ZA PESA ETI KUUWA WADUDU ,watu wanakula tu MATUMBO KAMA PIPA.

MAGOTI NA LWAMBANO WANAASTAHILI KUFUKUZWA KAZI. HOJA HIZI HAPA

1.LWAMBANO alimuunganishia ajira ndugu yake ERASTO MHAGAMA anaejua fika kuwa anatumia vyeti vya KENETH MAPUNDA nakumpeleka kusomeshwa na serikali MBA mlimani,alipomaliza tu akapandishwa cheo tofauti na wafanyakazi wengine ambao tupo chuoni na MBA ZETU miaka hatujapandishwa, mbali na hivyo kabla ya miaka 2 ya kisheria kupita akapelekwa kusoma PhD na mshahara wake wa zaidi ya milioni 1 na nusu akilipwa.

Tulipiga sana kelele tukapuuzwa baada ya gazeti kutishia kuandika > MAGOTI AKAMSHUSHA CHEO NA TULIPOZIDI KULISEMEA HAKUCHUKUA HATUA BADALA YAKE TUNAAMBIWA ERASTO KAAMUA KUCHA KAZI.WAKATI ALISOMESHWA NA NA ALIKUWA AKILIPWA MSHAHARA HUO MKUBWA : MAGOTI NA LWAMBANO WAMEITIA HASARA SERIKALI WANASTAHILI KUFUNGWA JELA.

2.NGONO: WAPO WALIMU WANAOA HAPA CHUONI BILA KUFATA SHERIA YA MIAKA 2, PIA MWALIMU BUKUKU, MALIGANYA NA KIHOYI PAMOJA NA DAKTARI WA CHUO WANAJULIKANA FIKA KWA KUDAI NGONO KWA WANAFUNZI WA KIKE ,HILI LIMESEMWA SANA NA MWALIMU BUKUKU ALIKAMATWA NA SAUTI YAKE ILIYOREKODIWA IKIDAI RUSHWA NA NGOGO KWA mwanafunzi alierudishwa mwaka, mwanafunzi aliandaa mtego na kutuma elfu 90 kwa Mpesa na mwalimu alimuita Kimara Korogwe akidai ngono ili mwanafunzi aendelee na masomo,baada ya suala hilo kulipuliwa na mwanachuo ambae kwa sasa KAFUKUZWA CHUO NA AMEKISHTAKI CHUO ambapo chuo kimemlipa wakili milioni 10 huku wakijua wanaficha ukweli , MWALIMU BUKUKU alisimamishwa kwa wiki 1 tu kwa kosa hilo la kudai NGONO na kutetewa na mpenzi wake mjumbe wa bodi BI: SARAH MWAKYAMBIKI ambapo ushahidi wa sauti kwenye memory card ulipotezwa mbele ya Mr Mushi aliekuwa naibu mkuu wa Chuo hijapokuwa bado tunao kwenye laptop na tutauweka mitandaoni siku zijazo .

Baada ya mambo kulipuka mwanafunzi aliekuwa ameambiwa arudie mwaka wa masomo aliitwa aendele na masomo yake na mwalimu akimwambia kuwa utaona tu,akarudishiwa pesa zake na alizotuma kwenye simu kwa lazima na aliekuwa mkuu wa idara ya jenda mzee wa miaka 75 bila kustaafu mzeee CHAMRIHO na mwaka huu amefelishwa tena na kuambiwa arudie mwaka ILI wathibitishe kuwa mwamafunzi alifeli kweli jambo ambalo mwenyewe analikataa .

DK MAGOTI ANALIJUA HILI YUPO BIDHE NA MKTABA WA UJENZI WA HOSTELI.

MWALIMU KIHOYI (MDAI NGONO MKUBWA KWA WANAFUNZI WAKIKE) SASA KAPANDISHWA CHEO NA KUWA MKUU WA IDARA YA UALIMU AKIWA NA MASTERS YAKE. MAGOTI ANAJUA KUWA CHUO KIZIMA HAKUNA MTU MWENYE PHD, NA ANAHOFIA KUWA WATACHUKUA NAFASI YAKE .

3.BWANA MAGOTI ANAJUA FIKA KUWA SERIKALI HAIRUHUSU KUMUAJIRI MTU AKIWA NA MIAKA 40,MAGOTI AMEMUAJIRI LWAMBANO KWA MIKATA HEWA AMBAE TAYARI ALIFUKUZWA KWA UFISADI KWENYE TAASISI YA KAHAWA NA CHAI, BWANA HUYU AMEAJIRIWA CHUONI MWAKA 2004 AKIWA MZEE TAYARI NAKULIMBIKIZIWA VYEO, LWAMBANO NDIO MSAJILI WA CHUO,YEYE NI MJUMBE WA BODI,YEYE AMEPEWA PIA CHEO CHA MUHADHIRI (LECTURER) AKIWA NA MASTERS TU wakati walimu wengine wote wanalipwa kama asistance lecturer.

LWAMBANO ANAMILIKI MALI NYINGI NA SASA AMENUNUA SHAMBA RUFIJI AMBAPO KILA WIKEND ANATUMIA MAGARI YA CHUO CHA UMMA KWENDA SHAMBANI KWAKE. MAGOTI ANATUMIA MAGARI YA UMMA YAENDE NYUMBANI KWAKE KUCHOTA MAJI. UFISADI HUU NDIO UMEMSABABISHA ALIEKUWA NAIBU MKUU WA CHUO KUKATAA KUENDELA NA NAFASI HIYO,NA MAGOTI KUMTEUWA MWALIMU AMBAE ANAWEZA KUWA KIBARAKA WAKE KUKAIMU.

4.DK MAGOTI KWAKUJUA SERIKALI IMEKATAZA KUCHAGISHA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WANAFUNZI WA SEKONDARY NA VYUO WALIOJIUNGA NA BIMA YA AFYA ,ALIWACHANGISHA ZAIDI YA WANACHUO 300 TANGU MWAKA 2010 HADI 2012 LAKI 1 KILA MWAKA MPAKA JUZI TU ALIPOLAZIMISHWA NA MGAZETI, JE FEDHA ZA WALIOCHANGISHW A AWALI MAGOTI UNAZIRUDISHA LINI? MAANA MATUMIZI YAKE HAYAJULIKANI NA WANACHUO HAWAKUSHIRIKISHWA.

CHUONI HAKUNA HOSPITALI BALI ZAHANATI YA VYUMBA 3 NA INA DAKTARI 1 TU,DAWA MNAPEWA NA SERIKALI NA TABIBU ANALIPWA NA SERIKALI FEDHA HIZO MAGOTI UMEPELEKA WAPI??

MAGOTI UNAJUAFIKA KUWA VYUO VYA UMMA VINATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA, ILI WANAFUNZI WACHANGIE ELFU 54 KWA MWAKA NA SI LAKI 1 UNAYOWA TOZA SASA WANACHUO ZAIDI YA 1500, MAGOTI HAUTAKI ZAHANAT I YA CHUO KIJIUNGE NA MFUKO WA BIMA YA AFYA, KWAKUWA UNAJUA UNAKULA HIZO FEDHA, HUU NI WIZI, UMEINGIA MKATABA BINAFSI NA HOSP YA BURHANI JUZI ETI MWANACHUO AKIZIDIWA AENDE HOSP HIYO, KWANINI CHUO KISIJIUNGE NA BIMA YA AFYA NA WANACHUO WAKIWA LIKIZO WATUMIE BIMA HIZOO KUTIBIWA KWENYE HOSP ZAO ZA MIKOANI??? MAGOTI UNASTAHILI KUWA JELA . TUTAKUANDAMA KWA UKWELI HUU MPAKA UTAKAPOFUNGWA JELA.

DHAMBI YA UFISADI HAITA ACHA KUKUTAFUNA DK MAGOTI AMBAE KWA TAARIFA UNATETEWA NA MSAIDIZI 1 WA RAIS AMBAE ANAKUFANYA UNAONGEZEWA MIKATABA,KILA KITU KINAMWISHO MAGOTI UNASTAHILI KUWA JELA Dk John Magoti anakifilisi chuo cha Nyerere Kigamboni
HUYU MZEE ANA AMINIKA NA CCM KUFUNDISHA WATUMISHI WA CCM JE ATAWASAIDIA WaTUMISHI WA CCM?

NA amenunua vitabu 1200 kwa tsh milioni 97 mkuu wa maktaba alipomfuata nakutaka ufafanuzi kwanini kitabu cha tsh elf 20 kariakoo msambaza awauzie kwa tsh laki na elfu 20 alimwambia nyamaza na mpaka sasa bado anamshughulikia mkuu huyo wa maktaba

waziri mkuu pinda aliponmgea na watumishi tulitoa malalamiko yetu na hatua zikachukuliwa baada ya muda kidogo wale wote waliosema wakat wa waziri mkuu kikaon sasa mmoja mmoja anaacha kazi kwa vitisho

dk huyu amesha tumia zidi ya tsh milion 100 kwenda india kutibiwa macho

bwana lwambano wanaekula nae sasa anamafuso 8 na anafanyakazi chuoni kama mwajiri mkuu,leckcha na mwenyekiti wa zabuni kazi zote anajipa mwenyewe

SARA MWAKYAMBIKI AMBAE N MPENZI WAKE AMEMFANYA KUWA MKUU WA CHUO ZAZNBAR WAKATI HUO HUO SARA AKIMTETEA KWENYE BODI MWALIMU BUKUKU ALIETUHUMIWA MWAKA JANA KULA RUSHWA YA PESA NA NGONO ILI KUFAULISHWA WANAFUNZI MPAKA LEO MWALIMU HUYU ANATETEWA NA YUPO, SISI WALIMU WA ZAMAN HAPA TUNATENGWA SANA NA HUYU MZEE ANASEMA WAZI KUWA KTK NCHI HII HAKUNA WAKUMCHUKULIA HATUA
Mwalimu Nyerere College Inahujumiwa!
Kwa taarifa nilizozipata leo hii kutoka kwa wadau wa Mwalimu nyerere Memorial Academy ni za kusikitisha sana. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, mambo haya yanafanywa na vijana, ambao tulitegemea wangeleta mabadiliko na kusahau ile kasumba iliyokuwa ikishusha hadhi ya baadhi ya vyuo mbali mbali hapa nchini! Kinachotokea Mwalimu Nyerere ni kwamba kuna baadhi ya walimu wamesahau wajibu wao wa kuwasimamia wanafunzi wao ili kufikia malengo yao ya kitaaluma na badala yake wamejigeuza miungu watu.

Haya yametokea hivi karibuni pale wanafunzi wa kada mbalimbali walipohitajika kuandika ripoti zao za tafiti mbalimbali kama utaratibu unavyoeleza. Kinyume na matarajio, baadhi ya wanafunzi hasa wa kike ambao wasimamizi wao ni wanaume vijana kukutana na vikwazo mbalimbali. Wengine walitakiwa kupeleka ripoti hizo nyumbani kwa walimu nyakati za usiku. Waliokataa kufanya hivyo wamefikia hatua mbaya, hata kukataliwa kupokelewa ripoti zao na hivyo kuwepo uwezekano wa kurudia mwaka! Cha kushangaza, ni kwamba, hawa wanaofanya haya wengine wamesoma ndani na nje ya nchi, na wameona ni jinsi gani huko walimu walivyo committed na helpful kwa wanafunzi wao kama wao walivyosaidiwa kwa hali ya juu. Cha ajabu ni kwanini wanaamua kuwafanyia ushenzi kama huu watanzania wenzao.

Kuna mwalimu mmoja baada ya kufanya upumbavu kwa mwanafunzi mke wa mtu, mumewe akaamua kutia timu chuoni, mwalimu alipolazimishwa kuipokea ripoti ya mwanafunzi na mkuu wake akamwambia yule mwanafunzi amwite mumewe wasaishe wote,mwanafunzi alipoambiwa vile akaamua kufikisha malalamiko kwa mkuu wa yule mwalimu, ndipo akabadilishiwa msimamizi, ndipo yule mwalimu wa awali akamfuata huyu mwalimu na kumpa maelekezo kwamba, ahakikishe yule mwanafunzi anarudia mwaka ama yeye anaunja urafiki nae.
Majina ya hawa walimu wote ninayo, na kuna mengi yaliyofanywa hapo chuoni, ikihitajika tutayaweka hapa.

Sasa najiuliza, haya mambo mbona hayafanani na falsafa ya Mwalimu kama chuo kilivyobeba jina lake? Ama ndio hujuma za makusudi kukihujumu chuo hiki kwa malengo maalumu?
[h=2]Utata wa vyeti vya O-level na A-level vya Mosses Kusiluka wa Mwalimu Nyerere Academy[/h]
Kuna utata katika majina ya Mosses Kusiluka wa Mwalimu Nyerere na Dr.Mosses Kusiluka wa Ardhi University. Hili suala linafaa kuchunguzwa kwani Dr.Magoti wa Mwalimu Nyerere Academy ameoa nyumba moja na Prof.Kusiluka aliyekuwa DVC Academy wa OUT na ndio maana alimuajiri Mosses Kusiluka ambaye vyeti vyake vina utata/walakini. Dr.Magoti pia alimuajiri Erasto Muhagama aliyetumia vyeti vya kugushi na alipofichuliwa baada ya kumsomesha degrii ya pili alimshauri aache kazi baada ya TAKUKURU kuanza kufatilia. Kwa kuwa Serikali inahakiki vyeti ni vema kuanzia na hili na kuwawajibisha viongozi wa Mwalimu Nyerere ambao wanapeana kazi kindugu na kufumbia macho kughushi vyeti na ufisadi mbalimbali kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa. Nawasilisha kwa hatua za haraka.

[h=2]Ushauri wa kisheria kutokana na kuonewa na Uongozi wa Chuo cha Mwl Nyerere-Kigamboni.[/h]
Mimi ni mwanafunzi niliyesoma Chuo cha Mwl Nyerere, nimeandamwa baada kutoa ushahidi wa Mwl aliyeniomba rushwa ya ngono. Nilirekodi tukio lote kwa kutumia simu na hadi nina sms niliyomtumia hela mwl huyo fisadi, cha ajabu niligeuziwa kibao kwa Mwl huyo kutetewa na hawara wake ambaye alikuwa kama Mwl wa nidhamu. Yule Mwl alisimamishwa lakini baadaye alirudishwa kazini na kuja kuendelea kuniandama. Kwa tukio hilo lililonitokea sitadhubutu kumshauri ndugu yangu kusoma katika chuo hicho, uongozi wa chuo unatetea rushwa ya ngono na fedha kwa wanafunzi masomoni ni kitu cha ajabu katika taasisi ya elimu yenye jina la Baba wa taifa. Naomba msaada wenu ili tukomeshe tabia hii katika taasisi za elimu hapa nchini.


[h=2]Chuo cha Mwalimu Nyerere kuhamishiwa Tawi la Zanzibar hutumiwa kama adhabu?[/h]
Wabaya wa Uongozi wa Chuo huhamishiwa huko kama adhabu kwa kuwa wanahoji ufisadi unaofanyika. Hata kama watoto wako shule hupewa barua ghafla ya kutakiwa kuhamia Zanzibar mara moja. Kama unasoma huhamishiwa hiko ili ukwame kusoma ili ubaki palepale kielimu. Wafanyakazi wengine wamehamishwa kwa nia ya kuwapa adhabu na kuamua kuacha kazi. Chuo hiki hutangaza nafasi za muda kila wakati na imekuwa mradi wa wakubwa kupata posho ya vikao. Wadau karibuni kwa ushuhuda na kuchangia mada.

 
Kaaaaaa,,,,mdau wa mwalimu nyerere madai yenu mareeeefu,wewe nakushauri uwah KUMUONA JK,KABLA YA HUYU MTOA MADA,me nakushauri tu,kumbe hata wahadhiri wanalialia,nilidhan ni kwa sisi walimu wa nasari
 
Watu wengine bwana muanzisha mada bado hajajibiwa tayari watu wengine mmeingiza shida zenu kama ulikuwa na ya kuongelea juu ya chuo hicho si ungeanzisha thread yako!
 
Watu wengine bwana muanzisha mada bado hajajibiwa tayari watu wengine mmeingiza shida zenu kama ulikuwa na ya kuongelea juu ya chuo hicho si ungeanzisha thread yako!

umesoma mwanzo alipoanza? huyo mwanzisha mada ameshajibiwa, na mimi namjibu aandike tu hapa hiko anachotaka kumwambia j.k maana wasaidizi wake wanapita, au anataka akutane nae ampe na nauli? ila subiria mwaliko wa Eid unaweza pata chance ya kubadilisha mawazo.
 
Wadau nimeandaa safari ya kwenda kuonana na rais lakin sio kama mjomba(mpoto) hata nahitaji nikaonane naye ana kwa ana nifanye naye mazungumzo kama raia wa kawaida kijana mpenda maebdeleo.

Watu wengi sana wamekuwa wakienda ikulu lakini hao ni wale wenye channel je kwa mimi nisiye na channel ama kujuana na yoyote mkubwa nifanyaje? Msaada wadau nipo serious.

Kaongee na mbunge wako kama una la kuongea. Rais hawezi kuonana na kila mtu kwa mazungumzo binafsi. Hata uko marekani kila mtu hawezi kwenda kuzungumza na Obama. Upo?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom