Uchaguzi 2020 Kuona ni Kuamini: Je, Oktoba 28, utachagua nini kati ya unachoona kwa macho kitu cha ukweli kilichopo vs ahadi tupu? Msikilize Masanja Mkandamizaji...

Hapo hamkukutana kama unavyosema, ni location ilipangwa kukiwa na mpiga picha na muongozaji wa Tangazo kabisa.

Njaa ni mbaya sana.
 
Mkuu Pasco, hoja yako ni kuwa mwenye kitu cha kuonyesha ndiye achaguliwe.
Mimi ninasema CCM ina kitu cha kuonyesha, UMASIKINI.
Kwamba kwa miaka 60 tumebaki kundi la nchi masikini sana Duniani.
Tatu, hawa Wapinzani hawana cha kuonyesha ! kwa miaka 5 hawakupewa fursa hata ya mikutano.
Muda mwingi wametumia mahakamani , leo mnataka waonyeshe nini, karatasi za dhamana.
Angalia chuki ilivyojaa dhidi ya CCM pamoja na kuwa na vya kuonyesha. Wananchi wanaonyesha kuchoshwa na chuki nzito dhidi ya waendesha V8 na HardTop.
Mkuu Nguruvi3 , kitakachofanya CCM ishinde sio hayo majengo bali ni utekelezaji tuu wa ile kanuni ya kwenye Bible ya mwenye nacho, ataongezewa.

Hiyo unayoiona kama chuki, ni mijini tuu, decisive votes hazitoki mijini, wala msihadaiwe na nyomi za makundi ya watu kwenye kampeni, zile sio kura. Kura ziko vijijini na ndiko iliko CCM.

Je, huwa unajua Watanzania huwa wanachagua nini?
karibu mitaa hii
Licha ya CCM kuwa chanzo cha umasikini, ujinga, rushwa na ufisadi, kwanini CCM bado huwa inashinda chaguzi mbalimbali?

Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?!
P
 
Hapo hamkukutana kama unavyosema, ni location ilipangwa kukiwa na mpiga picha na muongozaji wa Tangazo kabisa.

Njaa ni mbaya sana.
Amini nakuambia, I was only a coincidence!. Mimi niko location na crews yangu, tukifanya Documentary ya maendeleo ya mkoa wa Njombe na yeye akifanya yale makitu yake, ikatokea tuu kukutana location moja.
P
 
Nimesoma heading tu, nikaamua kukoment bila kusoma kontenti maana najua umeandika ugoro.

Kwani 2015 alipochaguliwa Magufuli, ahadi zake zilikiwa zimeshaanza kutimizwa?

Kama tulivyomchagua Magufuli huku akiwa hajawahi kuahidi na kutimiza hapo kabla(maana hakuwahi kuwa Rais kabla ya 2015), ndivyo nitakavyomchagua Lisu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais lakini ambaye naona hatakuwa na serikali iliyojaa USHAMBA NA ULIMBUKENI WA MADARAKA.
Ikiwa mkongwe anawaza hivi Tanzania tuna safari ndefu sana kufikia uchumi wa kati.
 
Inawezekana mkashinda lakini ushindi wenu tayari umeshakuwa haramu.
Najua utafurahia haramu kwasababu tu ya kuzoea kula haramu
Mungu atawahukumu kwa hili.
Magufuli ni chaguo la Mungu, ushindi wake ni mipango ya Mungu, mambo ya haramu yaliletwa kwenye sheria ya Musa, Torati, Mwana wa Adamu alipokuja, alikuja kuikamilisha Torati kwa kufuta haramu na najisi nyingi, hivyo kubakiza najisi tuu za kile kimtokacho mtu na sii kiingiacho

Kama ulikuwa hujui kuwa Magufuli ni chaguo la Mungu, subiria October 28, utajua

Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani. Je, Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika
P
 
Mandela aliingia madarakani akiwa hajajenga hata mtaro wa kupitisha maji mtaani kwake, tena akiwa ametoka jela. Hao wazungu aliokuwa analazimisha kuwatoa walikuwa wamejenga mara elfu ya hivi vya Magufuli leo. Hivyo huo utetezi wako kwa Magufuli ni wa watu wenye uelewa finyu wa mambo ambao sikutegemea kwako. Ila sasa hivi unafiki ndio fashion ili utoboe sishangai unachofanya hapa.

Kwa taarifa yako hapo Magufuli hana jipya kwenye awamu yake ya pili iwapo atalazimisha kutangazwa mshindi. Ana miradi mikubwa miwili ya 15t yaani SG& SGR respectively. Na miradi hiyo miwili pekee hajafika hata mmoja robo, acha miradi mingine kama madaraja ya Busisi nk. Hivyo kwenye hiyo miradi hajafika hata nusu ya hela yaani 7t. Kwa hiyo ndani ya hiyo miaka mitano anapaswa kupata 10t+ ili kukamilisha miradi hiyo kwa 100%, kitu ambacho hataweza. Anasema umeme wa maji kwenye hilo bwawa lake utakuwa wa bei rahisi, mbona miaka yote ukiacha hivi karibuni tulikuwa tunatumia umeme wa maji, na bado bei yetu ilikuwa juu kuliko baadhi ya majirani zetu?

ukitaka mchague ww unayeamini yeye ndio alfa na omega ya maendeleo ya nchi hii. Sisi wengine hatumpi kura, na ikitokea mgombea wa upinzani akapita na yeye kuwa rais, asipeleke hayo maendeleo yake. Kisha baada ya miaka mitano afanye ulinganifu wa kiwango cha umasikini/utajiri huko alikopendelea na kule alipopasusia. Maendeleo yanaletwa na kodi za wananchi, na hata yeye akitoka atakuja rais mwingine anayejitambua, atasimamia kodi za wananchi kupata maendeleo na sio kutaka kusujudiwa.
Njaa hupunguza uwezo wa kifikiri msamehe bure.
 
Mayalla kwa usomi wako hautakiwi kuuliza swali la mwanafunzi wa shule ya msingi, mkoloni alikuwa hapa na alijenga reli, barabara na meli ziwa Victoria na Tanganyika, Nyerere wakati huo hakujenga hata kibanda cha kuishi yeye! Lakini watanzania walimchagua.
JF of GT's has lost GT's.
Mkuu elvischirwa , during Nyerere's era, was there an option to choose from? Si ni alikuwa Nyerere only!

Sasa Magufuli ndio kama Nyerere, mgombea aliyepo ni Magufuli tu!

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au ni Magufuli tu?
P
 
Pascal Mayalla NJAAA MBAYA SANA..NI WEWE UMEANDIKA AU?
MIAKA 60
DAR UMEME UNAKATIKA
MAJI YA KUNYWA NI ISHU
BADO MNAHUBIRI CCM..
Msikilize vizuri alicho kisema, kuwa yeye hapigii kampeni chama chochote bali kwa taaluma yake anatusaidia sisi wananchi kuona ukweli ili tufanye maamuzi sahihi sisi baada ya kuona na kutambua.
 
Ukweli heading imeharibu kila kitu, sijapata kusoma uliyoandika ndani, ila...

Mwaka 2015 tulivyomchagua Magufuli kwa imani kubwa akiwa hajawahi kuahidi, kutimiza lolote kwani hakuwahi kuwa rais ndivyo atakavyomchaguliwa Lissu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais.
 
Back
Top Bottom