Uchaguzi 2020 Kuona ni Kuamini: Je, Oktoba 28, utachagua nini kati ya unachoona kwa macho kitu cha ukweli kilichopo vs ahadi tupu? Msikilize Masanja Mkandamizaji...

Mayalla kwa usomi wako hautakiwi kuuliza swali la mwanafunzi wa shule ya msingi, mkoloni alikuwa hapa na alijenga reli, barabara na meli ziwa Victoria na Tanganyika, Nyerere wakati huo hakujenga hata kibanda cha kuishi yeye! Lakini Watanzania walimchagua.
JF of GT's has lost GT's.
 
Baadhi ya Watanzania wenye vijeelimu vya kuunga au karisha wamekuwa wajikomba komba ili kuendesha family zao sasa huyo masanja na wewe paskali ndiyo maisha yenu hayo hivi kweli kuifiki kwa wake zenu unajiita wavulana au wanaume?

Sijaandika tu ila nachukia sana matendo yenu na maneno yenu maana wanafiki wakubwa nyiye yani ningekuwa mchawi ningewachukuwa msukule.
 
Daaa
IMG_20201022_230227.jpeg
IMG_20201022_230224.jpeg
 
Tunachagua Lissu kwa taarifa yako.
Wanabodi,

Sisi wana tasnia ya habari, kwenye uchaguzi huu, zaidi ya kuwahimiza watu na kuwahamasisha, hiyo tarehe 28 October, wajitokeze kwa wingi, kwenda kupiga kura, na kuitumia haki yao ya kidemokrasia, kuwachagua viongozi wanao wataka, media pia tuna wajibu wa ziada wa kuwaelimisha Watanzania, to make an informed decisions, wachague viongozi bora, watakao waletea maendeleo, na kuchagua vyama vyenye uwezo wa kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

Sasa kwa vile uchaguzi wa mwaka huu una ushindani mkubwa kati ya kuna chama chenye uwezo, the ability, the capacity and the capability ya kuwaletea Watanzania, maendeleo ya kweli, ambacho kiliahidi, na kimetekeleza, halafu kuna msururu vya vyama vya ahadi tuu, ili Watanzania waweze kufanya an informed decisions, tuwasaidie kuona vitu visivyo onekanika, kuona ni kuamini, tuwasaidie Watanzania waone, kisha tuwape uhuru wa kuchagua, ama wachague kitu cha ukweli, kinachoonekanika, au wachague ahadi tupu kama tulivyo ahidiwa mbingu na peponi.

Last week, nimekutana mahali na Msaanii Masanja, Mkandamizaji, msikilize kwa makini, anasema nini na anawashauri nini Watanzania.

Kwa faida ya wale wenzangu na mimi, ambao bundles na ku play video clips ni issue, naomba kuwasaidia, kwa kifupi Masanja anasema, ukimsikia mgombea anasema ataleta maendeleo, usiishie kusikiliza tuu ahadi za kuleta maendeleo, pali mfanyie huyo mgombea the simple assessment test ya his/her ability, capacity and the capability ya kuwaletea maendeleo, kwa kuangalia personal development yake, amewahi kufanya nini, kujenga nini au kuleta maendeleo gani, ukiona ana kitu cha kuonyesha, then mchague, atawaletea maendeleo ya kweli kwa sababu ameonyesha uwezo. Lakini kama hana chochote cha kuonyesha, ambacho alikwisha fanya, then ujue mgombea huyo ana piga tuu blah blaha lakini hawezi kuleta maendeleo yoyote.
Hivyo kwanza ona,



Kisha Amini na tarehe 28 October, ufanye uamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi wa ukweli, wa kuleta maendeleo ya kweli, kutoka vyama vya ukweli vya maendeleo.

Paskali
 
Kwanza asante kuchania uzi wangu, nayaheshimu mawazo yako, ndio maana nimekupa like,
Mimi mwenzio, nikukutana na posts za ugoro, I end up there and then, sijisumbui hata kufungua, let alone kuchangia!.
Next time save your time and jf space, jipitie tuu!.
P
Naimani kubwa sana post zako zote skuizi sisi tunao abudu mabadiliko tunasoma headings tu coz tunajua tu humo ndani lazima unaunga juhudi ili angalau uonekane labda upate favour flani kutoka kwa kiongozj wa Malaika.

Hivyo basi post zako skuizi zasomwa na wana CCM tu wengi tunagonga heading tu tunakupa makavu yako haooo tunasepa.

Sasa kwa bahati mbaya kiongozi wa malaika kakalia kuti kavu katika dakika za mwisho kabisa baada ya PONDA kupindua meza na kubadilisha sura ya mchezo.

Kwanza tumewapoteza na Ponda then tukawavuruga na ugomvi feki wa Membe na Maalim sasa Jumapili ndio funga kazi Raisi wa chuma anamalizia kwa KO ya chembe msukuma tunamkalisha chini.

Hiyo lazima nchi nzima itasimama kwa sababu ni bonge itakua ni bonge moja surprise alooo!!! Hongera sana kwa timu ya kampeni this time mmejua kuwazunguuka katika dakika za mwisho BIG UP sana.

#NI YEYE 2020
#RAISI WA CHUMA
#IRON PRESIDENT
#THE BULLET PROOVE
 
Kuna Watanzania ambao wana chuki binafsi na JPM. Kwa mambo ambayo JPM amefanya ni ukweli usiopingika amefanya kazi kubwa ya kuwavusha Watanzania wale ambao walikuwa omba omba kwa mabeberu wakati wa JMK na sasa ni matajiri wanaotembea kifua mbele. Watanzania wengi watamkumbuka JPM mara tu pale atakapoondoka madarakani na kutambua walichopoteza. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Itakapofika 2030 Tanzania itakuwa imezitimulia vumbi nchi nyingi za Afrika na wengi watakuwa wanakuja kujifunza kwetu.
 
Nimesoma heading tu, nikaamua kukoment bila kusoma kontenti maana najua umeandika ugoro.

Kwani 2015 alipochaguliwa Magufuli, ahadi zake zilikiwa zimeshaanza kutimizwa?

Kama tulivyomchagua Magufuli huku akiwa hajawahi kuahidi na kutimiza hapo kabla(maana hakuwahi kuwa Rais kabla ya 2015), ndivyo nitakavyomchagua Lisu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais lakini ambaye naona hatakuwa na serikali iliyojaa USHAMBA NA ULIMBUKENI WA MADARAKA.
Asante mkuu maana umenisaidia nilichotaka kusema. Sijategemea kama Pascal Mayalla anaweza kufikia hatua ya kujitoa ufahamu wa kiwango hiki as if jiwe alishawahi kuwaga rais miaka ya nyuma zaidi ya kuchaguliwa baada ya kuahidi alihoahidi 2015.
Lissu nae ameahidi naye ana haki ya kuchaguliwa kama alivyochaguliwa kiongozi yeyote wa awamu zilizopita.
Najua ikatokea Lissu akashinda na kuapishwa amini nakwambia mkuu, wapo wanaccm wengi watahamia Chadema na hoja yao kubwa itakuwa "Tulikuwa tunaogopa kufisiliwa mali zetu"
Time will tell
 
Huu uzi hata mtoto wa la darasa la 5 mkuza primary akiona anajua tu umeandika pumba.
 
Nimesoma heading tu, nikaamua kukoment bila kusoma kontenti maana najua umeandika ugoro.

Kwani 2015 alipochaguliwa Magufuli, ahadi zake zilikiwa zimeshaanza kutimizwa?

Kama tulivyomchagua Magufuli huku akiwa hajawahi kuahidi na kutimiza hapo kabla(maana hakuwahi kuwa Rais kabla ya 2015), ndivyo nitakavyomchagua Lisu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais lakini ambaye naona hatakuwa na serikali iliyojaa USHAMBA NA ULIMBUKENI WA MADARAKA.
Nakubaliana na wewe kabisa Rais aliye madarakani nae alichaguliwa kwa ahadi tu ambazo miaka 5 madarakani hata Mradi mmoja mkubwa hajatekeleza mpaka anatuomba miaka mingine 5 aweze kukamilisha kazi aliyoanza kufanya. Wananchi hawataki kusikia bila kuona au kutumia kuwa unajengwa Mradi wa umeme mkubwa kuliko yote duniani kwa gharama ya Sh. Trilioni 7 umefikia asilimia 90% huku hata nguzo moja ya kupeleka umeme kwa wananchi haijasimikwa. Au wananchi hawataki kusikia inajengwa SGR ya kisasa ya umeme kwa Sh. trilioni 5 mpaka Morogoro ambapo ilikuwa ifike Novemba, 2019 lakini miaka 5 sasa imekamilika asilimia 75% tu na Walugulu bado wanatumia Abood Bus Service kwenda Dar.

Hata Wasukuma hawataki kusikia madege yamenunuliwa, manane yamekwisha wasili bado manne yatakuja baadaye na Chato International Airport kuleta watalii Mbuga ya Wanyama ya Burigi inajengwa kwa matrilioni ya shilingi ujenzi ukifikia asilimia 50% Wasukuma bado wakisafiri kwa Musukuma Bus Service bila watalii. Aliyopo madarakani hata apewe miaka 10 zaidi hatakamilisha Miradi hiyo aliyoanzisha miaka 5 iliyopita, wananchi wanataka kuona Rais wao mpendwa anafungua Mradi wa Umeme wa Stiegler's Gorge kwa kuwasha umeme au anasafiri kwa SGR kwenda Mwanza kufungua reli hiyo ikiwa imekamilika badala ya kuweka mawe ya msingi Mradi mmoja kule Mwanza, Isaka, Uvinza, Makutupora, Kilosa, Morogoro na Dar es Salaam.

Wananchi hawataki kusikia Awamu ya Tano itawatua wanawake ndoo za maji vichwani, wanataka kuona wake zao weupe na weusi wakijitwisha ndoo za maji safi na salama kutoka karibu kuwapa nafasi ya kushiriki shughuli za maendeleo. Wasaka uteuzi kama akina Pascal Mayalla (Njaa) wanajua wao ni homeboys na Awamu ya Tano ikiendelea kuwa madarakani hata kama inachofanya hakionekani, nafasi yao ya kuteuliwa inabaki palepale ndo maana wanataka sote tuendelee kuunga mkono juhudi ingawa yajayo yanafurahisha. New Broom sweeps cleaner!
 
With due respect, Mkuu Nguruvi3, Tanzania yenye umasikini, mwisho ni Tanzania ya Kikwete, hii Tanzania ya Magufuli, Tanzania sio masikini tena, sasa yuko nchi ya uchumi wa kati!, tumpe mitano tena ili huu utajiri u reflect mpaka kijijini Mashokolo kunangashee kwa mababu na mabibi zetu.

Masanja amesema jambo la maana sana, charity begins at home, uwezo wa kuleta maendeleo unaanzia kwako, kwenye chama chako na ndipo kwenye taifa kwa ujumla. Ukipigiwa hesabu ya baadhi ya vyama, vimepata ruzuku kiasi gani ndani ya hii miaka 28 ya vyama vingi, na viefanyia nini ruzuku hiyo, you will be surprised! halafu mtu kama huyo aje kukuambia nichague mimi nitakuletea maendeleo...utaliwa!
Mkuu Pasco, hoja yako ni kuwa mwenye kitu cha kuonyesha ndiye achaguliwe.

Mimi ninasema CCM ina kitu cha kuonyesha, UMASIKINI.
Kwamba kwa miaka 60 tumebaki kundi la nchi masikini sana Duniani.

Haijalishi nani alikuwa madarakani huo ni ukweli, na hawa wanaotuongoza walikuwepo humo.

Pili, nimekuuliza kuna tofauti gani ya jimbo la Zitto Esther Bulaya, Mbowe, Sugu , Bwege na majimbo ya mkoa mtiifu wa Morogoro au Tanga ambako CCM ina cha kuonyesha?

Tatu, hawa Wapinzani hawana cha kuonyesha ! kwa miaka 5 hawakupewa fursa hata ya mikutano.
Muda mwingi wametumia mahakamani , leo mnataka waonyeshe nini, karatasi za dhamana.

Lakini kama ni ruzuku, CCM imefanya nini zaidi ya kupora mali za umma kama viwanja na majengo?
Ruzuku ya CCM si ndio imetumika kununua madiwani na Wabunge! chama cha miaka 60 ya utawala.

Pole pole anasema imetumika kununua V8 na HardTop, huko Hedaru wanawake na wanaume wanalala mzungu wa nne katika wodi. Mwaka 2020! tunaongelea vitanda hospitali wenye nchi akina Bushiru na Pole pole wanatamba na V8

Hongo kwa kutumia mali za umma inatumika wazi wazi. Hivi Mwenyekiti wa CCM anapotoa milioni 100 wakati wa kampeni kupitia unawezaje kumlinganisha Mpinzani anayekimbizana na OCD !!

Kuonyesha Jengo haitoshi, wananchi wanataka kujua hivi kule Hedaru kwanini pesa zimetolewa ikiwa CCM wana cha kuonyesha! Miaka 60 hakukuwepo na Hospitali na hilo ni la kujivunia kweli!

Mwisho wa Yote haya ni CCM kushinda kwa kishindo. OCD kasema! NEC wanajua!

Kitu cha kufikiria kwa mwenye akili, pamoja na msaada wote, miaka 5 ya kampeni peke yao na kutumia rasilimali za umma n.k. Leo CCM wanasaga meno kama vile hawajawahi kutawala.

Hivi chama cha miaka CCM 60 kinatambia V8 ndicho cha kuonyesha hicho?
V8 na hardTop wakati watu wanalala mzungu wa nne hospitali! ndicho cha kuonyesha hicho

Angalia chuki ilivyojaa dhidi ya CCM pamoja na kuwa na vya kuonyesha. Wananchi wanaonyesha kuchoshwa na chuki nzito dhidi ya waendesha V8 na HardTop.
 
Kwani 2015 alipochaguliwa Magufuli, ahadi zake zilikiwa zimeshaanza kutimizwa?

Kama tulivyomchagua Magufuli huku akiwa hajawahi kuahidi na kutimiza hapo kabla(maana hakuwahi kuwa Rais kabla ya 2015), ndivyo nitakavyomchagua Lisu mwaka 2020 ambaye naye hajawahi kuwa Rais lakini ambaye naona hatakuwa na serikali iliyojaa USHAMBA NA ULIMBUKENI WA MADARAKA.
Huu uzi ! Yaani watu wamefikia mahali pa kuona Watanzania ni majuha sana

Nyerere alizaliwa na kitu? Mwinyi , Kikwete, Mkapa je, walitokea mbinguni.

Halafu wanasema wamefanya mengi wana chakuonyesha! Well, UMASIKINI wa nchi pia ni jitihada zao.

Kila siku ukiwasikiliza Watanzania utabaki unajiuliza. Soma huu uzi halafu urudi ule wa Pole pole na V8 na hard Top. I mean kuna tatizo gani ? Mbona watu wanaongea tu?
 
Sasa mtu hajajenga hata choo cha ofisi halafu anasema atafanya. Akajenge kwanza ofisi ya makao makuu chamani kwake ndio aje atujengee flyover
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip, kwa sasa be free kusema lolote, chochote, lakini baada ya October 28, tutaelewana tuu, Watanzania wanajua, wanataka nini, na wanajua watamchagua nani, wa chama gani, atakayewapatia wanachotaka, sasa hii ya mimi kuwa na credibility humu jf au Masanja ndio wale wale, hizi ninazoleta humu ni clips zimekwenda hewani, tuna deal na Watanzania wote na sio wana jf pakee, hivyo mimi kukosa credibility humu, doesnt matter much, kwa sababu wana jf ni wasemaji wazuri sana lakini sio wapiga kura!.
P
Inawezekana mkashinda lakini ushindi wenu tayari umeshakuwa haramu.
Najua utafurahia haramu kwasababu tu ya kuzoea kula haramu
Mungu atawahukumu kwa hili.
 
Back
Top Bottom