Kuombwa msaada mara kwa mara na hata na wasionifahamu

Tatigha

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
1,957
2,012
Wakuu habari za wakati huu hope mko poa.

Tokea niko secondary mpaka sasa chuo, marafiki zangu, ndugu zangu, na watu wa karibu wakiwa na shida mara nyingi hunifuata mimi ili kuweza kuwasaidia. Mtu wangu wa karibu akihitaji kukopa kiasi kadhaa lazima mtu wa kwanza niwe mimi kufuatwa.

Na kweli uwezo wa kuwasaidia huwa uko ndani ya uwezo wangu. Lakini cha ajabu mimi bado sijaanza kujitegemea bado niko kwa wazazi mpaka nitakapomaliza chuo,

Ila hilo swala la jamaa zangu kuomba msaada kwangu hilo halinishangazi sababu wanajua nina uwezo huo wa kuwasaidia sababu wananifahamu,

Kilichonifanya mpaka kuandika thread hii. Mara nyingi nikiwa natembea barabarani nimeongazana na watu kadhaa mbele yangu, hutokea mtu ambaye simfahamu wala yeye hanifahamu atawapita wale wengine woote ila atakapofika kwangu atanisalimia baadae ataanza kueleza shida zake.

Mara nyingi huwa ni suala la kukwama kwenye nauli na kweli huwa nawasaidia, wengine utakuta amekwama kwenye kupata msosi anahitaji buku mbili, huwa nawasaidia. Na sio mara moja hiyo huwa inanitokea mara kwa mara.

Na pia naweza kupata rafiki kwenye social network baada ya kuzoeana Bila kuonana, siku akikwama lazima anicheki ilihali hafahamu hali yangu ikoje! Sasa mimi najiuliza huwa wanajuaje kama watapata msaada kwangu? Hili limenitisha baada ya kusoma makala moja, inayosema "kwanini watu wengi hawaendelei" na moja ya sababu iliyotajwa ni kupenda kutoa toa msaada kwa watu.

Yaaani eti ukiona kila mtu wako wa karibu akipata tatizo la kifedha wa kwanza kukimbiliwa Kuwa wewe unapaswa ujitafakari. Daaa wakuu hiyo point ilinigusa sana.

Ningependa kuona shuhuda za Wana jf wenye kesi kama zangu wao maisha yao yakoje??
 
Wakuu heading nimekosea kidogo, ni wasio ni fahamu wala kuwafahamu mods rekebisheni
 
Tatigha mura,inaonekana una nyota ya kusaidia watu.Fanya hivyo kama inakuwa katika uwezo wako.UTABARIKIWA ZAIDI
Ni kweli mkuu huwa nikiwa na uwezo huo nafanyaga hivyo kwa kweli, ila Kuna wengine wapenda bata unakuta hana shida, hao huwa nawachomolea
 
mkuu mpk sasa kuna kadem kanasoma huko mwaswa kinanisumbua kweli, kina dai hakina nauli ya kuja kwao Dar mana kinasoma boarding, lkn navyo muona naona kama ni kitapeli,
Najiuliza nimtumiee?
 
mkuu mpk sasa kuna kadem kanasoma huko mwaswa kinanisumbua kweli, kina dai hakina nauli ya kuja kwao Dar mana kinasoma boarding, lkn navyo muona naona kama ni kitapeli,
Najiuliza nimtumiee?
Umakadharau sana mpaka "kukaita kademu".
Mpotezee
 
Hiyo ni karama yako uliyopewa na Mungu kuwasaidia wengine cha msingi kuwa makini kuwasaidia wale wenye shida kweli
Kutoa ni kuzuri mno wewe unawasaidia wengine hata kama hawatakusaidia pia ila Mungu atakupa msaada kwa namna ya tofauti usiache kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji endelea ila tu uwe na kiasi
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom