Kuombwa msaada mara kwa mara na hata na wasionifahamu

Aiseee upo km mimi ilinilijua mapema sana kuwa nimeridhishwa kuwasaidia watu ovyo na wazazi wangu bas nikajifunza kuwa selfish in hard way...saivi naweza hata kumuambia rafiki yangu sina wakati zamani nilikuwa siwezi kabisa kusema sina nikililiwa shida
umewezaje mkuu
 
Kila mtu anajinsi anavyoonekana.

Shukuru Mungu unaonekana ni mtu wa kuwasaidia wengine.
Cha msingi ujitawale na usiwe na huruma kupita kiasi kwani itakufanya usiendelee.

Kwa upande wangu sijui watu wananionaje kwani huniogopa na kutii mambo niyasemayo. Pia huamini kila nikisemacho hata kama hawanifahamu.

Jambo hili limenifanikisha kwenye mambo mengi ikiwemo uongozi, kupata temporary job n.k.
 
Kila mtu anajinsi anavyoonekana.

Shukuru Mungu unaonekana ni mtu wa kuwasaidia wengine.
Cha msingi ujitawale na usiwe na huruma kupita kiasi kwani itakufanya usiendelee.

Kwa upande wangu sijui watu wananionaje kwani huniogopa na kutii mambo niyasemayo. Pia huamini kila nikisemacho hata kama hawanifahamu.

Jambo hili limenifanikisha kwenye mambo mengi ikiwemo uongozi, kupata temporary job n.k.
Mimi siamini usemalo "shukuru Mungu".

Siamini Mungu yupo.

Labda kama umesema kifasihi tu.

Kwa hiyo kuna wengine hatukuamini.
 
mkuu hongera sana. mimi nilikuwa kama ww nilikua nasaidia sana marafiki kuna siku chuo nilifuria, atm ikawa haitoi pesa nikawa naomba 400 tu ya nauli nikatoe pesa mjini maajabu kila niliyemfata ananiambia sina hela nikaenda kwa jamaa ambaye nilimsaidia sana na nilimsamee pesa nyingi tu nikamwomba 400 akanijibu "nina pesa ya sadaka ya kesho jumapili". siku hiyo nilishinda njaa kwa kukosa 400 tu. ila nilijifunza, tokea siku hiyo hakuna rafiki niliyewahi kumkopa hata 100.
 
Mkuu wala usijali...Saidia kadri uwezavyo (ujaliwavyo) kama hauko vizuri kuwa muwazi tu..BARAKA ZITAKUJIA NYINGI TU
 
Wakuu habari za wakati huu hope mko poa.

Tokea niko secondary mpaka sasa chuo, marafiki zangu, ndugu zangu, na watu wa karibu wakiwa na shida mara nyingi hunifuata mimi ili kuweza kuwasaidia. Mtu wangu wa karibu akihitaji kukopa kiasi kadhaa lazima mtu wa kwanza niwe mimi kufuatwa.

Na kweli uwezo wa kuwasaidia huwa uko ndani ya uwezo wangu. Lakini cha ajabu mimi bado sijaanza kujitegemea bado niko kwa wazazi mpaka nitakapomaliza chuo,

Ila hilo swala la jamaa zangu kuomba msaada kwangu hilo halinishangazi sababu wanajua nina uwezo huo wa kuwasaidia sababu wananifahamu,

Kilichonifanya mpaka kuandika thread hii. Mara nyingi nikiwa natembea barabarani nimeongazana na watu kadhaa mbele yangu, hutokea mtu ambaye simfahamu wala yeye hanifahamu atawapita wale wengine woote ila atakapofika kwangu atanisalimia baadae ataanza kueleza shida zake.

Mara nyingi huwa ni suala la kukwama kwenye nauli na kweli huwa nawasaidia, wengine utakuta amekwama kwenye kupata msosi anahitaji buku mbili, huwa nawasaidia. Na sio mara moja hiyo huwa inanitokea mara kwa mara.

Na pia naweza kupata rafiki kwenye social network baada ya kuzoeana Bila kuonana, siku akikwama lazima anicheki ilihali hafahamu hali yangu ikoje! Sasa mimi najiuliza huwa wanajuaje kama watapata msaada kwangu? Hili limenitisha baada ya kusoma makala moja, inayosema "kwanini watu wengi hawaendelei" na moja ya sababu iliyotajwa ni kupenda kutoa toa msaada kwa watu.

Yaaani eti ukiona kila mtu wako wa karibu akipata tatizo la kifedha wa kwanza kukimbiliwa Kuwa wewe unapaswa ujitafakari. Daaa wakuu hiyo point ilinigusa sana.

Ningependa kuona shuhuda za Wana jf wenye kesi kama zangu wao maisha yao yakoje??
pole hauko peke yako,tuko pamoja.. nikitoa msaada lazima nitarudishiwa mara dufu ya nilichotoa ...ila sijawahi saidia mtu nisiyemjua
 
mkuu mpk sasa kuna kadem kanasoma huko mwaswa kinanisumbua kweli, kina dai hakina nauli ya kuja kwao Dar mana kinasoma boarding, lkn navyo muona naona kama ni kitapeli,
Najiuliza nimtumiee?
Kuna dada nlimtumia 25,000 aje hadi leo bdo ypo njiani anakuja nakushauri hela yko kale karanga yote!
 
b7b6eecf6fa53bbb3d1fb9fc4f94d29d.jpg
 
1. Namna unavyojiweka nadhifu inaweza kuwa ni moja ya ssbabu
2. Pengine una sura ya upole na utaratibu ambayo inafanya watu wawe na matumaini kuwa kwako anawezwa kusikilizwa shida yake pasipo kupewa majibu ya hovyo
........ila mwisho wa yote kama uwezo unaruhusu endelea kusaidia haina shida hasa kwa wale wenye shida za chakula na nauli na wawe wale ambao kwa kumuona unajua kabisa huyu kweli ana shida.
Angalizo:
Dunia ya sasa ni mbaya hivyo utoapo wengine hufanya kama chuma ulete hivyo kwa imani yako utoapo nuhia kwaneno la kuangamiza nia yoyote mbaya kama ni kusudio la unayemsaidia
 
Back
Top Bottom