Kuombwa damu kwa waathrika wa ukimwi - serikali inashindwa kuwalinda watu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuombwa damu kwa waathrika wa ukimwi - serikali inashindwa kuwalinda watu wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kakolo, Jul 12, 2011.

 1. k

  kakolo Senior Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Jumapili siku ya tarehe 10 mwezi huu kituo kimoja maarufu cha redio kilirusha kipindi kikimuhoji dada mmoja muathrika wa ukimwi aliyeombwa damu na mama mmoja ambaye anafahamiana nae. Lakini kwa kujua kuwa si sahihi yeye kutoa damu yake ikatumike kumuathri mtu mwingine alikataa na wakati huo tayari alikuwa ameshafikishwa hospitali fulani ya binafsi.

  Huyo mtu wa maabala alitumia muda mwingi kumbembeleza huyo dada akubali ili hali yule mama aliyempeleka pale akiwasiliana na watu wengine kwa simu akilalamika kwamba yule dada amekataa. Yule dada (muathrika) anaamini kuwa ule ni mtandao si kwamba yule mama alikuwa peke yake. Pia walikuwa wanajadili kumuongezea hela kama hiyo laki moja anaiona ndogo na wakamwahidi bado wataendelea kumpa deal kwani wanahitaji sana damu yake!

  Pia katika kipindi hicho kulikuwa na kijana mmoja ambaye yeye ni kibaka anayetumia hiyo damu kuchoma watu wanaokuwa wabishi kutoa walichonacho wakiingia katika mitego ya huyo kijana na wenzake.

  Je ni kweli serikali haiwezi kuwatafuta hao watu wakasaidia katika uchunguzi?
  Au ni wazo zuri - to do nothing?

  Source: J2 - Radio ya watu.
   
 2. dizbap

  dizbap Senior Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  INATISHA........! Watu kama hao wakikamtwa ni kupigwa RISASI tu. tuwe kama china sometimes ktk sheria, hao watu wa haki za binadamu tunawaweka kando kidogo.
   
 3. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ina maana walikuwa wanamuomba wakati wanajua ameathirika au hawakujua wakadhani anawanyima tu sababu ya mauchoyo yake?

  Kama walijua na wakamuomba hivyo hivyo lazima nikiri nimeshtuka mno na habari hii!
   
 4. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa nilivyoelewa walijua kuwa ana ngoma na ndo maana wakaimaind hiyo damu yake ikatumiwe na vibaka kudunga wabishi wa kutoa.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Huyo dada kwanini asiende kutoa taarifa kwenye vyombo husika?
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  hivi hii inaweza kuwa na ukweli? hiyo damu ya kutishia nayo watu wakati wa kuiba ni tabia ya machokoraa wa kenya,sijaisikia tz. lakini unapotishiwa na damu kwenye syringe,ambayo huwezi ku-prove kwa haraka kama ina virusi ama la,sidhani kama utawaza mara mbili! my take is,hata kama stori ni ya kweli,hao vibaka wenyewe wanajuana wenye ngoma ni wepi manake kuna drug addicts. ukanunue damu kwa laki moja afu ukawauzie kwenye vichupa? labda huyo mama alikuwa anataka akamdunge nyumba ndogo ya mumewe!ukizingatia complication za kuitunza hiyo damu isiharibike kabla ya kufanya uhaini uliokusudiwa,inahitaji well organised crime gang! nb: labda damu ni kwa ajili ya kutishia mafisadi warudishe hela zetu
   
 7. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndio hivo, wanajua kabisa amehathirika alafu wanamuomba ili waitumie kama silaha kunyanyasa raia. Tunakoenda sasa ni kubaya kuliko tunako toka...
   
 8. m

  mhondo JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wakimtishia kumchoma mtu aliye athirika tayari na anajifahamu hali inakuwaje?
   
 9. k

  kakolo Senior Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Sijui kama TZ ukienda polisi kufungua kesi kama unalipa hela ya kufungulia jalada, ila kwa maoni yangu ingawaje si mtaalamu wa sheria hao wahusika yaani waombaji wa damu wangeshitakiwa na jamhuri halafu huyo dada muombwaji akawa shahidi.

  Ana evidence maana anamjua yule mama aliyembeba kwenye gari, anaifahamu hiyo hospitali pia kuna evidence za simu kuwa-link hao waliokuwa wanataarifiwa kwamba amekataa (Naamini serikali ikitaka recorded messages toka kampuni za simu watapata).

  Hao watu walijua ni muathrika, na huo mchezo unafahamika na hiyo hospitali binafsi kama la basi mtu wa maabala anaujua huo mchezo.

  Tatizo la polisi wetu hawa-investigate hadi wapelekewe evidence kama wanavyoomba evidence ya ufisadi.
   
 10. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inatakiwa waathinirika wakiombwa damu waanze kwa kuwachoma hao wanaoomba kwanza
   
 11. k

  kakolo Senior Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Lengo lao kwa kweli siyo dogo hivyo maana Kama wakotayari kutoa laki plus ina maana wao wanapata zaidi ya hapo. Ila yule kibaka aliyekuwa amealikwa ktk hicho kipindi yeyeshughuli zake za uporaji anafanyia Temeke Mwembe Yanga.Ku-justify kama alishaitumia hiyo njia ya uporaji alisemaktk tukio moja walimchoma jamaa akazimia, na akasemaIkikutokea wewe toa haraka sana vitu ulivyonavyo maanahuwa hawatanii. Tahadhari.
   
 12. k

  kakolo Senior Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Shida siyo Ukimwi tu bali kuna hep C ambayo haina dawa ila ina kinga.
   
 13. k

  kakolo Senior Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kikwete ktk mahojiano yake na CNN kama sikosei alisema "TO BE BORN IN AFRICA IS A CHALLENGE" Therefore serikali hata kulinda raia wake walipa kodi ni vigumu.
   
Loading...