Kuombana sukari na chumvi ni kuendeleza umasikini?

Inawezezekana kabisa, Yaani wao wakifua mie wala sihangaiki kufua naacha ipite, lakini mie nikianza kufua lazima naye afue jamani! Mpaka nikamuuliza kwani ukiacha leo nifue mimi utapungukiwa na nini!,
Looh,
Alikuwa na lake jambo huyo si buree.. hahah
 
Yeye anaongoza kwa kutoa/kugawa anapoombwa.

Huwa namwambia sio kila kitu lazima atoe, watu washamjua kuwa huwa hanyimi, wataendelea kutumia huo udhaifu ili kuomba vitu hata vidogo
Duu mie nilikuwa mjinga kama hivyo, ila mie wananinyima siku moja nikanyimwa vibanio vya nguo vyaku vilipotea akawa wananinyima, siku nikaongea kwa sauti nambia marufuku kutoa kitu ndani.
 
Vifuniko vya asali vianike faragha bana, hata ukivianika public jitahidi visionekne.

Mke wangu anaanikaga ndani, nje hapana, hata majirani pia huwa hawaaniki nje na wakifanya hivyo lazima wavifiche.
Sasa hapo umefunika na kanga unabana na vibanio vinasogezwa, kuanikà ndani tutamalizwa na ma fungus jamani
 
Tanzania siyo Dar peke yake. Hapa nazungumzia maisha yetu vijijini kwetu.
Kama mie Kijijini kwetu tulikuwa hatukai kwa mbanano, labda siku hizi, ilikuwa kuazima vitu kidogo sana eti kisu mama anakwambia ukienda kuazima kisu mtu anajua Leo wanakula nyama au wanaenda kuchinja kuku sasa nikama kujitangaza
 
Ni kujiendekeza tuu wakati mwingine

Mama'ngu alinambia "mwanangu ukiona unaenda kuazima kwa jirani kitu mara ya kwanza, ya pili na ya tatu basi jua hicho kitu una umuhimu nacho, lazima ununue chako" haya maneno nayaishi na nitayaishi yameniepusha na kupishana na watu pale inapotokea nimeenda kuishi mbali na nyumbani.

Hata biblia inatuambia usiende kwa jirani yako sana asije akakuchoka, akakuchukia... Tuwe na kiasi.
Funzo! mimi kuna jamaa kila siku ana azima ungo wa kuchambulia mchele... uswahilini kuna shida
 
Huwa tunagombana nikimkataza akiwa anaazimisha/kutoa vitu ovyo ovyo, huwa ananitafsiri kama nina roho mbaya lakini sivyo, ila huwa namsihi sio kila kitu akiombwa lazima atoe. Watu wakigundua udhaifu wa kutonyima vitu watakuwa wanatumia udhaifu huo kufaidika nao.

Sasa nilipoona huu Uzi nikamuambia ona leo mnavyonangwa hapa, baada ya kuuona akaukimbia maana umemgusa sana
 
Yaan leo hii hii kuna dada mmoja(jirani) amekuja kuniomba kiberit ilikuwa imebaki njiti moja nikamwabia lakn akasema lete hvyo hvyo bila hata ya woga, dah nikaona hamna noma nimpatie tu.

Sasa hvi mda mchache kabla ya kuingia humu amekuja dada mwingine na jagi lake kuomba maji ya kunywa aaahhh yaan tabu tupu hapo cjaongelea Jana. Yaan dah uswahilini pagumu sana
Vingine vinawashwa tu vinahitaji kupigwa miti hiyo ya kuombaomba Ni gia tu ya kukuingia
 
wananiuzi wale majirani wadokozi. umeondoka umeacha maji yako kwenye jaba au vidumu mwenzio anakuja anachukua vidum kazaa anapotea navyo au anachota maji kwenye jaba anaacha kiduchu.
Usiweke nje. Utawatekea kila siku
 
Back
Top Bottom