Kuomba mvua ili ijaze mabwawa ya maji tupate umeme na kuokoa kilimo

Kwaio ndio tumefikia hapo wabongo, kusali na kuomba ili mvua ije ijaze mabwawa yetu.
Tuokoe kilimo na muhimu zaidi tupate umeme wa kueleweka.
Je wenzetu wa UK, Japan, USA na nchi zingine huwa wanafanya hivi?
Ina maana tatizo ni mwenyezi Mungu kutokuteletea mvua au ni ufisadi, wizi na rushwa iliokithiri ndio chanzo cha matatizo yote?
Wadau leteni mada.
It is the only alternative we are left with!
 
kwa kweli khali ni mbaya wanaaacha kuisisitiza serikali izalishe umeme kutokana na makaa ya mawe..................wanakwenda kusali aiseeeeeeeeeeeee,hali tete.............
 
Mungu hatengenezi mvua,bali binadamu ndio wanaotengeneza mvua. No evaporation....no rain,period.

Exactly, sasa tunaomba Mungu tu halafu tunaendelea kuharibu mazingira (kukata misitu ovyo, kulima mpaka kwenye vyanzo vya maji au kwenye maporomoko), huyo Mungu atatusaidia kweli? Hiyo mvua itapatikana wapi wakati sayansi ya mvua inaeleweka vizuri tu?

Hata huyo Mungu tunayemwamini alisema 'nisaidie nikusaidie' siyo ukae msikitini au kanisani hufanyi kitu unaomba Mungu tu.
 
Kweli jambo hilo la kwenda bwawani hakika ni aibu! Ni juzi tu Mzee wa upako alitamba sana kuwa mvua itajaza mabwawa. Haikuwa hivyo. Kwani mzaliwa wa Tz anashindwa kujua kuwa nchi yetu inaathirika kadri tunavyozidi kuomba/ sali! The only thing to do is to reduce the speed and times of prayers ili kuiokoa nchi yetu. Biblia hufika mahali ikasema NYAMAZENI... Huu ndio wakati mwenyewe.
 
Back
Top Bottom