Kuolea nyumbani kunadumisha ndoa

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Ndugu wana JF,

Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?
 
Ni sawa kabisa! Hata watoto kuwafundisha lugha mbili (ya mama na ya baba) ni shughuli; lakini kama lugha ni moja tu watoto wana-enjoy! (Ndi wa Mureba nshamba na mukazi wange wa Mureba nshamba)
 
Kama kawaida yako wiliyeye, hahahahahah! unanifurahisha sana huishi kutapatapa , sasa umekuja na kabila , haya tunasubiri kesho utakuja na nn.
Ingawa mm najua kabila, dini haiingiliani na mapenzi.
 
Kama kawaida yako wiliyeye, hahahahahah! unanifurahisha sana huishi kutapatapa , sasa umekuja na kabila , haya tunasubiri kesho utakuja na nn.
Ingawa mm najua kabila, dini haiingiliani na mapenzi.

Sio kwamba natapatapa, ila naona wenzangu wana furaha sana na ndoa zao. Nilipochunguza nikaona wengi wameoa kwao au mikoa ya jirani ambayo wanaelewana lugha.
 
Sio kweli....ndio nasema kwa msisitizo kuwa uyasemayo hayana ukweli wowote. Bora ungeishia hapo hapo.[QUOTE=Wiyelele;5149979]Ndugu wana JF,

Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?[/QUOTE]
 
Hizi mambo zinachananya kwa kweli.........
Ngoja niwaachie waliooa makabila yao, mie nimewowa Mgiriama
 
Sio kwamba natapatapa, ila naona wenzangu wana furaha sana na ndoa zao. Nilipochunguza nikaona wengi wameoa kwao au mikoa ya jirani ambayo wanaelewana lugha.
Hapana wiliyeye, usiingie kwenye ndoa na Mizani ya Adam, nina maana gani usiangalie ndoa ya mwenzio ukafananisha na ya kwako, au ya wazazi wako ukataka na wewe yako iwe hivyo la hasha kaka yangu, Ndoa ni kama nchi na wewe mume ndiye Rais( kichwa cha Nyumba) sasa unatakiwa kwanza uwe strong, pili uwe na maamuzi magumu na mepesi, Tatu penda familia yako no matter what happen inside of ure house.

sikatai sisi wanawake saa zingine tunamatatizo yetu, ila ukiona mkeo hakujali, hakupigii pasi, ukirudi home hakupokei, embu fanya wewe akirudi mkeo mpokee, mjali , nguo zako usikubali housegirl afue fua mwenyewe na piga pasi mwenyewe utaona mkeo atakavyoogopa , na amini Mungu kuanzia hapo atakuwa nafanya hayo majukumu yake.

Lakini kama yeye hafanyi wewe unamwachia Housegirl ndipo hapo unaanza kumtamani , kwa kuwa mnakuwa karibu, usikubali hayo mazingira Wilyeye.
 
Sio kwamba natapatapa, ila naona wenzangu wana furaha sana na ndoa zao. Nilipochunguza nikaona wengi wameoa kwao au mikoa ya jirani ambayo wanaelewana lugha.

Ngoja nikwambie Wiliyeye, wewe kuanzia leo hii ukirudi home kama unachuki na mkeo ziondoe , na pia mkiss mkeo kama mwanzo mlipokutana.
Pili penda kucheza na kuongea na wanao , wasaidie Homework zao, yaani wewe kuwa busy na watoto wako utaona na yeye anakuja na mtaongea vizuri bila kutegemea.

Sisi wamama tukiona mwanamme anapenda sana watoto tunafarijika , Automatically tunawapenda waume zetu.
lile penzi ulilokuwa hulipati, kwa muda utaanza kulipata, kama alikuwa hakushirikishi kwenye mambo yake ataanza kukushirikisha na NDOA yako itachipua upya kama mwanzo.

Fanya hayo, Ukiwa Juu na Mkeo Yuko Juu hakutakuwa na suluhu mmoja lazima ashuke ndipo mtaelewana.
 
..Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya...
Lugha si mtu anajifunza tu? Sifikirii kwamba kinacholeta raha ni lugha mnayozungumza. Mimi nafikiri kinacholeta raha zaidi ni kile mnachokizungumza! Kwani kuna raha yoyote kutukanana kwa 'kilugha'?
 
Kuna ka ukweli fulani hapa, ndio maana mimi natafuta mmasai humu ndani, sijabahatika tu kumpata. lol
 
Nakubaliana na wewe, japo sio kuhusu lugha. Manake kuna wasiojua mother tongue zao kwa kukulia mjini. Kwenye ndoa, tamaduni ni chanzo kikubwa cha migogoro. Kama walau mnaamini kwenye same stuff (najipatia picha nnavyochukia matambiko na babangu Mtambuzi anavyoyafyagilia)
 
Last edited by a moderator:
Lugha si mtu anajifunza tu? Sifikirii kwamba kinacholeta raha ni lugha mnayozungumza. Mimi nafiki cha kinacholeta zaidi ni kile mnachokizungumza! Kwani kuna raha yoyote kutukanana kwa 'kilugha'?

Ni kweli, kwa mwanamke muelewa anaweza kujifunza, lakini wengine haaa! Unatangaza vita na janjawid!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom