Kuokoa Theluji ya mlima Kilimanjaro, miti yote ya kigeni ikate, ya asili ioteshwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuokoa Theluji ya mlima Kilimanjaro, miti yote ya kigeni ikate, ya asili ioteshwe

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Nov 8, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mlima Kilimanjaro unaisha, theluji (snow)itayeyuka iishe katika kipindi kifupi kijacho.

  Sababu za mlima kuyeyuka.

  -i) Ongezeko la joto duniani (global warming).
  hii inatokana na uchafuzi wa hali ya hewa angani kwa sababu ya viwanda na magari

  -ii) kupungua kwa mawingu katika mlima kilimanjaro.
  Mawingu yamepungua kutokana na miti ya asili (indigenous)kukatwa na kupanda ya kigeni (exotic).

  miti ya asili ilikatwa na Wizara ikapanda ya kizungu kwa ajili ya biashara.

  Miti aina ya pines na cypres imepandwa kuzunguka mlima kilimanjaro, hasa rongai na west kilimanjaro.

  Pine ni miti inayotakiwa kupandwa kwenye udongo wa tindiga au marsh kama kule australia au norway. Kule udongo muda wote umejaa maji.

  Pale Sokoine University of Agriculture pana Kitivo cha Misitu, na wafanya kazi wengi wa Idara ya misitu wanatoka pale. SomebodyDR. Kilahama, Prof Madofe, Prof Temu wanajua haya mambo kuhusu hii misitu.

  Tumeona madhara, sasa tuchukue hatua. Misitu yote ya Kisasa ikatwe na misitu ya asili iachwe iote yenyewe. Upepo unapovuma kutoka sehemu moja hadi nyingine mbegu za miti asili itasambaa na itaota. Mpaka hii miti asili iote na hali kama zamani irudi itachukua kama miaka 5
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ni kweli,miti ya asili iliota sawa na mazingira husika ndio maana kukawa na uhusiano mzuri wa kimazingira, katika kazi ngumu ambazo Mtanzania wa sasa anapaswa kufanya ni kupanda miti ya asili sawa na mazingira husika.

  Mkuu hii miti ya kuletwa,madhara yake ni makubwa sana tunapoipanda bila mpango endelevu. Kama serikali ingekuwepo ingetenga maneo maalumu ya kupanda hii miti ya kuletwa.
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Miaka mitano tu? labda kama miti ya asili ni mitumbaku!
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mti wa kiasili mpaka uje ufikie kiwango cha kuonekana kama mti hesabu miaka 20. Inaweza kuwa typing error au ameteleza.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hiki kitu nimekifikiria siku nyingi sana kwa nini miti yetu ya asili inazidi kupotea tu tunazidizi kuishobokea miti ya kigeni, kuna ile wanaiita mijoholo sijui km sijakosea kwenye shule nyingi za msingi utakuta imepandwa, ile miti sehemu nyingi imelalamikiwa kuwa inakausha vyanzo vya maji hata ukiangalia sehemu nyingi ilikopandwa chini yake hata nyasi hakuna hazioti
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mtiki ni mti wa kigeni,lakini kwa bahati nzuri ni mti ambao unaweza kukua bila kuua mimea mingine around kama ulivyo mjoholo,mwarobaini,mlingoti,pines,cyprus etc.
   
 7. A

  AM_07 Member

  #7
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  lakini tatizo la mlima kilimanjaro its more Global, maana ukiangalia greenhouse gases zinazotolewa na african countries ni moja ya kumi ambazo inatolewa na developed countries and the trends is still increasing, am sorry kuwa hata tupande miti haitasaidia sana, na pia mazingiza ya mlima kilimanjarao hayajaharibiwa kwa trend ambayo mlima unavyopoteza theluji yake, tangu mwaka 2000 umepoteza theluji kwa asilimia 26 wakati mazingira yake hayajaharibiwa kiasi hicho, kwa hiyo suluhisho ni Global cut off of gree house gasses emmission ambalo ni ndoto maana ni kuwaambia wafunge viwanda vyao!!! think of all the summit and forums from kyoto protocols till now, it nevers help. we will ends up loosing,
   
Loading...