kuokoa maisha (25000) vs kuchunguza maiti(100000))

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
mwezi wa pili au wa tatu mwaka huu tulimsikia waziri mkuu ndugu Pinda akitangaza ongezeko la posho ya kuitwa kazini baada ya muda wa kazi (call allowance) kwa wahudumu wa afya.
Ni hivi majuzi tulisikia kutoka bungeni kupitia kwa waziri wa afya ndg mwinyi na pengine waziri mkuu ndg Pinda kuwa posho ya uchunguzi wa maiti(postmortem allowance) imeongezwa kutoka 10000 hadi 100000.ongezeko la postmortem allowance limewashangaza madaktari kwani kwa mujibu wa viongozi wao,hawakuwahi kuomba ongezeko la posho hiyo na pia hawakuwahi kulipwa posho ya mamna hiyo.

Kwa upande wangu nimeshtushwa na aliyeweka huu mpangilio wa hizi posho mbili alidhamiria nini haswa.

Yaani daktari akiitwa kufanya upasuaji wenye kuokoa maisha mfano(c-section) analipwa 25000.halafu daktari huyo huyo akiitwa kufanya upasuaji wa kuchunguza maiti anapewa 100000,hivi hapa unategemea madaktari watapendelea kuokoa maisha au kusubiri vifo vitokee wavichunguze?
Hawa watunga sera hufanya kazi zao gizani wakiwa wamelala au wamelewa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hilo nalo neno, Mi nimeshuhudia Madaktari wakichunguza maiti, kwa kweli ni wizi mtupu kama watalipwa hizo hela, maranyingi watu waliokufa kwa ajali ndo kundi kubwa la watu wanaochunguzwa na madaktari, wanachofanya nikuwauliza kama ni kweli mnaamini marehemu alikufa kwa ajali basi mkisema ni ajali basi ndo uchunguzi umekamilika na Dr hapo atavuta Laki yake, Na kwa Silka ya Watanzania wengi watauwawa ili wakapate hela yakuchunguza, coz ubinadamu miongoni mwa watanzania unatoweka kwa kasi ya ajabu kama ccm inavyopukutika
 
Jingalao sijapenda ulinganifu ulioutoa kwasababu:
1. Uchunguzi wa Maiti (postmortem) unawezesha kufanyika kwa ugunduzi wa chanzo na sababu ya kifo. Uchunguzi huu ni muhimu kuweza kugundua namna bora ya tiba na kuzuia vifo. Kwa maneno rahisi postmortem ni njia ya kuzuia vifo visitokee kwa kuboresha tiba ya walio hai.
2. Allowance mbalimbali anazopewa daktari ni sehemu tu ya malipo anayopewa daktari kama sehemu ya kazi.(routen payment).
Katakana na sababu nilizoonyesha bila kujali ni kiasi gani kinalipwa kwa routen activity na occasional activity si vyema kuziweka kazi hizi za tiba kwenye mizani moja. Kwa mtazamo wangu Mtoa mada anakua Kama vile analinganisha kilo moja ya pamba na kilo moja ya nyama.
 
kweli shuhuli ipo.. Utata mtupu.. Wamepanga gharama ya kuchunguza maiti iwe juu kwa vigezo gani? Na ya kufanya operation ya mtu mzima iwe chini kwa misingi ip?
 
Yaani daktari akiitwa kufanya upasuaji wenye kuokoa maisha mfano(c-section) analipwa 25000.halafu daktari huyo huyo akiitwa kufanya upasuaji wa kuchunguza maiti anapewa 100000,hivi hapa unategemea madaktari watapendelea kuokoa maisha au kusubiri vifo vitokee wavichunguze?
Hawa watunga sera hufanya kazi zao gizani wakiwa wamelala au wamelewa.
Unashanga nini na huu ndio udhaifu wa kufikiri alokuwa anauzungumzia Mnyika
 
Viongozi wa CCM ni wavivu wa kufikiri na ni dhaifu kama alivyosema mnyika.
mwezi wa pili au wa tatu mwaka huu tulimsikia waziri mkuu ndugu Pinda akitangaza ongezeko la posho ya kuitwa kazini baada ya muda wa kazi (call allowance) kwa wahudumu wa afya.
Ni hivi majuzi tulisikia kutoka bungeni kupitia kwa waziri wa afya ndg mwinyi na pengine waziri mkuu ndg Pinda kuwa posho ya uchunguzi wa maiti(postmortem allowance) imeongezwa kutoka 10000 hadi 100000.ongezeko la postmortem allowance limewashangaza madaktari kwani kwa mujibu wa viongozi wao,hawakuwahi kuomba ongezeko la posho hiyo na pia hawakuwahi kulipwa posho ya mamna hiyo.

Kwa upande wangu nimeshtushwa na aliyeweka huu mpangilio wa hizi posho mbili alidhamiria nini haswa.

Yaani daktari akiitwa kufanya upasuaji wenye kuokoa maisha mfano(c-section) analipwa 25000.halafu daktari huyo huyo akiitwa kufanya upasuaji wa kuchunguza maiti anapewa 100000,hivi hapa unategemea madaktari watapendelea kuokoa maisha au kusubiri vifo vitokee wavichunguze?
Hawa watunga sera hufanya kazi zao gizani wakiwa wamelala au wamelewa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hivi na wale watumishi wanaohudumia vyumba vya maiti wanakumbukwa kweli kwenye posho hizo? Watumishi wale naona wangepewa posho kubwa kwasababu kazi wanayoifanya na mazingira yake ni magumu mno kuzidi hao madokta na pia wasomi hawaombi hata kama kuna nafasi wazi!
 
hii serikali sijui inaongozwa na watu wa namna gani!Hivi ukiwauliza walitumia criteria gani kuamua call-allowance iwe elfu15-elfu25 na sio labda elfu5-elfu10 au elfu50-elfu80 wateweza kutoa majibu?na hicho kichekesho cha postmortem kutoka elfu 10 hadi laki moja walikitoa wapi?
kwa kweli kazi tunayo
 
Jingalao sijapenda ulinganifu ulioutoa kwasababu:
1. Uchunguzi wa Maiti (postmortem) unawezesha kufanyika kwa ugunduzi wa chanzo na sababu ya kifo. Uchunguzi huu ni muhimu kuweza kugundua namna bora ya tiba na kuzuia vifo. Kwa maneno rahisi postmortem ni njia ya kuzuia vifo visitokee kwa kuboresha tiba ya walio hai.
2. Allowance mbalimbali anazopewa daktari ni sehemu tu ya malipo anayopewa daktari kama sehemu ya kazi.(routen payment).
Katakana na sababu nilizoonyesha bila kujali ni kiasi gani kinalipwa kwa routen activity na occasional activity si vyema kuziweka kazi hizi za tiba kwenye mizani moja. Kwa mtazamo wangu Mtoa mada anakua Kama vile analinganisha kilo moja ya pamba na kilo moja ya nyama.
mimi naona ulinganifu ni sahihi.mtu anaitwa kuokoa maisha ni shilingi 25000 wakati anayeitwa kutambua kifo kimesababishwa na nini atapewa 100000.kwa nini tusiwekeze kwenye kuzuia vifo?
 
maiti iliyozikwa na kufukuliwa ni tabu kuichunguza kuliko exploratory laparatomy ya masaa nane.
 
Ilikuwa janja tu hiyo, imepachikwa makusudi

Kwanza postmortem zinafanyika chache sana

Ni sawa na kumpa mchuzi aliyeagiza nyama rosti
 
maiti iliyozikwa na kufukuliwa ni tabu kuichunguza kuliko exploratory laparatomy ya masaa nane.

Tabu ya kuchunguza maiti na tabu ya kuokoa maisha ipi ina tija?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
kweli shuhuli ipo.. Utata mtupu.. Wamepanga gharama ya kuchunguza maiti iwe juu kwa vigezo gani? Na ya kufanya operation ya mtu mzima iwe chini kwa misingi ip?

Wazee wa mipango hao!washachukua perdiem na kutokomea.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
mimi langu kwenye hili ni onyo tu kwa serikali..! kujifanya mjanja(msanii) kwenye mambo sensitive kama haya ni kama kulala kama popo na kujidanganya kua unamnyea mungu..! sasa wasipo rekebisha haya mambo na kuchunguzana wenyewe huko na kusimamia mambo ya msingi wakawa bado wanaleta stori za vyama hapo bungeni badala ya kusema matatizo ya watu...! iko siku hii amani nzuri tuliyo nayo itatoweka ghafla..!
 
Back
Top Bottom