Kuokoa Gharama na kuiongezea thamani siku ya uhuru: Tuwe na Baraza la Kumbukumbu ya Siku ya Uhuru badala ya Gwaride

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Japo huu utaratibu uko karibu dunia nzima,sidhani kama na sisi nchi masikini tunastahili kuiga kila kitu kinachofanywa na mataifa yaliyoendelea na yenye kujitosheleza kiuchumi.

Hivi kweli ni sahihi kila mwaka kutumia mabilioni kuanda gwaride la uhuru ili hali watoto wanakaa chini mashuleni, watu vijiini wana-share maji na mifugo,watu wanakufaa kwa kukosa madawa,huduma za afya,n.k?

Uhuru huu tunaouadhimisha kila mwaka una maana gani kama matatizo haya yameendelea kuwepo kwa muda wa zadi ya nusu karne sasa tangu tupate uhuru?

Je,moja ya malengo ya uhuru ilikuwa ni watu kukutana,kulipana posho na kuangalia wanajeshi wakivunja matofali kwa mikono huku maeneo mengine ya nchi huduma za maji safi na salama ikiwa ni ndoto kwao?Haya ndio yalikuwa malengo ya uhuru?Je,si kweli kuwa kimekosekana chombo cha kusimamia malengo na madhumumi ya sisi kudai uhuru?

Je,tungekuwa na chombo kama hiki cha kisheria na kikatiba tangu siku nyingi, leo hii tungekuwa na vyeo vya wakuu wa wilaya?Tungekuwa na baadhi ya sheria zinazofanna na zile za mkoloni na mambo mengine ya aina hiyo?

Mimi nafikiri wakati umefika tubadili utarabu na tuweke sheria badala ya sherehe hizi kufanyika kila mwaka, sheria itamke wazi kuwa sherehe hizi ziwe zinafanyika kitaifa mara moja kila baada ya miaka miwili au tatu na badala yake tuwe na Baraza la kumbukumbuku la siku ya uhuru kila ifikapo December 9 ya kila mwaka.

Hoja yangu hapa ni kuwa,Baraza hili liingizwe kwenye katiba na kisha litungiwe sheria na Bunge ili majukumu yake yatambulike kisheria na Kikatiba.

Mwenyekiti wa Baraza hili awe ni Raisi wa Jamuhuri ya Muungano na makamu wake awe ni Raisi wa Zanzibar japo kiuhalisia uhuru huu ni wa Tanzania Bara lengo likiwa ni kulinda na kuimarisha Muungano.

Wajumbe wengine wa Baraza hili wawe ni wale wale wanaoalikwa katika maadhimisho ya sherehe za uhuru kama vile viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini, wakulima, wafanyakazi na makundi mengine muhimu katika jamii kama vile wasomi,n.k ambapo kila kitu litwakilishwa na idadi maalumu ya wajumbe itakayokubalika kwa mujibu wa sheria itayounda baraza hili.

Majukumu ya baraza hili yawe ni kusimamia utekelezaji wa malengo ya uhuru,kuratibu na kuandaa maazimisho ya kitaifa kila baada ya miaka hiyo miwili au mitatu,kuwa kiungo katika ya Bunge na serikali katika kutimiza malengo ya uhuru, kushauri na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya maswala yote yanayohusu uhuru wa nchi, n.k

Hivyo,badala ya kuwa na gwaride la uhuru,baraza hili liwe linakutana kila tarehe 9 December chini ya mwenyekiti wake na kufanya tathimi ya maswala yote yanayohusu uhuru na kutoa taarifa kwa umma na hata kupokea na kuchambua maoni na mapendekezo ya wananchi kuhusu uhuru na siku ya uhuru.

Baraza hili liwe na Katibu Mtendaji ambae ataliongoza baraza hili na ambae atakuwa na wajibu wa kutoa taarifa ya kiutendaji kwa mwenyekiti wa baraza(Raisi) na pia kuandaa hotuba itakayotolewa na Raisi kwa Taifa kila tarehe 9 December kwa kushirikiana na ofisi ya Raisi.

Gwaride la uhuru licha ya kuwa na gharama kubwa,lakini halitoa fursa kwa Raisi kuhutubia siku hiyo,halitoa fursa kueleza ni kwanini tulidai uhuru,nini yalikuwa malengo ya uhuru, tumefanikiwa kwa kiasi gani kutimiza malengo na madhumuni ya kupigania uhuru, tunakosea wapi kuhusu malengo ya uhuru na wala haliandai vipeperushi au vitabu kueleza historia ya uhuru na mambo mengine mengi tu ambayo yanapaswa kufanyika siku hiyo ya uhuru.

Tukiwa na chombo hiki kilichoundwa na watu kutoka makundi mbalimbali ya jamii nahakika kitasaidia kwa mambo mengi ikiwemo kukumea vitendo vinavyoondoa dhana nzima ya sisi kudai uhuru kutoka kwa wakoloni.

Siamini uhuru wenye mambo mengi,malengo kadhaa, na historia ndefu inastahili kuazimishwa kwa tukio la siku moja kama vile birdhday na tukio likipita basi tunasubiri mwaka unaofuata.

Hili ni wazo ambalo wataalamu na wadau mbalimbali wanaweza kuliboresha.

Ifike wakati na wengine waige kutoka kwetu na si kusubiri kila kitu kianzie kwao na sisi tuwe watu wa kuiga tu.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,570
2,000
Asante kwa gazeti
Watoto wa siku hizi mna matatizo sana,siku ya uhuru sio ya mchezo mchezo
Uwepo wa jeshi ni kuonesha tuna uwezo wa kujitawala na kujilinda
Gwaride la kijeshi ni heshima kuu na utii kwa mamlaka
Jiongeze kidogo kwenye somo la civics
 

Google chrome

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,118
2,000
waanze kufuta mwenge wa uhuru kwanza ili kubana matumizi, mwenge unazungushwa nchi nzima kwa gharama kubwa ukifika wilayani wanazindua kisima cha maji cha mil 15 wakati umezungushwa nchi nzima kwa zaid ya bil 300. Wangeuweka makumbusho hizo gharama za kuuzungusha zingefanyia mambo mangapi?
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Asante kwa gazeti
Watoto wa siku hizi mna matatizo sana,siku ya uhuru sio ya mchezo mchezo
Uwepo wa jeshi ni kuonesha tuna uwezo wa kujitawala na kujilinda
Gwaride la kijeshi ni heshima kuu na utii kwa mamlaka
Jiongeze kidogo kwenye somo la civics
Ni gharama za bure tu wakati kila mwaka mambo ni yale yale tu.

Kwenye zana za kijeshi na sisi tupo?

Haya mambo tuwaachie Norh Korea,Marekani na mataifa mengineo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom