Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,927
- 22,075
Kuoga aoge Rostam, Mengi, halafu watakate waandishi!
Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi; Tarehe: 5th May 2009
http://habarileo.co.tz/michezo/?n=244
Hakuna ubishi kwamba hivi sasa nchini, habari zinazotamba katika vyombo vya habari ni zile zinazozungumzia suala la ufisadi nchini. Kutokana na ukweli huo, kwa miezi kadhaa sasa, vyombo vingi vya habari vimekuwa vikifuatilia habari hizo kwa karibu na kuzichapisha au kuzitangaza kwa lengo la kuongeza mauzo au kujipatia umaarufu kwa njia moja au nyingine. Pia kuisaidia jamii.
Lakini jambo baya zaidi ni kwamba sasa inaonekana wazi kuwa vyombo vingi vya habari vimeanza kupoteza mwelekeo, kwani katika siku za hivi karibuni, suala la maslahi ya taifa limewekwa pembeni hivyo kinachoangaliwa zaidi ni maslahi ya kibiashara tu. Kibaya zaidi ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vimejiingiza katika mijadala hiyo bila kujua kwamba ina athari gani kwa taifa letu.
Katika hoja yangu, napenda nizungumzie mvutano uliopo sasa kati ya wafanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz na Reginald Mengi ambao kwa sasa umeshika kasi kubwa kiasi kwamba kwa siku kadhaa kumekuwapo na majibizano kati yao kupitia vyombo vya habari. Ingawa Waingereza wanasema big names make news (majina makubwa hutengeneza habari), wakati umefika sasa kwa vyombo vya habari nchini kuwa makini katika ufuatiliaji na uchapishaji wa habari za watu hawa wenye majina makubwa.
Sitoi hoja hii kwa lengo la kutaka suala hilo lisijadiliwe, bali ninachotahadharisha ni kwamba kwa jinsi mjadala unavyokwenda umehama kutoka katika maslahi ya taifa, na sasa yameibuka malumbano ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na vyombo vya habari. Kuna faida gani kwa waandishi? Yanatusaidia kweli? Hebu tutazame jamani, tusije tukafananishwa na paka wa hoteli, ambao hukaa meza yenye chakula na kama mahali hakuna chakula hawakai. Ni ukweli usiopingika kwamba kila mfanyabiashara kati ya hawa wawili ana wafuasi wake na jinsi mjadala unavyozidi kupanuka, wafuasi wao wanazidi kuongezeka.
Hii inatokana na uhusiano ulipo kati ya mtu mmoja mmoja au kundi la watu na mfanyabiashara mmojawapo au jinsi mmoja kati yao anavyoweza kuchanga karata zake mbele ya vyombo vya habari hivyo kufanikiwa kuushawishi umma ili uamini maelezo yake dhidi ya mwingine. Hii ni hatari kubwa! Kinachojitokeza ni kwamba hivi sasa vyombo vyetu vya habari vimeacha kuibua mijadala ya masuala yanayohusu maslahi ya taifa kama vile hali ya uchumi wa taifa letu na jinsi ya kujikwamua katika uchumi wa dunia ulioporomoka, badala yake nguvu zote zimeelekezwa kwa watu hawa wawili.
Kila kukicha vyombo vya habari vinafuatilia nani atajibu nini juu ya tuhuma zinazomkabili. Vyombo vyetu vya habari vimegeuka waendesha mashitaka ambao huwauliza maswali wahutumiwa ili kujenga hoja mbele ya hakimu au jaji. Vyombo hivi vimesahau kabisa kwamba malumbano yanayoendelea sasa yanapaswa kusikilizwa mahakamani badala ya vyombo vya habari kuyatangaza hivyo kuongeza uchonganishi kati ya watu hawa wawili matajiri, kwa maisha ya Kitanzania.
Kama itakumbukwa kutokana na nguvu ya malumbano hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliulizwa bungeni kuhusu mwenendo wa mjadala huo, naye alisema ni wajibu wa aliyetuhumiwa kwenda mahakamani kulalamika na kuonya kwamba si vyema masuala yalioko mahakamani kuzungumzwa na mtu yeyote. Ingawa alijibu kwa ufupi, kauli yake ilikuwa na maana kubwa kwani hakuna atakayetupatia ufumbuzi zaidi ya mahakama. Kwa kuwa kila mtu anasema kwamba anao ushahidi dhidi ya matendo ya kifisadi ya mwenzake, aende akatoe taarifa kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake badala ya kuuondoa umma katika ajenda muhimu za kijamii na kujadili mambo yao ambayo yanahitaji ufumbuzi wa kisheria.
Hatuna haja ya kujadili tuhuma zinazomkabili mmoja kati ya hao, kwani wananchi ni wasikilizaji tu na hawana la kufanya juu ya tuhuma hizo. Tunahitaji tuhuma hizo zifikishwe mahakamani na ushahidi wa kutosha ili fisadi wa kweli atumikie adhabu kutokana na ukubwa wa makosa yake. Vyombo vya habari bado vina kazi kubwa ya kuibua changamoto zinazowakabili Watanzania badala ya kungangania mivutano hiyo ambayo mwisho wake haujulikani. Vyombo vya habari havina budi kubadilika, Tanzania si ya watu wawili tu walio katika neema, ina watu wengi masikini ambao sauti zao hazisikiki popote, ambao wanahitaji kusikika kupitia vyombo hivi.
Ni vyema sasa waandishi tukawa makini katika mjadala huu, kwangu mimi nasema Mengi na Rostam wameoga, sasa waandishi iweje tutakate sisi? Ikumbukwe kwamba mwisho wa siku tutageukana sisi kwa sisi, na jambo hilo limeshaanza kujitokeza kwani baadhi yetu wameshaanza kujibizana kwenye magazeti tena kwa kukashfiana. 'Any way', tumeyataka wenyewe! Tusipeleke dhahabu kwa mhunzi badala ya sonara, tutakuwa tunakosea. Mhunzi kazi yake ni kufua vyuma, jambo la msingi ni kuwaambia waungwana hawa wapeleke mambo yao mahakamani. Lakini jambo la msingi kwa Mengi na Rostam hakuna haja ya kulaani giza, bali wawashe mshumaa. Maana yangu ni kuwa kama nilivyoeleza wasitupiane maneno makali, waende mahakamani, kwisha. Naomba kutoa hoja, nikiamini msema yote husifiwa na wachache. Ukweli ndio huo!