candymarry
Member
- Aug 4, 2012
- 32
- 8
Habari wana MMU, leo nimekuja kwenu tena kuna jambo linanitatiza kidogo kwani nimejiuliza sana, mara nyingi katika jamii yetu tuliyolelewa tumekuwa tukiona kuwa watu wanapochumbiana na hatimae kuoana, mara nyingi mwanaume ndio anakuwa mkubwa na endapo itatokea mwanamke ni mkubwa basi kutakuwa na either pingamizi au changamoto kwa wazazi wa pande zote mbili pamoja na jamii kwa ujumla. Swali langu kwenu ni je jamii inachukuliaje swala la watu kuoana wakiwa na umri mmoja, na pia humo ndani wataishi kwa kuthaminiana, kuheshimiana na kuvumuliana kama vile ambavyo wangeishi ikiwa mwanaume ni mkubwa kwa mwanamke?