Kuoa ni kujilipua ujasiri unahitajika

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,641
75,656
Itamsaidia zaidi anayeogopa ogopa kuingia.

Mimi nimesoma na I na J darasa moja kabisa. Tukamaliza wote STD seven I akafeli sisi na J tukaendelea na masomo ngazi zingine.

I akapelekwa shule nyingine akafaulu. hatukuonana naye tena.

Siku ya kwanza kumwona I yupo na rafiki yake N. Rafiki yake I ni mzuri saana akanisalimu mambo shemeji! kumbe tayari ni shemeji kwa kaka yangu. I naye kumbe mpenzi wa rafiki wa kaka yangu.

Miezi mitatu kupita baadae I akapata mimba lakini kizungumkuti kikaja ni ya nani? rafiki wa kaka bado anasoma na familia zao ni marafiki hakuweza kumtaja, akamtaja jamaa mwingine.

Kufupisha stori.

I akajifungua mtoto anafanana na rafiki wa kaka yangu. Kikwazo hawawezi rudiana tena mapenzi yalishakufa.

Classmate wangu J akajilipua akatangaza ndoa kwa I...leo hii wanaishi wanalea watoto. Huyu jamaa ni jasiri saana. Licha ya kuijua historia ya I vizuri lakini akasema hapana liwalo na liwe.

Hivyo, kuna mida ya kujilipua unafumba macho...Asaalam.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom