Kuoa mwanamke anaefanya kazi kwenye massage parlour ni kijitakia matatizo.

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,641
6,267
Huyu jamaa huwa tunaenda kuchuliwa kila weekend siku za jumapili kwenye Barber shop flani hivi, kama mnvyojua ukishakua mteja unajichagulia na mtu spesho kukuhudumia sio kila siku unabonyezwa bonyezwa na kila mtu wengine wana mikono kama ya wanawake wa kikurya hivyo huwezi furahia shughli yenyewe.

Turudi kwenye sababu ya kuleta hili bandiko, kwenye hiyo palour kulikua na mrembo moja aliyekua anamuhudumia jamaa ndiye alikua mteja wake.

Siku moja nilishtuka jamaa anasema kuwa anataka kuoa huyo msichana, nilimkatalia na kumwambia kuwa huyo mwanamke hafai kuoa, na sababu sio kuwa hawezi kuishi na mwanamume bali mazingira anayofanyia kazi hayawezi mruhusu kuwa mke mwema.
Jamaa alikubali ushauri, kinyume chake kumbe jamaa alishaoza kwa mdada hadi kufikia hatua ya kubanjuana.

Sababu nilizompa ni kuwa huyo mdada ni mrembo sawa lakini kumbuka kazi anayofanya ni ya hatari kwa mahusiano kwa sababu mbili, moja huyo mdada anao Wateja wengi, pili wanaompa vichenchi baada ya huduma pia ni wengi.

Hivyo mwanamke aliyezoea kushika vifua vya wanaume wengi kwa siku hawezi tulia kwenye ndoa.
Mwisho wa siku jamaa alimuamisha toka massage parlour hadi parlour ya nyumbani, siku ya leo kapiga simu tukaongee na shemeji amemshindwa, mpaka hapa najiuliza nitaenda kuongea nini wakati toka mwanzo sikuwahi kumkubali? Natafuta maneno ambayo nikisema shemeji aodoke kabisa.
 
Mkuu kumbuka mke wake Dr. Slaa, josephine alikuwa anafanya kwenye massage.

Alichofanya Dr. Ni kumuondoa huko kwa sababu aliona huyo mwanamke ana maono makubwa zaidi na ana ndoto kubwa kuzidi massage.

Lakini tusiwacrush wadogo zetu, kuna wengine wanafanya kazi bila kuwa na magumashi. Tuheshimu mkate wao wa kila siku.
 
Nawewe unaweza mruhusu mkeo aendelee kufanya huko??
Majibu kwa niaba ya smart.

Inategemea na utashi wa mwanamke.

Kuna wanawake ambao wanafanya kazi baa kwa malengo. Ukimnunulia bia hataki. Anaweza akakuambia nina mtoto nyumbani, badala ya kunywa bia naomba unipe hela ili mwanangu ale.

Mwanamke kama huyu ana vision. Baada ya muda hutamwona tena kwenye bar akimpata mwanaume atakayeikubali ndoto yake na kuifanyia kazi.
 
Unajua nini mahondaw wangu... Wengine wanafanya kazi huko siyo kwa sababu ya kupenda... Wakipata channel zingine wanasogea na kutulia... Kama mwanamke anadhamira kweli na kapata mwanaume wa kumuoa regardless her job hatoweza fanya ujinga...
Majibu kwa niaba ya smart.

Inategemea na utashi wa mwanamke.

Kuna wanawake ambao wanafanya kazi baa kwa malengo. Ukimnunulia bia hataki. Anaweza akakuambia nina mtoto nyumbani, badala ya kunywa bia naomba unipe hela ili mwanangu ale.

Mwanamke kama huyu ana vision. Baada ya muda hutamwona tena kwenye bar akimpata mwanaume atakayeikubali ndoto yake na kuifanyia kazi.


Sawa nimewaelewa !
Thanks
 
hapana aisee mi sikubali...!!!!
tumblr_inline_o4ghx4Lz2r1t0ijhl_500.gif
 
Back
Top Bottom