Kuoa/kuolewa na mume/mke ambaye tayari ana mtoto moja na zaidi...

Msandawe Halisi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
647
350
Je ile dhana ya ukipenda boga penda na ua lake. Je mke/mume ataweza kuishi na mtoto wake nyumbani kwenu ili hali mzazi mweziye aliyezaa naye yupo hai.

Je kama anaamua kumuacha mtoto kwa mzazi mwenzake na nyinyi kuishi wawili kuanzisha familia yenu. Je pindi mtoto akiumwa, imani itakuepo kiasi gani pindi ukimrusu mke/ mume kwenda kumjulia hali mtoto wake.

Kifupi nina mpenzi wangu tayari nipo kwenye taratibu za kuoa, ana mtoto moja pia mzazi mwenzake yupo hai.

Naomba tupeane uzoefu kidogo wa hili jambo.
 
Hiyo habari imenikumbusha kitu. Kwani mimi pia nina mpenzi ana mtoto mmoja tena wa kike. Usikute tunashare mpenzi!!Ila mpenzi wangu ni kiwembe hasa, ana wapenzi kama 10 hivi! Na kila mmoja amemuuahidi kumuoa. Kazi kweli kweli!!
 
Mimi naona poa tu, miaka ya nyuma nilitafuta sana mtu wa dizaini hiyo ili tukianza maisha tusiwe na presha ya kutafuta mtoto.Halafu kwakuwa pia mzee wangu alimuoa bimkubwa wangu akiwa na watoto 3 tayari wakati yeye muzee alikuwa fresh from chuo na tumeishi na wale ndugu zetu vizuri kabisa hadi sasa wote wakubwa na familia zao.

Nilipenda sana kum copy mzee wangu na busara zake za kumchukua mwanamke mwenye watoto 3 akaamchukua na watoto wake wadogo kabisa na kuanza kuwalea yeye wakati baba yao yupo na yupo vizuri kiuchumi kuliko hata yeye ambaye alikuwa fresh from chuo anaanza maisha.
 
inategemea ustrong wako kwn ukilegeza mwanamke atakuypanda kichwani kila siku atataka kwenda kumuona mtoto kwan wenzetu hawa hujisahau kwamba walishaachwa au kuacha pale anapopata amani ndani ya roho yake ujisahau na kumrudia yule baba watoto wake alikadhalika na sie wakiumeni shida hua iyoiyo ni PM namaba yakop ya cm ntakupigia nikueleze zaidi
 
Wanaume waliokwisha kuzaa nje wengi wao uja kuwa wakorofi kwa baadaye ukilinganisha na wanawake katika ndoa zao...
 
Wanawake wapo wengi tu. Chukua kitu kipya achana na makapi hayo.
 
Mimi naona poa tu, miaka ya nyuma nilitafuta sana mtu wa dizaini hiyo ili tukianza maisha tusiwe na presha ya kutafuta mtoto.Halafu kwakuwa pia mzee wangu alimuoa bimkubwa wangu akiwa na watoto 3 tayari wakati yeye muzee alikuwa fresh from chuo na tumeishi na wale ndugu zetu vizuri kabisa hadi sasa wote wakubwa na familia zao.

Nilipenda sana kum copy mzee wangu na busara zake za kumchukua mwanamke mwenye watoto 3 akaamchukua na watoto wake wadogo kabisa na kuanza kuwalea yeye wakati baba yao yupo na yupo vizuri kiuchumi kuliko hata yeye ambaye alikuwa fresh from chuo anaanza maisha.

nimekupenda bure.......
 
Hakuna ujinga kama kuoa mwanamke mwenye mtoto ambaye baba yake yupo, au kuolewa na mwanaume mwenye mtoto ambaye mama yake yupo. Wakati genye zinawasumbua, hamtaona tatizo, hapo kila mtu chupi inamuwasha wala mambo mengine hamkumbuki.

Issue inaanza kuwa tata siku mtu anaenda kumuona mtoto kwa mzazi mwenziwe.
 
thred zingine zinaweza kuharibu mood za watu tu humu nakuambia.

ngoja sisi wenye watoto wa nje tuendele kuona upande mwingine wa shilingi.
 
Hiyo habari imenikumbusha kitu. Kwani mimi pia nina mpenzi ana mtoto mmoja tena wa kike. Usikute tunashare mpenzi!!Ila mpenzi wangu ni kiwembe hasa, ana wapenzi kama 10 hivi! Na kila mmoja amemuuahidi kumuoa. Kazi kweli kweli!!

kweli wewe mvumilivu.:clap2:
 
Je ile dhana ya ukipenda boga penda na ua lake. Je mke/mume ataweza kuishi na mtoto wake nyumbani kwenu ili hali mzazi mweziye aliyezaa naye yupo hai.

Je kama anaamua kumuacha mtoto kwa mzazi mwenzake na nyinyi kuishi wawili kuanzisha familia yenu. Je pindi mtoto akiumwa, imani itakuepo kiasi gani pindi ukimrusu mke/ mume kwenda kumjulia hali mtoto wake.

Kifupi nina mpenzi wangu tayari nipo kwenye taratibu za kuoa, ana mtoto moja pia mzazi mwenzake yupo hai.
Naomba tupeane uzoefu kidogo wa hili jambo.
Hakuna tatizo lolote mkuu, nakutakia kheri katika ndoa yenu. Kuhusu suala la kuaminiana hilo linategemea mapenzi yenu mumeyaanda vipi, lakini kwamba kwenda kwa mkuu mwenzie anaweza kukusaliti hilo halina mashiko. Mtangulizeni Mungu kwa maisha yenu, vitu kama hivyo havita sumbua kabisa...
 
Back
Top Bottom