Kuoa/kuolewa na mtu wa imani tofauti na yako kunavyoweza kuharibu uhusiano wako na Mungu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
404
650
Hili sio jambo geni kwa wengi wetu, tunaweza kuwa tumeshuhudia au tumesikia, na wachache tunaweza kuwa hatujakutana na changamoto hii au hawajaona kabisa.

Kijana ambaye hajaoa/hajaolewa anaweza asijue shida atakayokutana nayo baada ya kuoa/kuolewa na mtu wa Imani tofauti na yake.

Imani ni jambo la muhimu sana na nyeti, ikiwa mtu atapuuza hili, akafanya maamuzi ya kuingia kwenye mahusiano ya ndoa na mtu asiye wa Imani yake, awe tayari kumfuata mwenzake kwenye dini yake. Kama hatakuwa tayari ajiandae kwa matukio magumu kwenye ndoa yake.

Vijana mara nyingi huona wanabaniwa au wanazuiliwa watu waliowapenda wao, wanaamua kujiingiza kwenye mahusiano na watu ambao baadaye wanageuka kuwa mwiba kwenye maisha yao ya wokovu.

Shida ya mtu ambaye hajamjua Yesu au ambaye hajaokoka, alafu wewe ukawa umeokoka, hupaswi kujiingiza kichwa kichwa kwa kigezo kuwa mnapendana sana, unapaswa kuelewa kuwa mkuu wa upendo wa kweli ni Mungu.

Imani zenu zikitofautiana na mwenzeko uwe na uhakika kuwa upendo wenu utaharibiwa na mivutano yenu, unaweza usilione hili mapema ila mkianza kuishi utaona shida ya kuishi na mtu wa Imani tofauti ilivyo mbaya.

Inawezakana mwenzako ni mkristo ila kwenye ukristo kuna madhehebu wana misingi tofauti kabisa unaweza kushangaa wanayoyafanya ni tofauti kabisa na neno la Mungu linavyoelekeza, ikiwa misingi ya Imani yako ni tofauti na misingi ya mwenzako, ujiandae vizuri, unaweza ukaasi Imani yako au ukaleta mgogoro kwenye ndoa yako.

Unaweza kutumia njia nyingine kufunga ndoa yako au usifunge ndoa ila mkawa mnaishi pamoja na mwenzako, ila ujue hamtakuwa na utulivu kutokana na kutofautiana kuamini kwenu. Mnaweza kushauriana vibaya ukabaki kuwa mtu alioacha Imani ya kweli.

Mwanzo unaweza usione hili kama lina shida kwako ila ukishaingia ndio utajua kuna shida, hasa kwa mabinti akiwa yeye alikuwa mkristo alafu akakubali kuolewa na Muislamu. Watafika mahali mwanaume hatakubali aendelee na Imani yake kikristo.

Wanaweza kuwa waliamua kupita njia zingine kufunga ndoa yao kwa kukubaliana kuwa kila mmoja atakuwa anasali dini yake, watakapokuwa mke na mume au watapokuwa na watoto, mwanaume hatakubali mke wake awe anaenda kanisani.

Ipo migogoro itaibuka, hasa pale mmoja atakapokataa kufuata makubaliano yao, wengine hufika hatua wakaona kuliko kuendelea kusumbuana bora kuachana, na wengine huona ya nini kusumbuana bora kumwacha Yesu na kufuata Imani ya mume wake.

Kumwacha Yesu kulinda mahusiano yako ya ndoa yasivunjike maana yake umekataa uzima wa milele mapema kabisa, na wengi huwa wanakosa ile Amani ya Kristo iliyokuwepo ndani yao kabla ya kufanya maamuzi ya kubadili dini.

Muhimu sana kuwa mwangalifu unapofanya maamuzi ya kuoa/kuolewa, hasa unapaswa kuwa mwangalifu kwenye eneo la Imani, hili usipuuze kama unataka kutimiza kusudi la Mungu ukiwa hapa duniani.

Ikiwa unampenda Yesu angalia mtu unayeenda kuishi naye, kumbuka bado tuna safari ya kwenda mbinguni, ikiwa utaharibiwa safari yako itakuwa ni hasara kubwa sana kwako. Ikiwa ni hivyo nakusihi sana usipuuze hili.

Mungu akubariki sana.
Samson Ernest
+255759808081
 
Sometimes dini zinatufanya tunabaguana,na kubaguana si lengo la Mungu bali sisi sote ni zao la upendo. Ndugu yangu upendo ndio kila kitu kwani asili ya dunia na vitu vyote vilivyomo ni UPENDO.
Sio kila unayempenda anafaa kuwa mwenzi wako wa maisha. Suala la imani ni muhimu sana, usilipuuze.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom