Kuoa/kuolewa na msomi ni chanzo cha mafanikio ya maisha?

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289

Mara nyingi binadamu tumekuwa tukikumbana na vikwazo vingi wakati wa kuoa kutoka kwa familia, ndugu, jamaa,marafiki n.k. juu ya mwanamke gani wa kuoa au mwanaume gani mwanamke anapaswa kuolewa kwa kutazama kigezo cha elimu.


Katika dunia ya leo baadhi ya wanaume hupendelea kuoa mwanamke msomi (angalau kwa elimu ya kidato cha nne kuendelea) tena mwenye kazi rasmi and viceversa. Vilevile misukumo toka katika familia juu ya mwanamke gani wa kuoa kwa kufuata kigezo cha elimu husababisha migogoro au kuvunjika kwa mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume.

Ni ukweli usiopingika (undeniable truth) kwa kijana msomi kwa ngazi ya chuo kikuu hukumbana na kikwazo hasa anapoingia kwenye mahusiano na mwanamke au mwanaume wasioendana kielimu kujikuta akiingia kwenye mahusiano ambayo yeye binafsi hakuridhika nayo kutokana na misukumo ya nje (external influence).

Kuna wakati unakuta mwanaume tayari amezaa na mwanamke aliyekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu, tena unakuta mwanaume/mwanamke huyu wanatofautiana sana kielimu kutokana na circumstances from either side lakini wanapendana kwa dhati na maelewano ya hali ya juu. Na zaidi mwanaume/mwanamke huyu unakuwa na guilty conscience kuachana na mwanamke/mwanaume.

Kwa bahati mbaya uhusiano wao huu unaingiliwa na wazazi wa upande mmoja na kupinga kijana wao asioe/asiolewe kwa kisingizio cha utofauti wa elimu.


Kwa kutumia kigezo cha elimu: Kuoa/kuolewa na msomi ni chanzo cha mafanikio ya maisha?

Nawakilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom