Kuoa au kuolewa

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
11,647
Points
1,250

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
11,647 1,250
"Kuoa na kuolewa" maana yake ni nini?
Maana yake ni ndoa...!

Ndoa ni nini:
Ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Yakiwemo kuwa na hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria...

Ndoa kwa mtazamo wa Uislamu inatarajiwa:

i) Kuihifadhi jamii na zinaa

ii) Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri

iii) Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia

iv) Kukuza uhusiano na udugu katika jamii

v) Kukilea kizazi katika maadili

vi) Kumuendeleza mwanaadamu kiuchumi.

(i) Kuhifadhi jamii na Zinaa

Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki.Wanyama pia wameumbwa na matamanio haya lakini yanatofautiana sana na yale yaliyopandikizwa kwa mwanaadamu. Matamanio ya jimai kwa wanyama yanakuja juu wakati maalum, wakati ule tu wanapokuwa tayari kupandikiza mbegu ya uzazi. Matamanio ya jimai kwa wanaadamu wa kawaida yako pale siku zote, mradi tu vipatikane vishawishi. Kwa hali hii, endapo mwanaadamu ataachiwa huru atosheleze matamanio yake ya jimai apendavyo pasina kuwekewa mipaka, kwa vyovyote patatokea madhara makubwa kwake binafsi na kwa jamii nzima. Hivyo, Mwenyezi Mungu (s.w.) aliyemuumba mwanaadamu kwa lengo na anayelifahamu vyema umbile la mwanaadamu na matashi yake kuliko yoyote yule, amemuwekea utaratibu madhubuti wa kukidhi haja zake za kimaumbile pasina kuleta kero kwa yeyote katika jamii. Mwenyezi Mungu (s.w.) ameharamisha jimai nje ya ndoa ili kuikinga jamii ya mwanaadamu na madhara makubwa ya zinaa ambayo huidunisha na kuivuruga kiasi kikubwa.
 

Forum statistics

Threads 1,392,139
Members 528,544
Posts 34,099,721
Top