Kunywa pombe watoto wakitembea uchi atajua mama yao!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Juzi siku ya Ijumaa ya tarehe 23/9/2011 usiku katika kipindi cha Kipima Joto cha ITV kilichokuwa kikiongozwa na Reinfred Masako, mmoja wa wachangiaji katika mjadala huo mama Rehema Mwateba kutoka mtandao wa kijinsia wa TGNP alizungumzia jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wanawake kila uchao.

Mfumo Dume, ndio kilio kikubwa cha mama huyo, kilichonisisimua ni pale alipotoa mfano wa jinsi mwanamke anavyobebeshwa majukumu ya kutunza familia kule Rungwe huku kina baba wakifuja fedha kwa ulevi.

Akiongea kwa uchungu mama huyo alidai kuwa kuna hata msemo unatumiwa na akina baba kule Rungwe wakiwa kwenye vilabu vya pombe, hujisifu kwa kusema, "Kunywa pombe, watoto wakitembea uchi atajua mama yao" (Neno hili alilitamka kwa lugha inayotumiwa na wakazi wa hapo Rungwe na alilitolea tafsiri)

Hii inadhihirisha ni kiasi gani mwanamke anabebeshwa majukumu kiuonevu, huku wanaume wakitanua na ulevi na pengine nyumba ndogo.
 
Kuna tofauti ya mume, mwanaume na mtoto wa kiume...... Kinachonisikitisha maisha ya leo bado kuna watu wanafanya hayo.... Itakua ni tatizo na jamii husika na mfumo mzima wa nchi km nchi. Hainingii akilini, mtu mzima, uamue kuoa na kufanya hayo mambo..... Bado tuna safari ndefu sana!
 
Huu mfumo dume sijui utaisha lini jamani,utakuta mtoto alieharibikiwa either kapata mimba za utoton,kakataa shule, kawa teja lawama zote anabebeshwa mama, jamani wababa badikikeni majukumu ya kulea ni wote.
 
Back
Top Bottom