KUNYWA MAJI ZAIDI KWA AFYA NA UZURI WA NGOZI YAKO

ELAFU

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
410
150
Miongoni mwa changamoto kubwa kwa watu wanaoshinda mbali na nyumbani ni kunywa maji ya kutosha. Hii hutokana na kulazimika kuyanunua kwa bei kuanzia sh 500/= hadi 1,500/= kwa chupa moja; akinywa chupa 1-3 kwa siku inakuwa ni pesa nyingi zaidi.
Leo nashauri watu kunywa maji zaidi kwa sababu kuu mbili :
1. Maji husaidia afya nzuri ya seli za ngozi na mwili kwa ujumla.
Kama unahangaika na vipodozi ili uwe na ngozi nzuri basi maji pia ni sehemu ya uzuri wako. Maji husaidia ngozi kuwa laini na kuzuia ngozi kuzeeka haraka, kukauka, makunyanzi nk
2. Maji ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani ya mwili wako (body reactions).
Kuwa na maji ya kutosha kutasaidia kupoza mwili wako na hizo shughuli zinazofanyika ndani ya mwili.

Maji zaidi. Afya zaidi.
 
Back
Top Bottom