Kunywa maji mengi

GlorytoGod

Senior Member
Sep 8, 2012
158
50
Heshima kwenu wana JF,

Mimi ninashida moja ya kuwa nikinywa maji mengi sana maana inaweza kufika saa 4asubuhi nimeshakunywa kama maji lta 4.

Ila nikikaa baada ya muda kichwa kinaanza kuniuma sana nasikia kizunguzungu mpaka nikae baada ya muda kama masaa 3 ndo napata nafuu.

Wandugu nisaidieni tatizo ni nini?
 
Umeanza lini kunywa maji mengi?

Kwa muda wa masaa 24 hutakiwi kuzidisha kunywa maji zaidi ya lita 3 na nusu, ajabu we mpaka saa nne asubuhi umeshamaliza lita nne ! bilashaka mpaka kufika saa mbili usiku utakuwa umemaliza lita 20.

Nani alikufundisha kunywa maji kwa staili hiyo unayotumia?
 
Kunywa maji zaidi ya lita tatu ni hatari sana kwa afya yako(you sweep out some nutrients from the body).kunywa maji kidogo kidogo,usinywe lita nzima kwa mara moja,zingatia kunywa saa moja kabla na baada ya kula.
 
heshima kwenu wana jf,

mimi ninashida moja ya kuwa nikinywa maji mengi sana maana inaweza kufika saa 4asubuhi nimeshakunywa kama maji lta 4, ila nikikaa baada ya muda kichwa kinaanza kuniuma sana nasikia kizunguzungu mpaka nikae baada ya muda kama masaa 3 ndo napata nafuu wandugu nisaidieni tatizo ni nini?

Kacheki kisukari faster
 
Kunywa maji zaidi ya lita tatu ni hatari sana kwa afya yako(you sweep out some nutrients from the body).kunywa maji kidogo kidogo,usinywe lita nzima kwa mara moja,zingatia kunywa saa moja kabla na baada ya kula.

Nusu saa kabla ya kula na unahesabu masaa 2 au 2.5 ndipo unywe tena maji kwa kiwango kile kile kwa mjibu wa uzito wako.
 
Ukila chakula kingi kupita kiasi unavimbiwa

Ukinywa maji mengi kupita kiasi yanasafisha tumbo linabaki wazi

Ukinywa kilevi kingi unakosa nguvu

Ukivuta bangi kwa wingi zinaondoa ufahamu wako
 
Kucheki sukari na pressure ni muhimu pia Fadhili Paulo. Asingojee kuumwa hata kama huamini kuwa anaweza kuwa ana tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Kucheki sukari na pressure ni muhimu pia Fadhili Paulo. Asingojee kuumwa hata kama huamini kuwa anaweza kuwa ana tatizo.

Mkuu, kilichotokea hapa ni kuwa yeye hakuwa na mazoea ya kunywa maji mengi siku za nyuma, ni juzi tu hapo alikuja na thread ya ugonjwa mwingine na nikamshauri anywe maji mengi na nikampa na link. Amini usiamini watu wengi ukiwauliza internet ni nini watakujibu ni facebook na yahoo, wengine waliozoea jf basi wataongeza na jf. Wapo internet kwao ni jf tu we unaona watu wanauliza vitu ambazo wange-google kwa dakika 1 wangekuwa wamepata majibu lakini hawawezi mpaka waje hapa waulize kwa kiswahili. Wengine hawataki kusoma, kwao mistari miwili ya habari inawatosha hawataki kuumiza kichwa. Wengine hata kubonyeza hizo link hawajuwi!, tutafika tu lakini.

Hata akipima kisukari haitasaidia kitu, juzi kuna mtu kaja hapa anasema baba yake anaumwa kisukari huu mwaka wa 12, nijuavyo mimi, kisukari, pressure, aleji, na hata pumu ni magonjwa yasiyotibika mahospitalini.

Kama wewe hujawahi kutumia maji mengi au kutumia maji kama tiba, basi usiamke tu na kuanza kunywa lita nne, anza na glasi moja na uongeze moja moja kila siku mpaka utakapofikia kiasi chako unachopaswa kunywa kwa mjibu wa uzito wako. Tembelea hiyo link niliyotoa hapo juu ina kila kitu kuhusu tiba kwa kutumia maji.
 
Fadhili Paulo, nakubaliana na wewe kaka. Binafsi nafanya medical checkup kila mwaka, lakini kila nikijisikia ovyo lazma nicheki sukari na pressure kama preucation kwa sababu nina risk factor (genetical history).

Nijuavyo kama umekunywa maji mengi sana kinachotokea sio kizunguzungu bali ni kupata haja ndogo kila mara. Ndo maana nasema pamoja na mengineyo, kupima kisukari na pressure ni jambo muhimu, kila mara na kwa watu wote.
 
Mkuu, ni vema akapime.
Kizunguzungu au kutokujisikia vizuri au kuuma kichwa lazima vikutokee kama kunywa maji haikuwa ni tabia yao kabla kwa sababu sumu nyingi zinatoka kwa wakati mmoja na unakuwa umeushtua mfumo mzima wa mwili, ndiyo sababu inahimizwa mtu aanze taratibu sana, huwezi kuurudishia mwili maji ambayo uliyakosa kwa miaka mingi kwa siku au wiki moja, na usipofuata kanuni hii unaweza kufa kweli. Bali hili lisikutishe unapaswa tu upunguze kiasi cha maji na ni wakati sasa yeye ajifunze vya kutosha kuhusu tiba hii kwa kutumia maji. Mi huu ni mwaka wa sita najifunza na kuitenda na sina shaka nayo.
 
heshima kwenu wana jf,

mimi ninashida moja ya kuwa nikinywa maji mengi sana maana inaweza kufika saa 4asubuhi nimeshakunywa kama maji lta 4, ila nikikaa baada ya muda kichwa kinaanza kuniuma sana nasikia kizunguzungu mpaka nikae baada ya muda kama masaa 3 ndo napata nafuu wandugu nisaidieni tatizo ni nini?

1.Wewe ni wa jinsia gani?

2.Je unanyonyesha?

3.Ulikua na matatizo ya kichwa kuuma sana kabla?

4. Unakunywa maji ya dukani au ya kuchemsha nyumbani ni maji salama au la?

5.Huwa unakawaida ya kunywa lita ngapi za maji kwa siku?

6. Je umesha jaribu kuacha hiyo dozi yako ya maji na kukaa kwa siku nzima moja au mbili na kuona kama kichwa kinaendela kuuma na kizunguzungu bado kipo au la?

7.Je katika familia ya baba na mama yako kuna mtu yoyote ana tatizo kama lako kama ndiyo kwa muda gani amekua nalo?

8.Je umeshawahi kuwa na miwani ya macho uliyopewa hospitali na si ile ya mitaani?

9.Je unafanya kazi katika mazingira gani na kwa kipindi gani?

Vitu ni vingi ila kwa sasa naomba nisaidie haya kwanza ili niwezi kutoa maoni
 
pole kuna shida nyingi, ila sijui tiba lakufanya kama upo MOSHI au ARUSHA naweza kukuelekeza kwa dokta mmoja anakifaa naamini ataweza kukusaidia. jaribu ushauri uliopewa ukishindwa nitumie ujumbe nitakuunganisha nae.
 
pole kuna shida nyingi, ila sijui tiba lakufanya kama upo moshi au arusha naweza kukuelekeza kwa dokta mmoja anakifaa naamini ataweza kukusaidia. Jaribu ushauri uliopewa ukishindwa nitumie ujumbe nitakuunganisha nae.

nashukuru sana mkuu mimi nipo arusha, ila tatizo langu bado halijaisha japokuwa unywaji wa maji nimepunguza, cyo kama nilivyokuwa nakunywa mwanzo, ungeniagizia kwa huyo doctor ningeshukuru sana mkuu
 
heshima kwenu wana jf,

mimi ninashida moja ya kuwa nikinywa maji mengi sana maana inaweza kufika saa 4asubuhi nimeshakunywa kama maji lta 4, ila nikikaa baada ya muda kichwa kinaanza kuniuma sana nasikia kizunguzungu mpaka nikae baada ya muda kama masaa 3 ndo napata nafuu wandugu nisaidieni tatizo ni nini?

Nenda hospitali kapime kisukari.
 
Back
Top Bottom