Kunywa dawa huku umesimama ni moja ya masharti ya babu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunywa dawa huku umesimama ni moja ya masharti ya babu?

Discussion in 'JF Doctor' started by Hmaster, Apr 4, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawasalimu wanajf wote. Naanza kwa kuomba samahani kwa vile naelewa wazi kuwa thread hii si pure siasa.
  Nimekuwa nikifuatilia picha zinazopigwa huko Loliondo kwa babu, jambo lililonifanya niwaulize nyie wenzangu ni huu utaratibu wa kunywa dawa huku wagonjwa wakiwa wamesimama. Je haya ni masharti au ni haraka tu ya wagonjwa wenyewe? Kama si masharti ina maana hata mabenchi ya kukalia yameshindikana kupatikana kwa ajili hiyo? Dawa ni kitu cha kuheshimika sana na hasa hiyo inayoambatana na imani ya kidini, sasa ni vipi inywewe kwa kusimama? Hepu shuhudia picha hii hapa chini.

  [​IMG]
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  MaRC Kandoro na Dr Balele walikunywa wamekaa.
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi kumbe tangu mwanzo hamkujua kwamba babu wa Loliondo ni mganga wa kienyeji na mtumishi wa shetani na hivyo kuwa na sifa ya kuitwa mshirikina-ushirikina ni ushirika na mashetani???? Au kwa kuwa alijitambulisha kama mchungaji??? Elewa sasa, na pia soma magazeti ya leo 4/4/2011 ya UHURU, HABARILEO,na DIRA utapata habari kamili.
   
 4. S

  Smarty JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  yesu alisema nawaambieni watakuja watu wangu wakijifanya ni KRISTO, hao watawadanganya wengi na pia atakuja mtu akijifanya katumwa na mungu na kuwa atataibu magonjwa mengi na wengi wataamini na kumsahau mungu wao,na mataifa mbalimbali watamfuata, hakia mkimuona mtu huyo ujue hiyo ni dalili ya siku ya mwisho kukaribia. TAFAKARI CHUKUA HATUA....................
   
 5. D

  Denice Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  mi nadhani uelewa mdogo na fikra mbovu mlizonazo ndo zinawaponza.we unadhani folen inayokuweepo kwa babu kila mtu angekuwa angekuwa anashuka na kukalia bench unazosema ni wangapi wangepata huduma?na mi nadhani we sio mfatiliaji maana kwa babu watu waokuwa kqwenye magar wanapewa dawa wakiwa kwenye magar yao ili kuarakisha zoezi, babu anajaza vikombe na wahudum wana wapa watu.au unataka kusema hata wakiwa kwenye magar wanaambiwa wasimame?kama unaumwa kanywe dawa ndugu bt kama we ni mzima waache wagonjwa wapate huduma.
   
 6. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu MGANGA WA LOLIONDO mbona mnampaisha saaaana?? shetani amewajaza utando hata msiweze kuhoji lolote na mnakuwa wakali na kuwashambulia wale wanaojaribu kuwaelimisha. SASA ni bora tuwaache...:disapointed:

  Ni miujiza mingapi inafanyika kanisani tena kwa uthibitisho wa vyeti na haipewi kipaumbele kwenye media kama huyo MGANGA WA LOLIONDO? Poleni mliokunywa na mnaofikiria kunywa, hakuna aliyeyepona na kama yupo na aweke vyeti hapa JF vya kabla na baada, sio kutuletea porojo sa KUSIKIA...

  Mungu awasaidie mfunguke akii na mje kanisani tuwaombee na kuvunja hiyo minyororo na mikataba(maagano) mliyoingia na shetani bila kujua, (kwa kunywa dawa inaotolewa kimasharti ya kiuganga) Mje mnywe damu ya thamani ya YESU na nyie mtaona tofauti.
   
 7. d

  digodigo Senior Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Je ikiwa kweli katumwa na Mungu na pia bado anashauri watu wasimsahau Mungu wao maana kabla hajaanza shughuli huanza kwa kupiga sala.
   
 8. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Mkuu ingekuwa watu wote wanakunywa wamekaa nalo pia ingekuwa nongwa..........

  Umenikumbusha mtu aliezoea kuona nguo nyekundu kuvaliwa na waganga wa kienyeji kwenye filamu, siku kaona kwaya (nadhani wimbo we Kekundu sijui kwaya gani) kisa wamevaa nyekundu anasema ni wa kishetani maana wamevaa nyekundu tupu na asilimia kubwa ya nyimbo zao kunatokeza rangi nyekundu

  Kweli Mungu anayo kazi
   
 9. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Inaonesha hata kwenye ATM huko kwenu kuna mabenchi. Pale kwa Babu hakuna prescription inayotolewa ila dawa tena kwa haraka,ile si pombe hadi watu wakae chini.

  Wanaodai Babu ni mfuasi wa Shetani kama D5,watatuthibitishia vipi kuwa wao si wahudumu wa kuzimu wanaopotosha jamii juu ya tiba ya babu? Kama Kakobe na Mwingira ni watumishi wa Mungu wa kweli ni kwanini wasimuombe Mungu amteketeze Babu badala ya kutulalamikia sisi? Ni kwanini wapinge Babu kupokea 500 wakidai kuwa Mungu haitaji hela kuponya,vipi wao hawapokei chochote makanisani kwao?
   
Loading...