SoC01 Kunyonyesha watoto wanne miezi 6 mfululizo (EBF) huku nikisoma Chuo, nikiwa mwajiriwa, mama na mke

Stories of Change - 2021 Competition

Lamkyeku

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
494
661
Habarini wana jukwaa na wapiga kura!

Naomba leo niandike historia yangu fupi kidogo huku lengo likiwa ni msisitizo kwa wanawake wote wanaopambana kujenga familia imara huku wakiwa na ndoto mbalimbali.

Mimi ni mama miaka 30, nimezaliwa huko Kaskazini mwa Tanzania, shule ya vidudu mpaka kidato cha nne niliipata huko huko Kaskazini, kidato cha 5 na 6 nilisomea Kanda ya Ziwa na Shahada ya kwanza niliipata huko Kanda ya Kati.

Baada ya kuhitimu 2014 niliingia mtaani kujitolea kampuni fulani kwa miezi 6, ambapo 2015 niliingia rasmi Jijini Dar. Katika pitapita zangu za kusaka ajira nilipata kibarua kwenye kampuni moja ya utangazaji hapa mjini. Baadae nikakutana na baba mmoja wa Makamu ambaye amenipita miaka 25 na tukaanzisha mahusiano.

Mwaka 2017 nilianza kusoma Shahada yangu ya pili katika chuo kikuu cha Dares salaam ambapo mwaka huo huko nilijigundua nimepata ujauzito.

Maisha yaliendelea ambapo baada ya kujadiliana na mwenzangu tulikubaliana kwamba tuanze kuishi pamoja kwakuwa na yeye walitalikiana na mkewe miaka 7 iliyopita. Maisha yakaanza rasmi, hapo nilihitajika kwenda kazini asubuhi mpaka saa tisa, saa 11 jioni niingie darasani na kutoka saa 2 usiku (Ilikuwa Evening class) halafu nirudi nyumbani kwa ajili ya kuhudumia familia ambapo mume wangu alikuwa na watoto 2 wakubwa, mmoja alikuwa chuo kikuu na mwingine kidato cha tano. Na hapo tayari nilikuwa na ujauzito, nilipitia kila aina ya changamoto lakini nikaamini kwamba maisha ni mapambano. Na hii ni kutokana na maisha niliyoishi hapo nyuma ambapo yalinifanya niwe mpambanaji (story nilishare hapa miaka ya nyuma).

Maisha yaliendelea hivyo na mwanzoni 2018 nilijifungua mtoto wangu wa kwanza, nilipitia changamoto za uzazi lakini namshukuru Mungu zilipita. Nililazimika kumuacha mtoto wa mwezi mmoja ili niende chuoni, lakini nilishaamua kwamba mwanangu nitamnyonyesha miezi sita bila kumpa chochote.

Nilinunua pampu yangu nikawa nakamua maziwa na kuweka kwenye chupa na kumuachia dada na ziada niliweka kwenye jokofu ili awe anampa mtoto nikiwa chuoni. Miezi mitatu ikaisha nikarudi kazini ratiba ikarudi kama kawaida kuondoka nyumbani saa 12 na kurudi saa 3 lakini pamoja na yote mtoto aliendelea kupata maziwa ya mama.

Baada ya miezi 6 kazini tulipunguzwa na mimi nikiwa mmoja wapo, lakini nilifanikiwa kupata kibarua kingine sehemu ambapo ofisini unaingia saa 12 asubuhi na kutoka saa 8 mchana, hii ilikuwa ni ahueni kidogo kwangu kwa sababu nilipata muda wa kurudi nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani kabla ya kuingia darasani saa 11.

Mtoto akiwa na miezi 7 nilijigundua nina ujauzito mwingine ambao ulinisumbua sana, baada ya kuanza kliniki nilikutwa na ujauzito wa mapacha. Changamoto zilizidi kuwa kubwa kwakuwa nilikuwa na mtoto mdogo tayari, nilikuwa nina masomo ya kuhudhiria, nilikuwa nina familia nyumbani pamoja na mume na bado nilitakiwa kwenda kazini.

Niliendelea kumnyonyesha huyu wa kwanza mpaka mimba ilipotimiza miezi 8 ambapo alikuwa na mwaka na miezi miwili, nilimwachisha lakini nikaendelea kumkazania chakula bora chenye makundi yote ya chakula ili asipate utapiamlo na alikuwa na afya nzuri sana.

Mwaka 2019 katikati nikajifungua kwa upasuaji watoto mapacha, safari nyingine ya unyonyeshaji ikaanza, na sasa chuoni nilishamaliza vya kusomea darasani ulikuwa ni muda wa kufanya utafiti. Niliendelea kukamua maziwa na kuwawekea kwenye chupa na mengine kuhifadhi , ila safari hii ilikuwa changamoto sana maana walikuwa ni wawili ila walikunywa maziwa ya mama pekee miezi yote sita.

Safari yangu ya maisha ikaendelea ambapo niliendelea na kazi pale wizarani lakini nilisumbuliwa sana na mgongo sababu ile kazi ilihitaji ukae kwenye compyuta muda mrefu na nilikuwa nimejifungua kwa upasuaji. Ilipofika Desemba mwaka 2019 ile projekti iliisha nikaendea na utafiti wangu ili nikamilishe shahada yangu ya uzamili.

2020 mwezi wa 6 nilijigundua nina ujauzito mwingine wa tatu ila atakuwa ni mtoto wa nne maana nilikuwa na mapacha, nilimshirikisha mwenzangu na kwakuwa aliona jitihada zangu alijua kabisa sitashindwa kuwalea watoto, hivyo tulikubaliana tuilee mimba.

Mungu si athumani mwaka jana baada ya muda mrefu nilitunukiwa Shahada yangu ya uzamili na kuibuka kuwa mwanafunzi bora wa mwaka na kupata udhamini wa kusoma shahada ya Uzamivu. Wakati huo nilikuwa na ujauzito wa miezi 3 lakini niliendelea kuwanyonyesha watoto mapacha.

Baada ya shamrashamra kuisha nilianza kutulia kidogo maana shule nilikuwa nimemaliza na kazi sikuwa nayo hivyo nilipata muda wa kuwahudumia watoto.

Niliendelea kuwanyonyesha mpaka Januari mwaka huu wakiwa na mwaka na nusu. Mwezi wa pili nilijifungua mtoto wangu wanne (wa mwisho) ambae sasa ana miezi 5, nimebakiza mwezi mmoja tu nikamilishe kumyonyesha bila kumpa chochote kwa miezi 6 ya mwanzo.

Watoto wote wanne wana afya, wamechangamka, hawaugui hovyo, huyu wa kwanza ameanza shule na anafanya vizuri darasani!

Baada ya kujifungua huyu wa mwisho nikiwa ndani nilianza kusoma kuhusu biashara ya kununua na kuuza hisa/ fedha za kigeni (forex trading) kutokana na uzi uliopo huku miaka mingi, nimesoma vitabu 10 ndani ya miezi 3 na sasa nimeanza rasmi kufanya trading nikiwa nyumbani na namshukuru Mungu napata chochote kwa ajili ya kusaidia kutunza familia huku nikitafuta mtaji kwa ajili ya kufungua kampuni yangu ya GIS ambapo taratibu za mwanzo nimeshakamilisha. Bado nina ufadhili wa masomo ya PhD ambapo nimesogeza mbele kidogo.

NB: Watoto wale wakubwa mmoja alimaliza shule ya Sheria na kupata Uhakimu na mwingine anasomea Udaktari.

Hitimisho
1. Watoto wanaonyonyeshwa miezi 6 wana afya ya mwili na akili hawasumbuliwi na magonjwa hivyo kumpa mama nafasi ya kufanya mambo mengine. Pia, unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya baadae.

2. Kwa wanawake wote wanaopambana kujenga familia zao na kujenga career zao ningependa ujue una nguvu ndani yako ambayo kama ukianza kuitumia utajishangaa kwa matokeo utakayoyapata. Bila kujali jana yako una nafasi ya kutengeneza kesho iliyo njema.

3. Wenza wote mlio na wenza wenye ndoto wasaidieni katika kutimiza ndoto zao, kwa ajili ya manufaa ya familia, jamii na taifa.

4. Wizara ya Afya na taasisi zote zinazohusika na afya ya Mama na mtoto watoe elimu kuhusu unyonyeshaji kwani kuna upotoshaji mkubwa juu ya unyonyeshaji, mfano kutomnyonyesha mtoto ukiwa mjamzito au kutolala na mtoto ukiwa mjamzito kwa woga wanaoita kubemenda.

Pia Elimu kuhusu ukamuaji na uhifadhi ya maziwa ya mama kwa matumizi ya baadae ambapo yanaweza kukaa mpaka miezi 6 katika friza bila kuharibika.

5. Mapenzi hayana umri!
 
Hongera Sana.Hapo kufanya exclusive breastfeeding kwa miezi SITA ya mwanzo ni muhimu Sana.Mwanangu ana miaka miwili hatujui hospitali nje ya kufuata chanjo.
Nilikuwa making Sana wife asimpe chochote
 
Yes ni muhimu sana, wamama wengi hawalijui hili! Pia hongera kwa kumsupport wife kwenye safari yake ya unyonyeshaji.
 
Hongera sana Mdada. Ila nimeona vile Attitude na Mindset yako ilivyotofauti na wanawake wengi. Wa dada wenye umri mdogo ambao bado wanayo nafasi ya kupambana na kufikia ndoto zao wana cha kujifunza kwako.

@Darlin
 
Kila mtu ana nguvu ndani yake ambayo kama akianza kuitumia atajishangaa kwa matokeo utakayoyapata, kitu kikubwa kinachowashida wadada wengi ni ule uthubutu/jinsi ya kuanza na kuwaza hivi nikishindwa itakuwaje but "A journey to thousand miles begin with a single step" na Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu!!!
 
Habarini wana jukwaa na wapiga kura!

Naomba leo niandike historia yangu fupi kidogo huku lengo likiwa ni msisitizo kwa wanawake wote wanaopambana kujenga familia imara huku wakiwa na ndoto mbalimbali.

Mimi ni mama miaka 30, nimezaliwa huko Kaskazini mwa Tanzania, shule ya vidudu mpaka kidato cha nne niliipata huko huko Kaskazini, kidato cha 5 na 6 nilisomea Kanda ya Ziwa na Shahada ya kwanza niliipata huko Kanda ya Kati.

Baada ya kuhitimu 2014 niliingia mtaani kujitolea kampuni fulani kwa miezi 6, ambapo 2015 niliingia rasmi Jijini Dar. Katika pitapita zangu za kusaka ajira nilipata kibarua kwenye kampuni moja ya utangazaji hapa mjini. Baadae nikakutana na baba mmoja wa Makamu ambaye amenipita miaka 25 na tukaanzisha mahusiano.

Mwaka 2017 nilianza kusoma Shahada yangu ya pili katika chuo kikuu cha Dares salaam ambapo mwaka huo huko nilijigundua nimepata ujauzito.

Maisha yaliendelea ambapo baada ya kujadiliana na mwenzangu tulikubaliana kwamba tuanze kuishi pamoja kwakuwa na yeye walitalikiana na mkewe miaka 7 iliyopita. Maisha yakaanza rasmi, hapo nilihitajika kwenda kazini asubuhi mpaka saa tisa, saa 11 jioni niingie darasani na kutoka saa 2 usiku (Ilikuwa Evening class) halafu nirudi nyumbani kwa ajili ya kuhudumia familia ambapo mume wangu alikuwa na watoto 2 wakubwa, mmoja alikuwa chuo kikuu na mwingine kidato cha tano. Na hapo tayari nilikuwa na ujauzito, nilipitia kila aina ya changamoto lakini nikaamini kwamba maisha ni mapambano. Na hii ni kutokana na maisha niliyoishi hapo nyuma ambapo yalinifanya niwe mpambanaji (story nilishare hapa miaka ya nyuma).

Maisha yaliendelea hivyo na mwanzoni 2018 nilijifungua mtoto wangu wa kwanza, nilipitia changamoto za uzazi lakini namshukuru Mungu zilipita. Nililazimika kumuacha mtoto wa mwezi mmoja ili niende chuoni, lakini nilishaamua kwamba mwanangu nitamnyonyesha miezi sita bila kumpa chochote.
Nilinunua pampu yangu nikawa nakamua maziwa na kuweka kwenye chupa na kumuachia dada na ziada niliweka kwenye jokofu ili awe anampa mtoto nikiwa chuoni. Miezi mitatu ikaisha nikarudi kazini ratiba ikarudi kama kawaida kuondoka nyumbani saa 12 na kurudi saa 3 lakini pamoja na yote mtoto aliendelea kupata maziwa ya mama.

Baada ya miezi 6 kazini tulipunguzwa na mimi nikiwa mmoja wapo, lakini nilifanikiwa kupata kibarua kingine sehemu ambapo ofisini unaingia saa 12 asubuhi na kutoka saa 8 mchana, hii ilikuwa ni ahueni kidogo kwangu kwa sababu nilipata muda wa kurudi nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani kabla ya kuingia darasani saa 11.

Mtoto akiwa na miezi 7 nilijigundua nina ujauzito mwingine ambao ulinisumbua sana, baada ya kuanza kliniki nilikutwa na ujauzito wa mapacha. Changamoto zilizidi kuwa kubwa kwakuwa nilikuwa na mtoto mdogo tayari, nilikuwa nina masomo ya kuhudhiria, nilikuwa nina familia nyumbani pamoja na mume na bado nilitakiwa kwenda kazini.

Niliendelea kumnyonyesha huyu wa kwanza mpaka mimba ilipotimiza miezi 8 ambapo alikuwa na mwaka na miezi miwili, nilimwachisha lakini nikaendelea kumkazania chakula bora chenye makundi yote ya chakula ili asipate utapiamlo na alikuwa na afya nzuri sana.

Mwaka 2019 katikati nikajifungua kwa upasuaji watoto mapacha, safari nyingine ya unyonyeshaji ikaanza, na sasa chuoni nilishamaliza vya kusomea darasani ulikuwa ni muda wa kufanya utafiti. Niliendelea kukamua maziwa na kuwawekea kwenye chupa na mengine kuhifadhi , ila safari hii ilikuwa changamoto sana maana walikuwa ni wawili ila walikunywa maziwa ya mama pekee miezi yote sita.

Safari yangu ya maisha ikaendelea ambapo niliendelea na kazi pale wizarani lakini nilisumbuliwa sana na mgongo sababu ile kazi ilihitaji ukae kwenye compyuta muda mrefu na nilikuwa nimejifungua kwa upasuaji. Ilipofika Desemba mwaka 2019 ile projekti iliisha nikaendea na utafiti wangu ili nikamilishe shahada yangu ya uzamili.

2020 mwezi wa 6 nilijigundua nina ujauzito mwingine wa tatu ila atakuwa ni mtoto wa nne maana nilikuwa na mapacha, nilimshirikisha mwenzangu na kwakuwa aliona jitihada zangu alijua kabisa sitashindwa kuwalea watoto, hivyo tulikubaliana tuilee mimba.

Mungu si athumani mwaka jana baada ya muda mrefu nilitunukiwa Shahada yangu ya uzamili na kuibuka kuwa mwanafunzi bora wa mwaka na kupata udhamini wa kusoma shahada ya Uzamivu. Wakati huo nilikuwa na ujauzito wa miezi 3 lakini niliendelea kuwanyonyesha watoto mapacha.

Baada ya shamrashamra kuisha nilianza kutulia kidogo maana shule nilikuwa nimemaliza na kazi sikuwa nayo hivyo nilipata muda wa kuwahudumia watoto.

Niliendelea kuwanyonyesha mpaka Januari mwaka huu wakiwa na mwaka na nusu. Mwezi wa pili nilijifungua mtoto wangu wanne (wa mwisho) ambae sasa ana miezi 5, nimebakiza mwezi mmoja tu nikamilishe kumyonyesha bila kumpa chochote kwa miezi 6 ya mwanzo.

Watoto wote wanne wana afya, wamechangamka, hawaugui hovyo, huyu wa kwanza ameanza shule na anafanya vizuri darasani!

Baada ya kujifungua huyu wa mwisho nikiwa ndani nilianza kusoma kuhusu biashara ya kununua na kuuza hisa/ fedha za kigeni (forex trading) kutokana na uzi uliopo huku miaka mingi, nimesoma vitabu 10 ndani ya miezi 3 na sasa nimeanza rasmi kufanya trading nikiwa nyumbani na namshukuru Mungu napata chochote kwa ajili ya kusaidia kutunza familia huku nikitafuta mtaji kwa ajili ya kufungua kampuni yangu ya GIS ambapo taratibu za mwanzo nimeshakamilisha. Bado nina ufadhili wa masomo ya PhD ambapo nimesogeza mbele kidogo.

NB: Watoto wale wakubwa mmoja alimaliza shule ya Sheria na kupata Uhakimu na mwingine anasomea Udaktari.

Hitimisho
1. Watoto wanaonyonyeshwa miezi 6 wana afya ya mwili na akili hawasumbuliwi na magonjwa hivyo kumpa mama nafasi ya kufanya mambo mengine. Pia
unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya baadae.

2. Kwa wanawake wote wanaopambana kujenga familia zao na kujenga career zao ningependa ujue una nguvu ndani yako ambayo kama ukianza kuitumia utajishangaa kwa matokeo utakayoyapata. Bila kujali jana yako una nafasi ya kutengeneza kesho iliyo njema.

3. Wenza wote mlio na wenza wenye ndoto wasaidieni katika kutimiza ndoto zao, kwa ajili ya manufaa ya familia, jamii na taifa.

4. Wizara ya Afya na taasisi zote zinazohusika na afya ya Mama na mtoto watoe elimu kuhusu unyonyeshaji kwani kuna upotoshaji mkubwa juu ya unyonyeshaji, mfano kutomnyonyesha mtoto ukiwa mjamzito au kutolala na mtoto ukiwa mjamzito kwa woga wanaoita kubemenda.
Pia Elimu kuhusu ukamuaji na uhifadhi ya maziwa ya mama kwa matumizi ya baadae ambapo yanaweza kukaa mpaka miezi 6 katika friza bila kuharibika.

5.Mapenzi hayana umri!
MashaAllah wee Mwanamke mmoja tu unawazidi waTz milioni 60 !!
Ubarikiwe sana..
 
Sasa tulia
Ngoja nitulie...ila saafi..umenikumbusha mdada m1 mwimbaj nyimbo za injili nakumbuka mim nikiwa 1st yr udam yeye ndo anamaliza...yaan yule dada kila nikikutana nae ana mimba...nahis ana watoto 8 yule...saaafi lakin..vzur...pambana pia kutengeneza wealth dada sio kufyatua tu...hyo era ilishapitwa na wakat ya mmama watoto 6++
 
Jifunze kuandika vizuri kwanza!
 
Ndio wapiga kura wako hao hala hallaa ohoo
Hahah usimtishe..mi mbona lazima nimpigie kura malkia wa nguvu kwenye sekta hyo ya ufyatuaj na umuhimu wa mtoto kunyonya.....

Ana point ya msing...watu hawajui kuwa maziwa yale ya mama sanasana ya kwanza ndo kila kitu kwa mtoto..yaan maisha ya mtoto kuanzia kinga..akili yanategemea snaa maziwa hayo

Madem zetu hawa ambao hawatak nyonyesha ndio wanaotuletea vizaz vya ajab vya kina amba ruty..hahahaha

So kwa hilo la kunyonyesha nampa kongole sana mtoa mada...aelekeze namna ya kumpigia kura tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom