Unyonyeshaji bora wa maziwa ya mama na maziwa mbadala iwapo ni lazima

Duh jamani kunyonyesha hadharani sio vibaya, but i wdnnt go unleashing my gals to everbody. So my suggestion kama ikiwezekana mama ajistiri, they call them nursing covers but u surely can improvise, nyumbani hasa kanga will be great, na kila mtu anayo ama???

pili, if its in avery busy place, it wd be good to move to a less busier area to avoid distractions and be more at ease, if you are tense maziwa yatagoma etc.

tatu, dont forget to wipe/clean tits before feeding.

fourth: this is the greatest way to establish a bond with your baby, so lets keep breastfeeding!!!!!

nakubaliana nawe,lakini kumbuka kuwa katika kutengeneza bond hiyo kati ya mama na mtoto,kujifunika au kufunika mtoto inaweza kuaffect kwa namna fulani.mara nyingi mtoto anapontonya basi anakuwa anaangaliana na mama yake kwa namna ambayo kwa kweli ni wao wawili pekee wanaweza kuielezea,so affectionetly.kwa mawazo yangu kumfunika mtoto itaharibu ukaribu huu wa mtoto na mama.sijui kama nipo for or against public breastfeading....
 
...if you have got it, flaunt it!! -God given assets shouldn't go hidden!

...and it is right time to practice if you haven't so far, do you need help on this?!



Kunyonyesha si vibaya.

But being a lady, and normally used to cover some of your body parts which are never shown in public, one needs to cover herself to feel comfortable.
I can not imagine, all passers-by looking at my breasts while feeding my baby!
Can't stand that!!!
Guess it goes with ones feelings as well. Siwezi, i feel shy!

Mnasemaje hapo?
 
What's wrong with breast feeding? Acheni madogo wapate haki zao.....kama wenyewe mnaona wivu, nyonyo kuonwa na wengine then acheni kuzaa.
 
mimi naona hakuna haja ya kunyonyesha hadharani, kama hakuna dharura.
kunyonyesha si kutoa ziwa na kuweka mdomoni mwa mtoto.
ni kujiandaa kisaikolojia mama na mtoto, kujiandaa kiafya na kujiandaa kimkao.
Ili unyonyeshaji uwe wa ufanisi, hadhara si mahali pazuri.
Hakuna usafi, hakuna utulivu wala hakuna position nzuri ya mama na mtoto kukaa.
Ushauri, (kama hakuna dharura)
Kupiga kelele (stori za mashoga) na kuhangaika si busara wakati mtoto ananyonya.
 
mimi mtoto wangu ni wa kiume anataka mimi nikae yeye asimame ndo anyonye alafu anataka nimtolee yote mawili anyonye hili ashike hili sasa hapo nitajisetiri vipi
 
mimi mtoto wangu ni wa kiume anataka mimi nikae yeye asimame ndo anyonye alafu anataka nimtolee yote mawili anyonye hili ashike hili sasa hapo nitajisetiri vipi

... :D mitoto mingine bana, utotoni weshaanza balaa, ...

...uamuzi ni wako JONGOMERO, madhali keshafikia umri wa kusimama na kutaka wewe ukae, akili ishaanza kumwingia huyo, STOP him upate kujistiri.
 
... :D mitoto mingine bana, utotoni weshaanza balaa, ...



:oops:
Mchongoma noma sana, mitoto, mijitoto, hii kasheshe kali, huyo azitaka nyonyo zote mbili apewe sima sasa, inaonekana keshapita umri wa kunyonyeshwa!!
 
Mimi wakwangu mapacha. Japo huwa hatutoki mara kwa mara kwa ajili ya inconvenience ila tukitoka wakililia nyonyo wanalilia kwa wakati mmoja, hata kama mmoja hana njaa akimuona mwenzie anapata msosi na yeye anataka, hawajali tupo wapi, kwenye basi, kwenye foleni ya hospitali popote pale,
hawapendi kufunikwafunikwa wakati wakula kwa hiyo hata huyu msaidizi akianza kufunika funika inakuwa balaa, manake watalia kwa kelele hao na kuattract everybody's attention.
Kuna hizi blauzi zenye matundu kwa ajili ya kujisitiri kidogo, kwa kweli zinanisaidia kufichaficha tumbo tu na seheme nyinginezo - hazisaidii sana
 
Last edited:
Mie binafsi sipendi kuona mama ananyonyesha hadharani. Kama kuna uwezekano ni bora mama anyonyeshe pahali faragha kidogo(ajisitiri) ila kama ndio hakuna budi halaumiki.

ni hayo tu.
 
Sioni tatizo lolote kuknyonyesha mtoto hadharani na wala siwafikirii vibaya wanaofanya hivyo na tena mtoto ni bora kuliko kuonyesha hilo ziwa la mama.

Tatizo langu ni kama lako.. sipendi watu waone ziwa la wife akinyonyesha! Ni hapo tu!
 
Family Wellness is not the place to be,
when Mommy wants to breastfeed me,
They sent us to where the ladies pee,
My swimming siblings she can no longer see,
I ask myself how can this be?
I'm newborn and just want a full belly!
What if my siblings get scared we're not there,
Because my bottle under her shirt she did bare;
I ask that you all just give mommy a break;
I'm fussy and thirsty for gosh golly sake!

AUTHOR - UNKNOWN
 
binafsi sidhani kama kuna ubaya tukumbuke kuwa watoto hawachagui muda wala saa ya kula. Wao si kama watu wazima ambao wanaoutashi wa kuchagua kutoka oficini waende Break Point au Rose Garden wakale. Mtoto njaa ikimwuuma mama uwe ndani ya basi, uwe beach au uwe hospitalini utanyonyesha na ni haki ya mtoto.

Cha muhimu ni kuwa angalau mama unatakiwa ujifunike hata kama ni kwa baby shaw ya mtoto. Funika kidogo si kuzuia watu wasione but kuzuia vumbi na takataka nyingine zitokanazo na upepo zisichafue plate ya mtoto.

Ni mtazamo wangu tu
 
hivi kweli mtu anaweza kutoka nyumbani kwake na kwenda kumnyonyeshea mtoto wake pale kongo k/koo au mnazi mmoja? Kimsingi hata wale wanaonyonyesha hadharani ni kwa sababu huwa hakuna njia mbadala ya kumtuliza mtoto.Nimesikia mara nyingi ktk daladala watu wakimlazimisha mama kumnyonyesha mtoto wake. kwa hiyo jamii yetu haina tatizo na uleaji wa watoto wetu.

Mtoto mdogo ambaye anaweza kula chakula kingine kama uji unaweza kumwandaa mapema ili asije akadai chakula hadharani.Tuachane na wale wanaoogopa nido zao kuanguka. Kimsingi kama hakuna ulazima wa mama kumnyonyesha mtoto hadharani si vizuri kufanya hivyo.
 
Kila mwaka, Agosti 1 hadi 7, Tanzania hujumuika na nchi nyingine duniani huadhimisha wiki ya unyonyeshaji, lengo likiwa ni kusisitiza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.

Wiki hii imewekwa maalum ili kutilia mkazo umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto kama inavyosisitizwa kwenye Azimo la Innocenti, lililopitishwa rasmi mwaka 1990 na wajumbe wa mkutano uliohusisha Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (Unicef).

Azimio hili lilipitishwa baada ya kuona kuwa jamii nyingi duniani zilikuwa zinaanza kupuuza kunyonyesha maziwa ya mama na kuona kuwa maziwa ya kopo yanaweza kutumika badala yake, jambo ambalo lina madhara, sio tu ya kiafya bali hata ya kijamii.

Ingawaje kuna baadhi ya akina mama hulazimika kutowanyonyesha watoto wao kabisa kutokana na sababu za kiafya kama vile maziwa kutotoka au matiti kupata uambukizo, wako ambao hawataki kuwanyonyesha watoto wao kwa sababu za ovyo kama vile eti matiti yao yataanguka. Wapo hata wale wanaodhani maziwa ya kopo ni bora zaidi.

Wataalam wanaeleza kuwa mtoto anatakiwa kuanza kunyonyeshwa walau ndani ya saa moja tangu kuzaliwa na kuhakikisha kuwa maziwa ya mwanzo kabisa ambayo mara nyingi yana rangi ya njano hayakamuliwi chini kwani yana viini lishe muhimu na humsaidia mtoto kupata kinga dhidi ya magonjwa walau kwa miezi 12 ya mwanzo.

Ili mtoto aweze kunufaika na unyonyeshaji huu, inasisitizwa kuwa mtoto anyonyeshwe kwa miezi sita mfululizo bila kupewa kitu kingine chochote kwani anapopewa vitu vingine kama maji ya matunda, uji na hata maji, inachangia kupata uambukizo wa magonjwa mengine kutokana na utayarishaji wa vitu hivyo kutokuwa wa uhakika sana na pia inasisitizwa hivyo kwa kuwa maziwa ya mama ni mlo kamili.

Utaratibu huu wa kunyonyesha bila kuchanganya na aina nyingine yoyote ya chakula una faida kubwa pia kwa akina mama wanaonyonyesha ambao wana virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi (VVU) kwani husaidia mtoto asipate uambukizo wa virusi hivyo.

Faida hii pia huwanufaisha hata watoto ambao mama zao hawana VVU kwani huweza pia kuwakinga wasipatwe na magonjwa mengine kama kuhara, mafua na magonjwa mengine. Ni kutokana na hali hii ndiyo maana wataalam wanasema kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama una uhusiano mkubwa katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Kijamii mama anayemnyonyesha mtoto maziwa yake hujenga uhusiano wa karibu na kumjenga mtoto hali ya kujiamini na mapendo kati ya mama na mtoto huwa makubwa. Kadhalika, baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba mtoto aliyenyonya maziwa ya mama anakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kiakili ikilinganishwa na aliyetumia maziwa ya kopo.

Kwa maneneo mengine, tunapoongelea unyonyeshaji wa maziwa ya mama tunaongelea suala zima la ulinzi, uhai na usalama wa mtoto katika makuzi yake, jambo ambalo linatiliwa mkazo chini ya Malengo ya Milenia yenye nia ya kuleta maendeleo hasa kwa nchi maskini kama Tanzania.

Kwa njia ya unyoyeshaji, watalaamu wanasema, tutaweza kupunguza magonjwa mbali mbali, utapiamulo kwa watoto na kuwaandaa watoto ambao siku za baadaye wataweza kumudu vizuri elimu yao na maisha yao kwa ujumla.

Tunahakika hakuna mama anayetaka kumpoteza mtoto wake au hata kama atapona awe ni mtoto mbumbumbu ambaye hawezi kumudu mambo muhimu katika jamii kutokana na kuwa na afya dhaifu tangu utoto wake.

Kama ndivyo, ni jukumu la jamii na serikali kwa ujumla kuhakikisha kuwa akina mama wanaelewa umuhimu wa kuwanyonyesha watoto wao. Hili litaweza kufanikiwa zaidi iwapo akina mama wengi zaidi watahudhuria kliniki wakati wa ujauzito na kujifungulia kwenye hospitali.

Hospitali nazo zinatakiwa kuwa rafiki kwa akina mama wajawazito na wanaojifungua kwa kuwaelimisha toka mwanzo juu ya umuhimu wa kunyonyesha watoto wao na jinsi ya kunyonyesha.

Hilo litawezekana endapo katika kila hospitali wakunga ambao ndiyo huwahudumia akina mama hawa, watatoa elimu hiyo kwa akina mama na kuhakikisha elimu hii inakuwa ya lazima.

Tunapenda pia kutoa angalizo kwamba pale itakapolazimu mtoto apewe maziwa mbadala tangu anapokuwa mchanga, kuna haja ya serikali kuhakikisha kuwa maziwa hayo yanayoingia nchini hayaharibu afya za watoto na ni salama.
http://www.ippmedia.com/
 
Kunyonyesha mtoto kunamsaidia pia mwanamke kupunguza huwezekano wa kupata saratani ya matiti (breast cancer).
 
yaani mie nilikuwa nanyonyesha wakakti wowote mtoto atakapojickia kunyonya. bila haya wala nini, na hata nikiwa home cjifuniki cjui khanga cjui nini najiachie na yeye atupetupe miguu kwa raha zake....
 
yaani mie nilikuwa nanyonyesha wakakti wowote mtoto atakapojickia kunyonya. bila haya wala nini, na hata nikiwa home cjifuniki cjui khanga cjui nini najiachie na yeye atupetupe miguu kwa raha zake....

hehehehe...tutegemee mwingine lini Mrs?
 
wa kwangu huwa hataki kabisa kuonekana wakati ananyonyesha mtoto.
 
Well kwangu mimi najaribu kuangalia umuhimu kati ya ziwa lamama kuwa nje au mtoto kupata mlo wake kwa wakati ule, kama hakuna ulazima wa mtoto kunyonya kwa wakati huo ambao wewe uko kwenye maeneo ya wazi basi si vyema kujianika, ila kama kweli mtoto analia anataka kunyonya basi apewe ni haki yake ila ni vyema pia kujaribu kadri mama awezavyo kujisitiri, kwasababu naamini wakati ule ni muhimu sana kati ya mama na mtoto na unatakiwa u-relax, uwe comfortable ,uwe proud kwa kuwa Mwenyezimungu kakupa upendeleo wa kipekee wa kushika mimba na kupata huyo mtoto kama zawadi na pia kukupa uwezo wa kumnyonyesha mwanao bila ya tatizo lolote Coz not every woman has that opportunity. wangu alikataa kunyonya after two months nilijaribu kila njia lakini ikashindikana en he was my first born iliniuma sana nikawa nalia coz my dream was to breastfeed him mpaka miaka miwili kamili.
 
Back
Top Bottom