Kunyimwa dhamana kituo cha polisi kwa siku 12 sasa

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
858
Habarini wasomi,

Leo ni siku ya 12 nimenyimwa dhamana hapa kituo cha polisi baada ya kifunguliwa kesi ua jinai kwa kujioatia pesa kwa njia ya udanyanyifu kitu ambacho siyo kweli kwani tulifanya biashara na mdai amekubali nimlipe kidogo kidogo lakini polisi wanataka nilipe nusu ya 15mln ninayodaiwa na nipate mdhamini ambaye ni mtumishi wa umma akiwa na barua ya mwajiri.

Nifanyeje kwani mpelelezi na uongozi wa polisi mkoa hawataki kunielewa kabisa.

Nasubiri.
 
Shinikiza kesi ikaendeshwe mahakam kama unao uhakika aliekushtak hawezi kuizunguka mahakama
 
Ukitoka hapo washitaki mkuu, hawaruhusiwi kukaa na wewe mda wote huo bila kukupeleka mahakamani.
 
Kama upo kizuizini(lock up) simu umepata wapi ndugu yangu?

Anyway:kwa wepesi wa jinai uliyonayo ni haki yako kupewa dhamana.
 
Kuna watu wanauliza simu jamaa katoa wapi

Kama gerezani vitu vinaingizwa vya kila aina itakuaje mahabusu?

Kuna kituo niliwahi kukaa siku 11 na niliona vingi sana suala la kuwa na simu hata siyo la ajabu.

Una pesa unapewa unachotaka. Simu zinawekwa kwenye vyombo vya kubebea chakula wewe utaona ni chakula analetewa kumbe ndani simu ipo na vocha juu.

Rushwa huwezi kuimaliza Tanzania hasa vituo vya polisi

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kesi yako dhamana iko wazi hao police wanataka noti tu so cha msingi komaa kesi iende mahakamani, pia waambie ndugu zako waandae wadhamini wawili. Mahakamani ukipelekwa tu unapata dhamana..achana na polisi hawajui wanachofanya. Pia ndugu wako waweke wakili aje hapo polisi utatoka kama upepo.
 
Back
Top Bottom