Kunyanyasika kwangu mie unlucky hili sio jina langu natumia tu

ndo mana leo nimerudi tena kuomba msaada wa mwisho manake nikimwambia mama anasema vumilia tu utaenda wapi utawalea vipi hao watoto watatau unanini nikimwambia mwingina ananiambia watoto waachie huyo mnyama awalee mwenyewe wewe kaanze maisha yako ukiwa peke yako utahangaika lakini na watoto utateseka watoto wake leo hataki hata kunioa sura yangu kafahamishwa na kaka yake lakini ye yupo pale pale kama mie basi jamani nifanye nini watoto niwasaliti nimwachie nisonge mbele kuliko kufanywa kama mnyama manake hata nikikimbia nao yeye anawataka watoto wake manake mara nyingi kasema we ondoka watoto waachie hapahapa mie nitawalea nikimwambia mwingine ananiambia ukichukua watoto utapata tabu mpaka dunia utaiona chungu gharaama zao utatoa wapi na utamwachia mwanya ya huyu bwana kustarehe nifanyeje hebu nisaidieni

Dada yangu wa kazi ana miaka 42' ana watoto watatu' alitokea kwenye ndoa dizaini yako. Ila maji yalipomfika shingoni alijua cha kufanya' yeye mwenyewe peke yake, bila ushauri wa yoyote anasema alipanda basi na kwenda dar kufanya kazi Za ndani
Alicha nyumba kubwa na watoto wake watatu plus wa mke mwenzie4.
Na hao watoto wanasoma secondary na analipa Ada.
Ipo siku utapata suruhisho la matatizo Ya ndoa yako' siku Hiyo ama utabeba kila kilicho chako' au utaacha Kila kitu na kuelekea usipopajua.
 
kweli mamn mie pia nimefikiria hivyo siwezi kwenda kuwatesa hawa watoto bora niondoke mie mwenyewe nikaanze maisha kuanzia mwanzo manake nikiwachukua watoto sitaweza kufanya chochote nitakuwa na stress kuwafikiria hawa watoto baba yao anauwezo atatunza tu kwanza nikiwachukua huyu bwana ndo atapata kustarehe vizuri bora akae nao ajue kulea inakuaje roho inaniuma mie mwenzenu naombeni mdada yoyote atakae weza kunisaidia kunipeleka ustawi wa jamii ili nichukue talaka yangu manake huyu bwana talaka kutoa ngumu kwake naomba jamani

Ustawi wa jamii hupelekwi na yoyote unaenda peke yako
Kama upo dar kila wilaya ina ofisi za ustawi
1.kinondoni b' maeneo Ya chuo cha tu
I
2.ilala' panaitwa kwa makamba
3.temeke' wilayani
Tena ustawi wanapenda sna kesi kama hizo 😄nenda mwaya
 
Pengine amebadilika, ni miaka mingi sasa imepita,
wapi unlucky useme kidogo hapa.
 
Last edited by a moderator:
Unajua kuna vitu vinauma kuvjua kuliko hata anayetendwa? Hebu nipe namba yake huyo mmeo mi niongee naye, hata kama hatanisikiliza lakini nitakachomwambia atakikumbuka daima. Na malipo ni hapa hapa duniani. NiPIM basi. Ila ni kama umesema jamaa ana mke mwingine na watoto watano, au sijaelewa? Kama uliingilia ndoa ya mwenzio basi ujue karudi zizini na anachokufanyia ni malipo yako kwa makosa uliyotenda.
 
Habari zenu wanajf haya habari mpya bwana kakimbia kaenda mbeya mpk leo hii hajarudi na kampigia simu mama na kumwambia kama hapo dar sirudi tena mie nitaishi hukuhuku mbeya haya sasa mnasemaje kuhusu hilo

Ndo vizuri, ustarehe kidogo, wew nawe unamtaka wa nini achana naeee
 
pole sana,miaka mitano uliyokaa ni mingi sana.una mchango mkubwa sana katika maisha yake.cha maana nenda ofis za ustawi wa jamii su kituo cha haki za binadamu au polisi watakusaidia sana.utapewa haki yako kama Mali mtagawana na watoto atawahudumia.Haya mambo ya kunyanyaswa kijinsia siku hiz serikal ipo makini sana
 
Kazi unayo dada' yaani maushari yote hayo bado tu!?
Kweli mapenzi upofu nimeamini.
Pole mwaya
 
Mbona miaka 29 kwa mwanamke inatosha kabisa hata kuongoza nchi?
Kwani foregner ndo nini?
Tena huyo mlaini hata kumbambika skendo na kumng'oa kabisa nchini

au hauishi TZ uko nchi ya ugenini?
Au umekua uiwa spoon fed?

Sipayuki najaribu kukuelewa na kuvaa viatu vyako afu sioni chalenji unayopata.
Mfukuze hapo kwenye nyumba tena mfukuze hasa.

huyu ana kila dalili ya ugonjwa wa kisaikolojia. Sijui alipitia makuzi gani. Wewe hutamwelewa, na yeye hatakuelewa kwa nini humuelewi. Yuko kwenye kifungo kibaya sana cha kiakili. Kitakachomfungua huko ni ukatili wa ziada utakaovuka mipaka atakaofanyiwa na huyu baba maana kama visa vyote alivyofanyiwa bado tu yupo unafikiri anasubiri nini? Akili yake iliyolala (subconscious mind) imeshazoea mateso na inajua mateso ndo mapenzi. Akili yake hai (conscious mind) inaona si sawa na ndiyo inayomleta mpaka huku JF kuomba ushauri lakini haina nguvu kama ile iliyolala. Huyu anahitaji counseling ya hali ya juu. Vinginevyo hata akienda tamwa na tgnp si ajabu kusikia baada ya miaka miwili kaolewa na bwana mwingine wa aina hii hii. Hapa mwanaume na mwanamke wote ni wagonjwa.

Hizi habari za watoto, sijui vitu vimefungiwa, mara sina baba, kaka hana msaada ni visingizio tu vya kubaki kifungoni. Mbona tumewaona wanaume kwa wanawake wakiondoka kwenye nyumba za ndoa, wakiacha vyote walivyochuma na pengine hata watoto? Watu wameondoka na nguo walizovaa tu na leo wamesimama. Waliokomalia kwenye mateso leo hii kama si marehemu basi ni wagonjwa na maskini. Huyu akizinduka mbona anaweza kubeba wanae akaenda nao hata msikitini au kanisani kuomba hifadhi? Utamaduni wetu bado wa kujali bado haujafa kabisa;hawezi kukosa pa kuanzia akiamua kujitangazia uhuru. Juzi tu nimeskia redioni binti alikuwa housegirl, akarubuniwa, akapata mimba, akaolewa kisha kutelekezwa na mume, akaachwa kwa mama mkwe. Mama mkwe nae kamchoka kamtimua eti anataka apangishe chumba alichokuwa anakaa yule binti na mwanae. Binti hakuja JF, alienda kwa mjumbe, akakomalia pale, haondoki mpaka mjumbe amsaidie.
 
hapana mie sitaki mali yake nitamwachia kila kitu yani namsubiri mfano anarudi kesho mie naondoka leo ili akija aone hamna mtu basi na wala sitagombania mbele kwa mbele nitamwachia tu mungu atampa adhabu yake

we si muondokaji wewe. Huishiwi vizuizi. Sasa kinachokufanya usubiri arudi mara akaribie kurudi ndo uondoke ni nini? Unataka kusema unaogopa asiseme umemuibia au? After all ushasema vitu kavifungia. kama we ni wa kuondoka paki leo ondoka, kisha mpe taarifa kuwa umeondoka ili ajue nyumbani hakuna mlinzi. Huyo ni chatu, we ni mbwa. Akija nakwambia huondoki maana akishakupa dozi ya matusi ya kukudhalilisha unakuwa mdogo kama mbegu ya haradali unaona anachosema ni kweli. Unajiona mnyonge, na utanyongwa nakwambia. Hebu kapaki uondoke, vinginevyo unyamaze milele tusome na kuchangia threads zingine. Kha!
 
Habari zenu wanajf haya habari mpya bwana kakimbia kaenda mbeya mpk leo hii hajarudi na kampigia simu mama na kumwambia kama hapo dar sirudi tena mie nitaishi hukuhuku mbeya haya sasa mnasemaje kuhusu hilo

Nilidhani hata mawasiliano mlishakata dah we bado una interest na huyo jamaa!
Pole yako!
 
Back
Top Bottom