Kunyanyasika kwangu mie unlucky hili sio jina langu natumia tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunyanyasika kwangu mie unlucky hili sio jina langu natumia tu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by unlucky, Dec 10, 2011.

 1. unlucky

  unlucky JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa naishi kwetu vizuri tu, nikaanza job kama miezi 3. Huyu bwana nilikutana nae akanipenda na mie nikampenda tukaoana. Baada ya mwaka nilipata mtoto wa kwanza ndo nikaanza kumwona makucha yake aliyoficha: alikuwa na wanawake huko nje! Kila siku ugomvi ulianza. Mara ikiwa ugomvi unatulia kama miezi 6 hivi anajibadilisha tena, nikashika tena mimba mtoto wa pili, ikaanza tena yale yale! Ndo kuzidi mpaka anaenda madisco anashinda na marafiki kutwa nikajifungua mtoto. Kufika mwaka akatulia tena akawa anaonyesha mapenzi sana ndo nikapata tena mtoto huyu wa mwisho wa tatu, wote wakike mungu kanipa. Ndo sasa hamna mapenzi kabisa.

  Katika hao watoto wote kanitesa sana, kanipiga sana, mpaka nilivyokuwa na mimba miezi minane alinipiga vibaya sana. Pia nikavumilia anabadilisha wanawake kama nguo yani nikikwambieni huyu bwana anakutana na mie hata baada ya miezi 3 anapotaka mtoto tu basi. Hata kunigusa hanigusi. Hata aseme akae aonge na mie hamna ananifungia mpaka mahitaji, chakula, kila kitu,na umalaya wote anaofanya ananionyesha.

  Huyu mwanaume alikuwa hana chochote mie nimechuma nae mpaka leo anauwezo wa kutosha na alikuwa na mke wa kwanza na watoto watano nilimpenda kufa wala sikufikiria kama ana mke leo nishajua kama alinitumia kwa ajili awe na uwezo. leo kanisaliti ananiambia mie sikutaki ondoka. kalala nje leo siku ya pili anasema sitakanyaga hapo mpaka wewe uondoke na kuna watu nje wanasema kama ameoa. huyu bwana nimevumilia mengi mpaka machozi yamekauka sasa kujiua siwezi. nilivyochoka miaka sita hajanipa chochote zaidi ya hela ya kutumia tu kila siku, ye anarudi alfajiri mpaka kula anakula nje chumbani kahama analala sitting room. Kila mwanamke anae yeye ukimwambia unapigwa kama mwizi.

  Sina pakwenda sina chochote. Mama yupo, baba sina. kaka yupo lakini ametutupa. nifanyeje? bwana ananiambia we mfanyakazi hapa na kama watoto nje pia wanapatikana. dah! leo hata sura yangu hataki kuiona, kosa kafanya yeye.

  Kamtaka mfanyakazi alikuwa anamvulia nguo anamuonyesha uchi wake na kumshika back yake huyo mfanyakazi kalia. Kaniambia mie nilivyomsuta ndo kapata sababu ya kuniacha. kataka kunipiga. dah! leo mie mbaya nimempenda sana na hata siku moja sikufikiria mwanaume mwingine na wala sitaki. yote kanifanyia nimevumilia.
   
 2. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 9,979
  Likes Received: 1,353
  Trophy Points: 280
  Pole sana unluck. Ila kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo si wewe. Huyo mumeo ni mfupa ulomshinda fisi. SI umesema alikuwa na mke kabla yako na watoto watano? Pole wakati mwingine tunahitaji kuwa extra careful na watu walokwisha oa/olewa kwani wanawweza kuwa ni watu wasio na uwezo wa kuishi na wenza au wakawa ni kweli ni victims wa wrong number.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,133
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Unlucky, nilidhani hii thread ulishaileta kitambo hapa na ukashauriwa? Hebu tupe mrudisho nyuma...
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 45,282
  Likes Received: 10,912
  Trophy Points: 280
  Dah!:shock::shock:
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,581
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Mimi sijui kama kuna ushauri zaidi ya kuanza maisha yako mapya! Mwenzio si alimuacha na watoto 5, lea wako na maisha yataenda tu!
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,138
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Yaani hii story sijaimaliza baada tu ya kufika alikuwa na mke na watoto watano akawaacha.
  Did u think utakuwa exceptional kama alidiriki kuacha mke na watoto watano?
  Uliyafikiria machozi yz bi mkubwa?
  Ulifikiria machungu ya watoto wake wale wa mke mkubwa?

  Siriazly unanshangaza, hata ukiamua kuchukua mme wa mtu hakikisha haachi nyumba kubwa na familia ya kwa huduma zote.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,045
  Likes Received: 18,558
  Trophy Points: 280
  unatuchosha kwa kweli
  tulishakushauri huko nyuma
  achana nae anza maisha upya
  mpaka 'akuue' ndo uelewe?
  nenda tamwa na tgnp wakushauri...
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,581
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Si ajabu aliendelea kuvumulia na kuhope kuwa atambadilisha kwa mapenzi...... Love changes all..... LOL
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,045
  Likes Received: 18,558
  Trophy Points: 280
  halaffu huyo jamaa ana dalili zote za mgonjwa wa akili
  tatizo wabongo tunafikiri wagonjwa wa akili wapo muhimbili na mirembe tu..
  wengine tunaishi nao na hatutaki kuwapeleka mahosipitalini
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,199
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Imagine ni rafiki yako anakusimulia wewe.......ungemshauri nini?
  Self reflexion ni bora kuliko free opinions from the forum sometimes

  alikutumia kupata uwezo!!!!!!!! sasa ni zamu yako kujitumia upate uwezo pia xperience si unayo tayari
   
 11. unlucky

  unlucky JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ndo mana leo nimerudi tena kuomba msaada wa mwisho manake nikimwambia mama anasema vumilia tu utaenda wapi utawalea vipi hao watoto watatau unanini nikimwambia mwingina ananiambia watoto waachie huyo mnyama awalee mwenyewe wewe kaanze maisha yako ukiwa peke yako utahangaika lakini na watoto utateseka watoto wake leo hataki hata kunioa sura yangu kafahamishwa na kaka yake lakini ye yupo pale pale kama mie basi jamani nifanye nini watoto niwasaliti nimwachie nisonge mbele kuliko kufanywa kama mnyama manake hata nikikimbia nao yeye anawataka watoto wake manake mara nyingi kasema we ondoka watoto waachie hapahapa mie nitawalea nikimwambia mwingine ananiambia ukichukua watoto utapata tabu mpaka dunia utaiona chungu gharaama zao utatoa wapi na utamwachia mwanya ya huyu bwana kustarehe nifanyeje hebu nisaidieni
   
 12. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 2,996
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Potelea kwa mbele kama ulishauriwa na wala hukuusikia ushauri huo.

  Jee unasubiri uletewe ukimwi halafu uje kutafuta ushauri mwengine hapa?

  Watu wengine mwe! Mungu amewapa akili hawawezi kuzitumia ipasavyo halafu wanakaa kulalama tu.
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 10,361
  Likes Received: 1,308
  Trophy Points: 280
  pole sana dada.. jaribu kuongea na wazee... nadhani huku atona haya kidogo...  "ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯

   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Du!..huku ni kubeep kifo!
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,045
  Likes Received: 18,558
  Trophy Points: 280
  kw
  enu hakuna wanaume wenye akili wa kukusaidia?

  mimi wewe ungekuwa dada yangu tungekuja 'kumpa kipondo na kumfukuza huyo mgonjwa wa akili hhapo

  tafuta namna hata wahuni wa kukodishwa umfukuze yeye hapo asije tena
  wewe uanze hata biashara ya kuuza vitumbua....
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,133
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Kuna vitu vya kungojea na ku-hope ila sio hivi! Huyu moyo wake hata upewe bure haufai hata kwa supu,kha!
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,138
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Ukiona mwanamme anaacha mke na watoto eti sababukakupenda wewe kimbia kama ukoma.
  Hiyo kitu haipo, it will nneva work.

  Kutelekeza tu mke na watoto 5 tayari mi kwangu ni kasoro ambayo haiwezi vumilika.
   
 18. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,618
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Pole sana unlucky...ni kama hii thread ulishaileta hapa ni nilikupa ushauri mzuri tuu..mpaka sasa hakuna mabadiliko yeyote? kama bado basi funguka ili tujue wapi tuanzie
   
 19. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Utazunguka kooote, lakini solution ni moja tu, toka haraka sana kwa huyo mwanaume!! Usione watu wanauza mahindi ya kuchoma ya sh 100, ni kwa sababu wamechagua kuwa huru!!
   
 20. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Sometimes ni kujinyanyasa yeye mwenyewe, wala sio kunyanyaswa kwa sababu ye ndo anakaribisha manyanyaso!! Dah........kuna watu wanajichukia jamani mweeh!!
   
Loading...