Kunyamaza pia ni dawa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunyamaza pia ni dawa...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msindima, Jun 17, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mnapoishi wawili katika kuta mmoja suala la kupishana ni jambo la kawaida kabisa. Na nikweli kwamba tatizo linapojitokeza namna hii basi linahitaji kutatuliwa kwanza kisha mengine yatafuata.

  Na mara nyingi mizozo inakuja kama matokeo ya kitu fulani, kwa hiyo ugumvi unaweza kuja kuwa sababu ya wewe kuamka kutoka katika usingizi mzito uliolala.

  Wengi wetu tunapoudhiwa hukimbilia kuchukua hatua lakini wakati mwingine kunyamaza pia ni njia sahihi ya kutatua matatizo.

  Wataalam wengi wa masuala haya wanashauri kuchukua hatua pale unapotendwa visivyo...

  Lakini kwa bahati mbaya sana kutotumia njia sahihi ya kutatua matatizo katika mahusiano kunaweza kupelekea mwisho mbaya wa mahusiano yenu na usishangae mkaja kutafutana na visu hapa mjini.

  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa ambao si rasmi umebaini kuwa si kila ugomvi unafanikiwa kufikia malengo yanayokusudiwa... na kwa sababu hiyo basi ni vyema ukajua wapi useme na wapi unyamaze.

  Mpaka hapa nadhani ushanifaham.

  Vile watu mnavyogombana unaweza kujua kule uhusiano unakoelekea kama mtadumu milele ama mtafikia mwisho wa safari na kuonana kama paka na panya.

  Kama wewe ni mmoja ya wale watu ambao huchagua kupayuka muda wote kuna wakati ni vizuri ukabadilisha stail ili umeweke pahala fulani mwenzako akae chini ajiulize unategemea nini hasa.

  Nyamaza, anategemea umuulize usimuulize na badala yake usilipize na wala usimpatilize, utamtia adabu.

  Unapoamua kuongea ni vyema ukajua njia sahihi ya kuwasilisha mambo ili kuweza kufikia muafaka.

  Na unapoongea mara moja mara mbili mara tatu sasa ni wakati wa kunyamaza. Unapoa mua kuchua hatua hii ya kunyamaza basi ni vyema ukajua kuwa kwa hatua hii pia hujakosea. Wakati huu huu tafakari hatama ya maisha yako...

  Mathalani ushamueleza dukuduku lako mara kadhaa sasa...wakati wa kufunga mdomo wako sasa umefika na kuendelea na mambo mengine muhimu katika maisha yako.
  Inapokuja katika kutatua migogoro yenu, njia hii ni nzuri wakati mwingine.

  Wengi wetu hutumia migogoro kusema na kuropoka bila kutoa nafasi, hali hii inaweza ikazoeleka na kushindwa kuwaleta mabadiliko yoyote. Unapoamua kumpuuza utashangaa mambo yanavyobadilika.

  Kujua na kujaribu kutumia njia sahihi ya kugombana kutasaidia kutatua migogoro yenu.

  Kivipi? Kama unavyojua kusema maneno yanayoudhi ni kama kumtupia kijinga cha moto mtu ambaye tayari ameshaoga mafuta ya taa.

  Kitu cha muhimu katika ugomvi ni kusema kile ambacho unakitaka kifikishe ujumbe wa uliyonayo moyoni, si kumtusi ama kumsema maneno ya kumuudhi kunakoweza kuwaleta katika muafaka. Na ukishasema sana nyamaza...

  Gombana ili ueleweke, usigombane ili kuhamisha maumivu kwa mwenzio.

  2. Tatua tatizo...
  Ukishaelewa kwa nini mnagombana, na ukajua sababu iliyopelekea kwanini mwenzako akachukua uamuzi uliokuudhi, sasa ni wakati wa kutafuta muafaka wa tatizo. Wazungu wanaita compromise.

  Wakati mwingine unaweza kukuta jambo kubwa mliligombania linakuwa dogo kutokana na uelewa wenu kwa kila moja wenu. Na njia uliyotumia kufika muafaka huo.

  Wakati mwingine unapogombana na mwenzio ukagundua kuwa ugomvi wenu haukuwa wa maana mnaweza kuchagua kukubali kutokubaliana na mkaendelea kuishi, si ushamjua bwana.
  3. Kupeana muda, pia inafaa...
  Ukishajua anajua kuwa amekuudhi, unaweza ukatumia njia hii. Mpe muda afikirie kwa makini kwa wakati wake na aamue... inatosha.
   
 2. M

  Misana Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msindima - i bet its true
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kama unatafuta suluhisho la haraka na rahisi basi kunyamaza ndio kimbilio lakini iwapo unataka suluhisho la kudumu katika mahusiano yako basi kuongea ndio njia sahihi sana. Kwa wanao ongea hufikia makubaliano ya aina fulani, tena baada kubadilishana maneno wapenzi hutmia muda kuyatafakari yale aliyoyasema mwenza wake na mazuri huyafanyia kazi hata kama hawezi kukiri hadharani. Lakini unapobakia nalo rohoni huendelea kukua na mwisho wake hutoweza tena kulibeba na hapo ndio mwisho wa uhusiano. Nashauri watu wajenge tabia ya kuongea ndani ya mahusiano yao hata kama kwa kufanya hivyo wanaweza kuhtarisha mahusiano yao, kumbuka vitu vizuri vyote vina gharama na gharama ya kuwa na uhusiano ulioshamiri ni pamoja na hii ya kubadilishana maneno kila mara.KIFUPI : kukaa kimya kutakufaa kwa muda mfupi tu lakini mwishowe mambo huaribika.
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kuna wakati mnataka kuongea but mwenzako yupo juu juu, ni wakati mzuri wa kumwacha hacra zake zipoe then mtafute muda muafaka wa kuyaongelea kiundani na kuyasuluhisha! kugngana kupo sana kinachotakiwa ni busara zaidi.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo wengi hukosea, kuna haja ya kufahamu kuwa si kwa sababu tu kuongea ni vizuri basi kila wakati ni lazima oungee. Ni vyeama hili likafanyika kwa busara kubwa tena kwa uangalifu ni maneno gani uyatumie wakati gani. Si vyema kuanzisha mazungumzo pindi wote mnapokuwa mmekasirika ni vyema pia ukaepuka kutoa maamuzi ukiwa au kauli zenye kuashiria maamuzi wakati wa hasira. Si kosa kumtuliza mwenzako akiwa amekasirika na ni busara pia kuepuka mijadala inayoleta ubishi kati yenu, hii inamaana pia muepuke mazungumzo yote yanayohusu vitu ambavyo mnamisimamo tofauti, mfano siasa iwapo wewe ni CUF na mpenzi wako ni CCM ni bora siasa zisiwe ni sehemu ya mazungumzo yenu. Nj vyema pia mkaepuka kuonesha tofauti zenu za mbele za watu, yaani kwa mfano mkiwa na wageni na mada ya siasa imeibuka basi ni vyema mkajiweka kwenye msimamo mmoja walau mbele ya za watu ilikuepuka kushusha heshima ya mpenzi na kuepuka kuwaruhusu watu wa nje wazijue tofauti zenu hivyo kuweka mwanya wa kukusanya mashabiki wa kila upande. Hii ni kwa wote wanaume na wanawake usiruhusu hali ya kuwa wewe ndio mtoa kauli, ufanunuzi na maelekezo kila wakati bali jaribu kutoa nafasi hiyo kwa mwenza wako hata kama maamuzi si sawa na ambayo ungeyatoa.Nimejifunza kutoka katika maisha jambo moja la muhimu kuhusu kutokukubaliana nalo ni iwapo utachukua muda kutaka kuelewa hoja na mwenzako basi unatoa fursa na yeye kujifunza zako kwani kwa kuogopa kushindwa watu hutaka kujua udhaifu wa wa wapinzani wao.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hii ni njia nzuri hasa unapokuwa na hasira. Ukiwa na hasira jitahidi kwa kadri uwezavyo kutokutoa kauli au kufanya maamuzi dhidi ya mwenza wako. Hili linasaidia sana. Na mara nyingi hasira zikiisha, maamuzi yanakuwa tofauti na bora zaidi.

  Nimejifunza pia hata katika malezi ya watoto - si vema kumwadhibu mtoto wakati unahasira. Hasira zikiisha mara nyingi unaweza kumpa nafasi mtoto ya kujitetea (kumsikiliza) kuliko wakati una hasira (na kiboko kipo karibu!).
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hili la watoto mkuu umenitoa tongotongo sikuwahi kulifikiria kabisa..shukrani
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...pia kunyamaza ni dalili ya kiburi, jeuri na anavyokudharau!
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  akinyamaza kabisa bila kuuliza/kutafuta ufumbuzi basi hiyo itakuwa hayo unayoyasema hapo, Mbu kuna ile mmeanza tu kuongea kitu mwenzio yupo hewani, sasa mkipanda wote hewani hakutakalika, mmoja akiwa mdogo kwa muda fulani kumpa mwenzie nafac apunguze hacra itasaidia zaidi.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Ni aje? pale njemba inapotoa kauli, "niachie kelele zako, nimechoka nataka kupumzika." na unajua akishasema hivyo ndiyo kamaliza hataigusa tena hiyo issue iliyozaa zogo ndani ya nyumba.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu naona kuwa mwanaume ukiwa unanyamaza nyamaza hovyo matokeo yake mamaa hakawii kukushika akili...

  Be aware!
   
Loading...