Kununua na kuajiri: Rais ana turufu?

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima kwenu,
Kwa kawaida mapato na matumizi ya nchi hujadiliwa na kupitishwa na wabunge. Hii ni baada ya serikali kuleta makadirio.Huu ni utaratibu wa nchi zote zenye bunge.

Kwa Tanzania mambo ni tofauti.Tumesikia ndege mbili zikinunuliwa kwa amri ya rais kwa mamia ya mabilioni.Rais ametangaza kuhamia Dodoma.Tayari kuna watumishi wametangulia.

Hili la Dodoma na ya ndege havikupitishwa na bunge.Hakukuwa na bajeti.Wabunge hawakupitisha kwa kuwa serikali haikuleta makadirio.

Waziri wa Afya ametangaza kuajiri madaktari 258 na wataalamu wengine 11.Haya ni mambo mazuri lakini yanahitaji bajeti.Nani amepitisha? Rais ana turufu ya kuamua mapato ya matumizi ya serikali bila idhini ya wabunge?
Nawasilisha.
 
Awamu hii kila kitu kinafanywa na RAIS wengine wako tu kama picha ya JKN ukutani
 
Back
Top Bottom