Kununua laptop msimu huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kununua laptop msimu huu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 4, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jinsi ya kununua Laptop Au computer ni maswali ambayo huwa yanaulizwa sana sehemu mbalimbali haswa kutokana na vifaa hivi kutumika sana kwa maisha ya kila siku na kwa sasa hivi vifaa vimekuwa ni sehemu muhimu sana ya watu wote .

  Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla ya kununua Laptop na sio kuangalia tu katika picha mfano kwenye Tovuti fulani au tangazo kwenye gazeti na vipeperushi au kuangalia sample kwenye maduka mbalimbali yanayouza bidhaa hizi .

  Kwa kuangalia vitu kama hivyo unaweza kweli kununua lakini ukaja kukuta mfano keyboard yake sio nzuri kwa ajili ya utendaji wa kazi hata kama ina spidi nzuri , programu nzuri na ambazo zimesajiliwa na vikorombwezo vingine vingi sana .

  Ni vizuri ununue laptop ambayo unaweza kuitumia kwenye mazingira tofauti mfano kwenye mwanga mkali , sehemu ya joto kali mfano tanzania kuna sehemu zenye joto sana , ukiacha hilo kuna watu wanaweka laptop zao kwenye magari ambayo hufungwa vioo ndani kuna joto inabidi uangalie mazingira kama haya kama laptop hiyo inaweza kuhimili .

  Unatakiwa utambue kwamba kila maelezo yana nafasi kubwa sana katika ufanyaji kazi wa laptop yako na ni muhimu sana kuyasoma ukaelewa na kuona kama unaponunua kifaa hicho kinaweza kuendana na shuguli zako za kila siku na mazingira ambapo utahifadhi laptop hiyo .

  Halafu kuna swala la kuongeza vitu vingine kwenye laptop yako kwahiyo unapoangalia na kununua angalia kama kuna sehemu za kukuwezesha kuongezea vifaa vingine pindi unapotaka kutumia vifaa hivyo mfano USB , Vifaa vya Sauti , Moderm na vingine vingi tu .

  Usisahau kwamba mwaisho wa mwaka ni msimu za manunuzi makubwa ya vitu hivi , kipindi hichi cha sikukuu ya xmass na mwaka mpya ni kipindi ambacho maduka mengi sana huwa yanauza vitu na vifaa kwa bei nzuri kidogo na pia watu wengi huwa wananunua bidhaa hizo kwa ajili ya shuguli zao unapoanza mwaka mwingine .

  Kwenye upande wa ununuzi wa vitu kama computer haswa laptop msimu huu mnunuzi anatakiwa awe makini zaidi , pamoja na kuangalia vitu kama ukubwa wa CPU , RAM , HDD , na vingine vingi anatakiwa akumbuke kwamba sasa nchi ipo kwenye kipindi cha Mgau wa umeme .

  Sehemu nyingi kwenye maofisi , makazi na mashuleni watu wanatumia umeme wa generator , umeme huu sio mzuri sana kwa afya na maisha ya jumla ya vitu kama laptop , simu za mkono , digital camera na vifaa vingine vya electroniki .

  Kwa upande wa laptop , umeme wa generator unachangia sana katika kupunguza maisha ya Battery pindi unapotumia laptop hiyo na umeme wa generator kama sio kuiua kabisa battery pamoja na Power Adaptor inayotumia kupeleka umeme na kucharge battery ya laptop husika .

  Unaponunua vitu kama Laptop , wanakupa warranty lakini ambayo haihusiani na umeme , yaani kama adaptor yako imekufa kutokana na umeme hiyo warranty haifanyi kazi tena , au kama ulitumia kwenye generator ikauwa battery pia kwenye duka hauwezi kurejeshewa kifaa kipya .

  Pamoja na yote haya kuna vifaa vya kuweza kuweka umeme sawa kwa majumbani na sehemu zingine ambapo vitu kama laptop zinatumika ni kazi tu ya mtumiaji kuamua kununua kifaa hicho kwa ajili ya office yake au nyumbani kwake , lakini ukiamua kutumia kavu kavu utapata hasara mara kwa mara .
  Na mwisho ningependa kushauri haya maduka yanayouza bidhaa kama laptop , digital kamera na zingine wawe wanawaambia wateja wao ukweli kuhusu tatizo la umeme , isije kuonekana kwamba wao ndio wanauza vifaa ambavo havidumu au havina hadhi wakati wateja wao ndio hawajaeleweshwa au kujulishwa vya kutosha .

  Kabla sijamaliza , pengine nikupe aina ya laptop ambazo ziko maeneo ya mjini kwa sasa unaweza kupata maelezo zaidi unapotembelea maduka hayo siwezi sema ni duka lipi haswa kwa sababu karibu maduka yote makubwa ya vifaa hivi hapa Tanzania yanamilikiwa na watu wale wale kwa majina tofauti kwahiyo vifaa vinatokea sehemu moja na kusambazwa sehemu hizo zote .

  Bila kusahau unaweza kununua kwa njia ya mtandao pia katika tovuti za kampuni hizo unaponunua kwa wengine kama Ebay kuna matatizo yake kwa mfano unaweza kupewa mali ambayo sio ile iliyoonyeshwa ingawa hii inatokea mara chache sana lakini mbaya zaidi ni kuwekewa program ambazo ni bandia ( pirated ) hili ndio tatizo kubwa ambalo watu wengi wanakutana nalo wanaponunua kwa kweli hili limekuwa tatizo kubwa sana .

  Na kumbuka kununua Laptop ambayo inaendana na kazi zako , kama wewe unafanya kazi mfano za graphics lazima uwe na laptop yenye ukubwa kidogo ila kama wewe ni mwanafunzi tu ambaye unatumia microsoft word , excell na programu zingine ndogo huhitaji inayofanana na mtu wa graphics huu ni ushauri wangu lakini unaweza kuamua wewe mwenyewe

  Kwa sasa majina ya Laptop Ni ACER , APPLE ,TOSHIBA ,SONY , DELL , HP , HPCOMPAQ , COMPAQ , IBM ,LENOVO , SAMSUNG ,GATEWAY , PANASONIC , FUJITSU ,NEC , ELECTROVAYA , hizi zote zina model mbalimbali kwahiyo angalia model ambayo ni ya kisasa inayokufaa kwa shuguli zako .

  Yona f maro
  Tembelea www.naombakazi.com kwa nafasi za kazi
  Tembelea www.askmaro.blogspot.com kwa maelezo mbalimbali ya programu na makala .
  Tembelea www.wanabidii.net kwa mijadala mbalimbali
   
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu Shy. IBM imeshanunuliwa na Wachina na sasa inaitwa LENOVO. IBM waliuza kitengo cha computer chote na sasa wamebaki kwenye mashine nzito na kubwa yaani big boys.

  Nafikiri kwenye computer umesahau Asus, MSI, LG na BENQ. Hawa Asus na BENQ wako very agresive maana wanakuja kwa speed kali sana kama kawaida ya Taiwan. LG ni Mkorea goigoi sana. Pana wakati nilifikiri atamzidi Samsung ila naona Samsung kawafunika wote hadi Mzee Sony. Sony kama siyo kifo cha Michael Jackson, angelikuwa na hali mbaya saaana.
   
 3. Kivuko

  Kivuko Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lenovo Didn't purchase the whole IBM computer UNIT!!that's a bit wrong,all they did was buying Rights to market and use the THINKPAD "personal" computer brand for 5 years,from 2005 to 2010.

  IBM still owns the "THINKPAD" brand,and still manufacture computers and servers.
   
Loading...