Kununua gari au kujenga nyumba

Nyumba kwanza gari baadaye. Huwezi kamwe kulinganisha Gari na Nyumba, Nyumba ni zaidi ya Mali. Hiyo ndio hekima na sio ufahari. Maisha ni kupanga na sio kuiga.

Una mke na watoto, anza kuwaza kuwa na Nyumba kwanza kwani ipo siku uchumi wako unaweza kuyumba au Ukafariki dunia, sijui Mkeo na watoto wako watakuwa wapi?

Mawazo ya watu waoga wa maisha hayo, kama mjanja ukiwa na gari unaeza jenga nyumba kwa haraka zaid ya kudunduliza kwa kuwa ni muonga
 
:peep:Jenga mkubwa kwanza familia yako tayari ni kubwa sana pia kuna Baba mwenye nyumba daima sio gari:car:
 
Mawazo ya watu waoga wa maisha hayo, kama mjanja ukiwa na gari unaeza jenga nyumba kwa haraka zaid ya kudunduliza kwa kuwa ni muonga

Jerrymsigwa Hakuna uhusiano wowote kati ya woga wa maisha na Uamuzi wa kujenga Nyumba.
Ila uamuzi wa kujenga Nyumba ni wa kijasiri zaidi tena unahitaji hatua, subira na tafakari mbalimbali.
Kwa mfano mahali utakapo amua kujenga nyumba yako ujue huenda ni mahali utakapoishi maisha yako yote ikiwezekana hata ukifa unaweza kuzikwa hapo hapo!!
Sasa piga picha Wewe ni mzaliwa wa Shinyanga vijijini na umeamua kuja kujenga Dar. Je huo ni woga wa maisha au ni ujasiri wa maisha?

Suala la kufanikiwa kimaisha na kudumu katika mafanikio hayo sio suala la ujanja ujanja bali ni juhudi na mipango tu.

Sasa embu tupe uhusiano wa kumiliki gari unaopelekea kukupa ujanja wa kuja kujenga nyumba, na mimi nitakupa Uhusiano wa kujenga kwanza Nyumba na namna inaweza pelekea kukupa Mipango na Juhudi za kuja kumiliki Gari siku za usoni.
 
Last edited by a moderator:
Waoga wa maisha huanza na nyumba ila kwa watu jasiri gari kwanza mengine baadae. Ukiwa na gari kwanza waweza kodisha, networking, unakopesheka, kama ni mtu wa skirts basi gari ni sumaku.

Gari kwanza mengine baadae,acha woga kijana

Hahahah uh yaan umemaliza kabisaa garii kwanza gari litaleta nyumba,likigongwa bahat mbaya jaman
 
Nunua gari na ujiandae pia kupandishwa kodi hapo unapoishi na matokeoyake utahama. Na kupata nyumba yenye parking hapo mjini balaaa. Ni upuuzi kuhitaji ushauri hata kwa mambo rahisi kama haya.
 
Ushauri Muhimu kabisa waanze na Nyumba kwa sababu:
1/Nyumba ni mali isiyohamishika hivyo ni dhamana muhimu mahali popote pale duniani iwe Mahakamani, Benki, Biashara, Maishani, Kazini nk.

2/Thamani ya Nyumba inakwenda inaongezeka kila siku(Hata siku wakitaka kuiuza wataiuza kwa thamani kubwa zaidi).

3/Watakuwa wameondoa gharama za kupanga na usumbufu wake(Watakuwa huru sana)

4/Nyumba ni Akiba ya kudumu maishani(Wataishi wao na vizazi vyao)

5/Nyumba ni kipimo cha Heshima, Hekima, Busara na Upeo kijamii, kifamilia, kimila, kiserikali nk.

6/Nyumba ni Mtaji wa Maisha(Hawatatoa tena pesa zao kila siku au kila Mwezi kulipia gharama za kuishi kwenye hiyo nyumba zaidi wanaweza kupata kipato zaidi kama sehemu ya hiyo nyumba watapangisha)

7/Nyumba inaweza kuwaletea vitu vingine vingi kama Gari kama watafanya mahesabu vizuri(Kwa mfano wanaweza kuitumia kama dhamana katika taasisi za kipesa kukopa pesa za kununulia gari nk.)

NOTE;
Kwanini wasianze na Gari:
A/Gari inahitaji gharama kubwa sana kulihudumia(Kwa mfano Insurance, Kodi ya Mapato, Mafuta ya kila siku, Service ya kila mara, Parking ya kila siku, Trafiki, Vipuri nk)

B/Gari itakuzidishia gharama zaidi za maisha pasipo msingi.(Mfumo wako wa maisha unaweza ukabadilika ili kukidhi tu fahari ya kumiliki gari. eg.Kula, kuvaa, Makazi, matembezi, Marafiki, Ndugu, Jamaa nk.) Hili jambo nimeliona kwa watu wengi sana mijini. Kifupi Gari halipatani sana na mbana matumizi!!!

C/Thamani ya Gari mara nyingi inakwenda ikipungua tokea ile siku unalimiki.

D/Gari ni chombo kinachochakaa kwa upesi sana kadri siku zinavyokwenda au unavyolitumia(Mara nyingi magari mengi yanakuwa yameanza kuchakaa vibaya baada ya miaka mitatu tu!!)

E/Gari lina tabia ya kukugeuza kuwa Mtumwa wake(Kwa mfano Wakati wote litakuhitaji kutoa pesa zako mfukoni ili uweze kulitumia). Kifupi Gharama za Gari ziko juu zaidi wakati wa kulitumia kuliko hata wakati wa kulinunua!!

Ningependa kushare na watu wengine uzoefu wangu..mimi mwenyewe kwangu mimi nilianza na gari...Lakini nashukuru Mungu aliniongoza kununua aina y Gari ambayo ..muda ulipofika nataka kuiuza haikunipa shida...kwakifupi ni yale magari ambayo hufungi nayo ndoa ya Kanisani!!!...Hii gari kwangu ndio ilinisaidia kupata kiwanja kile roho yangu ilikuwa inataka yaaani ilikuwa msaada mkubwa sana kwangu...nilizunguka nayo sana kutafuta pale roho yangu inataka...naweza kusema kama sio hii gari isingekuwa rahisi mimi kufika kule kote nilipotakiwa kufika wakati natafuta kiwanja...kumbuka huku kote nilikuwa nawabeba madalali au marafiki wananipeleka haya maaeneo...na nilikaa na hii gari mpaka nakuja kuanza ujenzi..ikanisaidia pia kuanza kupeleka vitu site...na nilipotaka kuiuza nikaiuza kwa faida...kwasababu ni aina ya gari ambayo demand yake ipo juu hata kama unataka kufanya biashara kwa kutumia hiyo gari....lakini wakati nainunua watu walisema pia..aaahh anaishi nyumba ya kupanga ananunua gari?!!! Maisha ni kupanga
 
Waanze na nyumba lakini kwa kipato hiko kujenga dsm majanga..nawashauri wajipange au watafute other sources of funds amasivyo watasota sana hata kujenga msingi...!Sio lazima gari washauri wanunue bajaji..
 
Ningependa kushare na watu wengine uzoefu wangu..mimi mwenyewe kwangu mimi nilianza na gari...Lakini nashukuru Mungu aliniongoza kununua aina y Gari ambayo ..muda ulipofika nataka kuiuza haikunipa shida...kwakifupi ni yale magari ambayo hufungi nayo ndoa ya Kanisani!!!...Hii gari kwangu ndio ilinisaidia kupata kiwanja kile roho yangu ilikuwa inataka yaaani ilikuwa msaada mkubwa sana kwangu...nilizunguka nayo sana kutafuta pale roho yangu inataka...naweza kusema kama sio hii gari isingekuwa rahisi mimi kufika kule kote nilipotakiwa kufika wakati natafuta kiwanja...kumbuka huku kote nilikuwa nawabeba madalali au marafiki wananipeleka haya maaeneo...na nilikaa na hii gari mpaka nakuja kuanza ujenzi..ikanisaidia pia kuanza kupeleka vitu site...na nilipotaka kuiuza nikaiuza kwa faida...kwasababu ni aina ya gari ambayo demand yake ipo juu hata kama unataka kufanya biashara kwa kutumia hiyo gari....lakini wakati nainunua watu walisema pia..aaahh anaishi nyumba ya kupanga ananunua gari?!!! Maisha ni kupanga

FuturePresident wewe unasema gari lilikusaidia kujenga nyumba kwa namna ya:
1/Kukubeba wewe mwenyewe wakati unazunguka kutafuta Kiwanja.

2/Kuwabeba Ndugu, marafiki na madalali wakati wa kutafuta kiwanja.

3/Kubebea vifaa vya ujenzi kwenda kujengea nyumba yako.
Je Unahisi hizo ni sababu za msingi sana kumshawishi mleta mada kwamba Gari kwanza Nyumba baadaye?

Jambo moja very interesting unaweza ukatuambia ni kwa nini uliamua kuliuza hilo gari baada ya muda fulani wakati lilikuwa ni muhimu sana katika maisha?
Lakini pia unasema uliliuza kwa faida hilo gari, is that garantee kuwa kama naye akija kutaka kuliuza gari lake anaweza kupata faida au ni pata potea tu?
 
Last edited by a moderator:
Acha kumdanganya mwenzio na magari 3rd hand. Gharama zake ni kubwa maana nyingi zimeshachoka. Na hio nyumba ya chini ya mil 30 ndio ikoje?? anyways, nyumba hata ikichukua miaka 5 mwisho wa siku utahamia kwako na kuepuka gharama za kodi na kero nyingine

Uwe unasoma vizuri kabla ya kukurupuka na kujibu. Mi nimemuuliza mtoa mada na nikatoa mawazo yangu hapa cjatoa ushauri sababu cjui ana kitu gani mpaka sasa.
 
iko hv afadhali gari kwanza kwakuwa ukiwa na usd 5000 tayari una mkoko mzuri tu barabarani na utasolve ishu kibao na heshima juu, lakini nyumba mmh utapata wapi ya bei hiyo?
vilevile ni rahisi kupanga nyumba kuliko kukodi gari kwa mwezi, ukiwa na laki tatu unapata nyumba nzuri tu ya kupanga kwa mwezi lakini hiyo pesa huwezi kukodi gari kwa mwezi
ANGALIZO:Ukitangulia kununua gari hakikisha una bajeti ya kulihudumia na vile vile ni muhimu mno kulikatia bima kubwa comprehensive inasaidia sana
 
anatakiwa alijaze mafuta kila anapotoka nalo kumbuka, halafu kuna hela ya parking kama anakaa nyumba isiyo na mahali pa kupaki gari hapo oandoa mambo ya maintanace maana sio kila mara.
Nyumba ndo haina maintenance? Nimegundua watu wanashindwa kutofautisha kati ya house na home. Sasa mtu kajenga vyumba viwili (chumba na sebule) na choo cha nje nae anajiita ana house??? Hapo ni home tu
 
Ushauri Muhimu kabisa waanze na Nyumba kwa sababu:
1/Nyumba ni mali isiyohamishika hivyo ni dhamana muhimu mahali popote pale duniani iwe Mahakamani, Benki, Biashara, Maishani, Kazini nk.

2/Thamani ya Nyumba inakwenda inaongezeka kila siku(Hata siku wakitaka kuiuza wataiuza kwa thamani kubwa zaidi).

3/Watakuwa wameondoa gharama za kupanga na usumbufu wake(Watakuwa huru sana)

4/Nyumba ni Akiba ya kudumu maishani(Wataishi wao na vizazi vyao)

5/Nyumba ni kipimo cha Heshima, Hekima, Busara na Upeo kijamii, kifamilia, kimila, kiserikali nk.

6/Nyumba ni Mtaji wa Maisha(Hawatatoa tena pesa zao kila siku au kila Mwezi kulipia gharama za kuishi kwenye hiyo nyumba zaidi wanaweza kupata kipato zaidi kama sehemu ya hiyo nyumba watapangisha)

7/Nyumba inaweza kuwaletea vitu vingine vingi kama Gari kama watafanya mahesabu vizuri(Kwa mfano wanaweza kuitumia kama dhamana katika taasisi za kipesa kukopa pesa za kununulia gari nk.)

NOTE;
Kwanini wasianze na Gari:
A/Gari inahitaji gharama kubwa sana kulihudumia(Kwa mfano Insurance, Kodi ya Mapato, Mafuta ya kila siku, Service ya kila mara, Parking ya kila siku, Trafiki, Vipuri nk)

B/Gari itakuzidishia gharama zaidi za maisha pasipo msingi.(Mfumo wako wa maisha unaweza ukabadilika ili kukidhi tu fahari ya kumiliki gari. eg.Kula, kuvaa, Makazi, matembezi, Marafiki, Ndugu, Jamaa nk.) Hili jambo nimeliona kwa watu wengi sana mijini. Kifupi Gari halipatani sana na mbana matumizi!!!

C/Thamani ya Gari mara nyingi inakwenda ikipungua tokea ile siku unalimiki.

D/Gari ni chombo kinachochakaa kwa upesi sana kadri siku zinavyokwenda au unavyolitumia(Mara nyingi magari mengi yanakuwa yameanza kuchakaa vibaya baada ya miaka mitatu tu!!)

E/Gari lina tabia ya kukugeuza kuwa Mtumwa wake(Kwa mfano Wakati wote litakuhitaji kutoa pesa zako mfukoni ili uweze kulitumia). Kifupi Gharama za Gari ziko juu zaidi wakati wa kulitumia kuliko hata wakati wa kulinunua!!
"if they are planning for the future basi wajenge nyumba lakini kama wana plan only for tomorrow then wanunue gali tu"
 
Maisha yako hivi,
Kwa waliiooa na kujaaliwa kupata watoto,jambo la kwanza katika maisha jitahidi kuiandalia familia yako makazi,yaani nao wawe na kwao kama wewe ulivyo na kwenu.

Na inatakiwa ujitahidi kabla hawajakuwa ili uweze kuwamudu vizuri pindi watakapoanza shule,namaanisha kuwasomesha bila kubahatisha,
vilevile kuna leo na kesho lazima ufikilie je siku kibarua kikiota nyasi au ukitoweka utawaachaje hao wanao na mkeo?

Gari ni tofauti na nyumba, Gari ni mali inayohamishika mda wowote inaweza ikawa historia,Nyumba ni mali isiyohamishika mda wowote inaongezeka thamani na kukuweka mjini,
Kama hiyo gari wanataka kunua kwa ajili ya kujiongezea kipato sio mbaya lakini kama ni kufuata mkumbo waambie waachane nalo kabisa,
Mjini mipango la sivyo utaaibika.
 
Back
Top Bottom