kwenye kila bidhaa kuna sehem ya kumtumia sms supplier au muuzaji na ukimtumia wengi ndani ya mda mfupi wanajibu... tena wanakubembeleza kabisa...
 
wengi wa alibaba ni waaminifu kwa expirience yangu cjaskia mtu ametapeliwa ishu ni kua direct to the point na ku order kitu unachokijua vizuri na umuandikie details zote kiusahihi Short and Clear and Exactly kitu unachokitaka Full desceiption all details model etc... usijaribu ku assum kudhani kua wanfikiri kama unavofikiri au unavojua Speak business straight language... ukikosea apo unaeza tumiwa mzigo huo huo ulio order lakini utapumzika utakavokua kituko.
 
wengi wa alibaba ni waaminifu kwa expirience yangu cjaskia mtu ametapeliwa ishu ni kua direct to the point na ku order kitu unachokijua vizuri na umuandikie details zote kiusahihi Short and Clear and Exactly kitu unachokitaka Full desceiption all details model etc... usijaribu ku assum kudhani kua wanfikiri kama unavofikiri au unavojua Speak business straight language... ukikosea apo unaeza tumiwa mzigo huo huo ulio order lakini utapumzika utakavokua kituko.
Poapoa
 
Shipping anae kuuzia atakupa suggestion... Mzigo nliohitaji ni box 1 kubwa tu... so nlitumia DHL... watakuletea mpaka ulipo na ukifika watakupigia sim. Kodi pia ipo waliniandikia Laki 5 nkaenda kufatlia ikapungua mpaka 250. so we chukua risk ujifunze anza na mzigo mdogo...
 
Kwa wanunuzi wa bidhaa mtandaoni hapa nazungumzia Aliexpress na Alibaba huu ni uzi maalum wa kujifunza kuagiza bidhaa kupitia mtandao huu hususan Aliexpress. Mjuavyo Aliexpress ni mtoto wa Alibaba

Alibaba imebase kwenye kuuza bidhaa za jumla huku aliexpress wakibase kuuza bidhaa za rejareja na mojamoja kwa mteja

Ndio mtandao unaokuwa kwa kasi na umekuwa na wanunuzi wengi kupita hata Amazon na Ebay

Kupitia uzi huu nimeanzisha hili tuweze kupeana elimu na maarifa kuhusu manunuzi kupitia hizi site kama walivyofanya wenzetu walivyoanzisha uzi wao tukajifunza kuhusu Ebay

Natumai wataalam na wenye uzoefu mpo humu na mtajibu maswali ya wengi wetu tunaopenda kufahamu zaidi na kujifunza kuhusu aliexpres

Na maswali mengi yatabase kwenye kila kitu

Mfano mpaka bidhaa imfikie muhusika, gharama, system ya malipo, muda, na uimara wa bidhaa n.k

Karibuni sana wadau
 
Wakuu mkumbuke bidhaa kutoka aliexpress sasa hivi zinatozwa kodi na TRA mzigo ukifika lazma uende tra ukalipe kodi
 
Mimi nimenunua vifaa vya photo studio ali express nililipa kwa paypal.. na mzigo ulitumwa dar kwa dhl.. ndio umefika nahangaikia kodi
 
EBAY NIKISET COUNTRY INAANDIKA UNITED STATE NIKIJARIBU KUBADILISHA INAGOMA KBS HADI INAJILOG OUT HAPO NDO NAWACHUKIA<br />BIDHAA WANAANDIKA WANASHIP WORLD WIDE UKIAGIZA UKIBONYEZA KWENYE ship TO INAANDIKA USA UKIBADILISHA UANDIKE TANZANIA INAKATAA <br />KWANI EBAY HAINA OPTION YA KUSHIP BIDHAA TZ?
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?


Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao:
watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop US Stores and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT

WAONGEZE VIABOX, They are the best shipping forwading service they can stay on the top of all those mentioned above.
nimewatumia once nna experience nao. nimeandika short review kwenye thread hii
Check comparison hapo chini.
viabox.jpg
 
Habari...
Kwa kifupi kuna dada mfilipino amekuwa akipost vitu vya aina tofaut tofaut fb mfano nguo,simu,viatu etc..siku moja nikamfuata inbox nikaulizia bei kwa baadhi ya nguo nilizozipenda akanitajia kwa gharama ya kwao nikabadili kwa Tshs,kiukweli haikuwa gharama kubwa sana na hapo nikavutiwa na kufanya biashara hiyo..

MSAADA...kunataratibu gani zinatakiwa kufuatwa ili nipate mzigo ukiwa salama??yeye sera yake atumiwe hela ndo anatuma mzigo..
Hapa nipo njiapanda nashindwa kujua nafanyaje juu ya hili, tafadhali wazoefu wa mambo haya mnisaidie.,.

Asante.
 
Habari...
Kwa kifupi kuna dada mfilipino amekuwa akipost vitu vya aina tofaut tofaut fb mfano nguo,simu,viatu etc..siku moja nikamfuata inbox nikaulizia bei kwa baadhi ya nguo nilizozipenda akanitajia kwa gharama ya kwao nikabadili kwa Tshs,kiukweli haikuwa gharama kubwa sana na hapo nikavutiwa na kufanya biashara hiyo

MSAADA...kunataratibu gani zinatakiwa kufuatwa ili nipate mzigo ukiwa salama??yeye sera yake atumiwe hela ndo anatuma mzigo..
Hapa nipo njiapanda nashindwa kujua nafanyaje juu ya hili, tafadhali wazoefu wa mambo haya mnisaidie.,.

Asante.

Ila angalia Facebook matapeli wengi sana mkuu usije lizwa
Maana unaweza tuma pesa na mzigo usiupate
 
Back
Top Bottom