Kunukuu maandiko ya kidini katika matukio na harakati za kisiasa ni upeo hafifu wa fikra

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
36,570
44,227
Kuna watu wengi mtandaoni hasa Wakristo na kutoka chama cha CHADEMA hupendelea sana kunukuu maandiko ya kidini kwa maana ya Biblia katika kuwasilisha hoja na hisia zao kuhusu matukio mbalimbali yanayohusiana na harakati za kisiasa zinazoendelea nchini kila siku.

Kuna huwa kipi kinaongezeka katika harakati za kisiasa kwa kutumia maandiko ya kidini yanayowalenga watawala na watu wenye dola.Watawala wengine wanaoandikiwa na kulengwa na hizo nukuu iwe ni kutoka kwenye Biblia au Quran hawaamini hata hivyo vitabu au kimojawapo na wanavichukulia ni vitabu kama vilivyo vingine vyovyote vilivyopo duniani.

Ifike hatua upeo wa kisiasa uwe juu kufahamu dini ina mchango mdogo sana na finyu katika kubadili kwa njia chanya hali za kisiasa katika nchi yoyote, zaidi sana huchangia utengano badala ya utangamano. Ushahidi wa kihistoria unathibitisha hilo.
 
Upo sahihi kaka
Hoja ya dini ijibiwe kwa dini na hoja ya siasa kwa siasa pia
 
Kwa mwenye akili na fikra chanya atajengeka na kauli zinazomrudisha ktk hali ya ubinadamu.. Siasa za Tanzania ni ushetani ambao uliobobea na wanasiasa wanauchukia ukweli kwa maana utawafelisha kutokana tamaa na matendo yao wengi sio rafiki kwa wananchi wengi na taifa lao.
 
Kuna watu wengi mtandaoni hasa Wakristo na kutoka chama cha CHADEMA hupendelea sana kunukuu maandiko ya kidini kwa maana ya Biblia katika kuwasilisha hoja na hisia zao kuhusu matukio mbalimbali yanayohusiana na harakati za kisiasa zinazoendelea nchini kila siku.

Kuna huwa kipi kinaongezeka katika harakati za kisiasa kwa kutumia maandiko ya kidini yanayowalenga watawala na watu wenye dola.Watawala wengine wanaoandikiwa na kulengwa na hizo nukuu iwe ni kutoka kwenye Biblia au Quran hawaamini hata hivyo vitabu au kimojawapo na wanavichukulia ni vitabu kama vilivyo vingine vyovyote vilivyopo duniani.

Ifike hatua upeo wa kisiasa uwe juu kufahamu dini ina mchango mdogo sana na finyu katika kubadili kwa njia chanya hali za kisiasa katika nchi yoyote, zaidi sana huchangia utengano badala ya utangamano. Ushahidi wa kihistoria unathibitisha hilo.
Historia inaonesha dini imetumika sana kulinda maslahi binafsi. Kabla hata ya Bwana Yesu, mfalme wa kwanza wa Israeli , Sauli, alidai kwamba nyara alizobeba vitani kinyume na maagizo ya Mungu, ilikuwa ni kwa ajili ya sadaka kwa Mungu. Kesi ya Yesu mbele ya Pilato ni jambo hilo hilo. Fast forward, Magufuli alitumia sana Biblia na viongozi wa dini, hata kujiona ana haki ya kuhutubia taifa toka madhabahuni. Wanaharakati wanayo haki kabisa kutumia dini, kwa malengo mema
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom