Kunjua makucha kwa kampuni za simu-Zungu

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
Serikali imetakiwa kutoa adhabu kwa kampuni za simu zinazotoa huduma zisizo na ubora ili zisifanye mambo kienyeji.
Akiuliza swali bungeni jana , Mussa Zungu (Ilala) alisema katika baadhi ya nchi Kampuni za simu zinasaini mkataba maalumu ambao utawataka kutoa huduma zenye ubora kwa wateja.
Alisema mkataba huo unalazimu kampuni kulipa faini iwapo wataenda kinyume na mkataba kwa kushindwa kutoa huduma bora.
“Kwa Tanzania, inafanya nini kwa Kampuni za Simu zinazoshindwa kutoa huduma bora kwa wateja wake,? alihoji Zungu.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alisema kwa Tanzania ipo Sheria ya Epoca ambayo inazitaka kampuni hizo kutoa huduma bora kwa wateja. Alisema sheria hiyo inatoa adhabu ya Sh5 milioni au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja kwa kampuni kushindwa kutoa huduma bora.
Awali akijibu swali la Mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu (CCM), Profesa Mbarawa alisema usiku wa Novemba 13 mwaka jana hadi asubuhi ni kweli kwamba Kampuni ya Simu ya Tigo ilipata tatizo la kutokuwapo kwa mawasiliano.
“Tatizo hilo lilisababishwa na hitilafu ya umeme ambao nguvu yake ilikuwa kubwa na kuunguza mfumo wa umeme katika kituo kikubwa cha kampuni hiyo kilichopo eneo la Sabasaba, Dar es Salaam
“Tatizo hilo pia lilisababisha kuungua na kuharibika kwa betri 4 ambazo zinatunza umeme wa kituo,” alisema
Alisema katika kuhakikisha matatizo kama hayo yanapatiwa ufumbuzi, Mamlaka ya Mawasiliano imeanza utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa kampuni zote za mawasiliano kwa lengo la kulinda maslahi ya watumiaji.

CHANZO: MWANANCHI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom