Kunguru na Mwewe wanashambulia sana vifaranga wangu

Kitabu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
302
26
Wakuu kunguru na mwewe wanashambulia sana vifaranga wangu wa kienyeji.

Je kuna mbinu yeyote ya kudhibiti?

Msaada tafadhali.
 
Wawekee sumu ya panya kwenye maanadazi halafu ukifanikiwa kumuua mmoja tu, ufunge mzoga wake na uuning'inize juu jirani na eneo unalofugia. Wakiuona tu mzoga wa mwenzao, hawatakuja wasogelee tena eneo lako.

Au kama una mikanda ya video/kanda (tape), au kamba za rangi rangi, zungushia eneo lako! Kwa akili yao watajua ni mtego na hivyo wataogopa kukaribia. Hao wadudu wanaongoza kwa uwoga duniani.
 
Kwanza niseme! Kuna tetesi Hawa kunguru weusi waliletwa hapa inchini (MIJINI) kwa ajili ya kampeni ya usafi (Enzi za W/Mkuu Edo-lowassa)!

Kama ni kweli, Wataalam walioidhinisha lifanyike Hilo Basi walikurupuka!

Ebu waza kunguru mweusi anapora Hadi tonge la nyama mkononi, Ebu waza kunguru wanachukua nyama hata ikiwa jikoni wanafunua na kudokoa;

Yote tisa Hawa Kunguru weusi sasa wamegeuka kero kubwa Sana kwa sisi Wafugaji wa Kuku wa kienyeji!

MFANO Kuku Mtetea,Unamtunza vizuri anaatamia mayai 22 (Unatamani uyale mayai lakini unawaza soko la kuku), anatotoa vifaranga 18 , Hadi vifaranga hao wakue kunguru anakuwa kashapunguza vifaranga 17 kwa kuwala!

Mimi Kama mfugaji nabakiwa na kimoja tu, hapo sijazungumzia gharama ya chanjo ya Mdondo n.k!

Na ili Kuku awe wa kienyeji lazima akale chakula cha kuparua, ukimfungia kuku wa kienyeji hakui haraka na Ni rahisi Sana kufa kwa magonjwa!

Je; Nitumie mbinu/dawa gani ili vifaranga wasiliwe na Kunguru?

Toa maoni kwa faida yako pia maana msipotushauri namna ya kutokomeza Hawa Kunguru, Sisi Wafugaji tutapandisha bei, Msishangae siku KUKU wa kienyeji tukaja UZA LAKI MOJA!

Naombeni maoni yenu wadau, Vinginevyo mtaendelea kula mabloiler ya kuku wa Kizungu huko mtaani mpate kansa, Hususani kwa wapenda virigisi ambako sumu zote za kuku bloiler hukimbilia!

Tushauriane hapa kuondoa Kunguru mweusi ili bei ya KUKU wa kienyeji ishuke tukuuzie wewe mlaji hata kwa 5000/= ule firigisi,utumbo na kuvunja mifupa!

KARIBUNI KWA MAONI JAMANI
 
Mkuu kuna njia nimeona huku mtaani pengine ikasaidia tafuta rangi ya purple sokoni ya ukindu wanauza sh 100 au 200. Koroga chovya vifaranga. Wakiwa na rangi hiyo kunguru hawachukui.
 
Mkuu samahani hii rangi ya purple inaweza saidia hata kuzuia vicheche kukamata vifaranga
 
Tushauriane hapa kuondoa Kunguru mweusi ili bei ya KUKU wa kienyeji ishuke tukuuzie wewe mlaji hata kwa 5000/= ule firigisi,utumbo na
Fanyeni hivi! mjiunge wafugaji kama 20 hivi, tafuteni dawa ya kweli ya mapenzi na kuzuia pombe! then tangazieni umma kwamba kunguru anatibu Mapenzi na pombe kwa sh. 200/= tu. kila mtu aje na kunguru wake! uone km hawataisha.
 
Hiyo njia ya rangi haitazuia paka. Hivyo ni vyema kuwa na banda imara ili uwe na uhakika wa usalama. Wape chakula wakiwa wadogo wakiwa wakubwa utawafungua
 
Kwanza niseme! Kuna tetesi Hawa kunguru weusi waliletwa hapa inchini (MIJINI) kwa ajili ya kampeni ya usafi (Enzi za W/Mkuu Edo-lowassa)!

Kama ni kweli, Wataalam walioidhinisha lifanyike Hilo Basi walikurupuka!

Ebu waza kunguru mweusi anapora Hadi tonge la nyama mkononi, Ebu waza kunguru wanachukua nyama hata ikiwa jikoni wanafunua na kudokoa;

Yote tisa Hawa Kunguru weusi sasa wamegeuka kero kubwa Sana kwa sisi Wafugaji wa Kuku wa kienyeji!

MFANO Kuku Mtetea,Unamtunza vizuri anaatamia mayai 22 (Unatamani uyale mayai lakini unawaza soko la kuku), anatotoa vifaranga 18 , Hadi vifaranga hao wakue kunguru anakuwa kashapunguza vifaranga 17 kwa kuwala!

Mimi Kama mfugaji nabakiwa na kimoja tu, hapo sijazungumzia gharama ya chanjo ya Mdondo n.k!

Na ili Kuku awe wa kienyeji lazima akale chakula cha kuparua, ukimfungia kuku wa kienyeji hakui haraka na Ni rahisi Sana kufa kwa magonjwa!

Je; Nitumie mbinu/dawa gani ili vifaranga wasiliwe na Kunguru?

Toa maoni kwa faida yako pia maana msipotushauri namna ya kutokomeza Hawa Kunguru, Sisi Wafugaji tutapandisha bei, Msishangae siku KUKU wa kienyeji tukaja UZA LAKI MOJA!

Naombeni maoni yenu wadau, Vinginevyo mtaendelea kula mabloiler ya kuku wa Kizungu huko mtaani mpate kansa, Hususani kwa wapenda virigisi ambako sumu zote za kuku bloiler hukimbilia!

Tushauriane hapa kuondoa Kunguru mweusi ili bei ya KUKU wa kienyeji ishuke tukuuzie wewe mlaji hata kwa 5000/= ule firigisi,utumbo na kuvunja mifupa!

KARIBUNI KWA MAONI JAMANI
Kuna mbinu hii itumie mkuu nunua pumba na asubuhi usiwatoe wape pumba halafu usiwafungulie nje na hao kunguru na mwewe muda wao wa kutafuta chakula kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana halafu wewe wafungulie kuku wako kila siku saa kumi na mpaka saa kumi na mbili halafu kuwa nao makini kwa muda huu kunguru na mwewe watakuwa wachache au wameshiba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom