Kungfu ya China (Ngumi Taiji)

Feb 13, 2021
5
5
Kungfu ya China--Ngumi Taiji


NGUMI TAIJI ILIYORAHISISHWA YA MIKAO 24

二十四式简化太极拳

HOW TO DO TAIJIQUAN

Imetafsiriwa na Tumaini

Mielekeo hufuatana na masaa l2 ya saa. Huanza kwa kuangalia kwenye saa 6 huku saa 12 ikiwa nyuma yako. Saa 3 ikiwa kwenye upande wako wa kushoto na saa 9 ikiwa kuliani kwako. Hivyo kugeuka na kuelekea kwenye saa 7 ni geuko la 30°kulia, na kugeuka na kuelekea kwenye saa 7-8 ni geuko la 45°.

SEHEMU A

第 一 部 分

Mkao wa 1: Hatua ya Kuanza (起势)​

1) Simama katika hali ya kiasili na panua miguu kulingana na upana wa mabega, elekeza vidole vya miguuni mbele, ning’iniza mikono katika hali ya kiasili na kuviweka vitengele vyako kwenye mapaja yako. Angalia mbele.

Mambo ya kukumbuka: Simamisha wima kichwa na shingo, na kidevu chako kielekee ndani kidogo. IJsibenue kifua wala kurudisha tumbo ndani, Jilegeze huku ukiwa umekaa tayari.

2) Inua mikono polepole kuelekea mbele halafu kuelekea juu hadi kwenye usawa wa mabega na viganja vikiwa vinaelekea chini.

3) Dumisha kiwiliwili wima. Kunja magoti huku ukisukuma viganja kwa chini polepole. na visugudi vikitelemka kuelekea kwenye magoti.. Angalia mbele.

Mambo ya kukumbuka: Shusha mabega na visugudi. Pinda kidogo vidole. Uzito ugawanywe sawasawa baina ya miguu miwili. Wakati huohuo pinda magoti, legeza kiuno na matako yasitokeze. Ushushaji wa mikono uandmane na upindaji wa magoti.

Mkao wa 2:Tenga Manyoya ya Shingo ya Farasi Mwitu katika Pande Mbili, Kushoto na Kulia

(左右野马分鬃)​

1) Geuza kiwiliwili kidogo kuelekea kulia(saa 7) na uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia. Inua kitengele cha kulia mpaka kigasha kifike mbele ya sehemu ya kulia ya kifua, kiganja kikitazama chini huku kitengele cha kushoto kikipindwa kama umbo la tao linaloangaliajuu mpaka kiwe kimefikia chini ya kitengele cha kulia . viganja vitazamane kama kwamba vinashika mpira (tangu hapa kitendo hiki kitajulikana kama “ishara ya kushika mpira”). Sogeza wayo wa kushoto karibu na wayo wa kulia na tuliza vidole vya mguu chini. Angalia kitengele cha kulia.

2) Geuza mwili kwa kushoto {saa 4) wakati huohuo wayo wa kushoto uwe ukipiga hatua mbele kuelekea kwenye saa 2-3,kunja goti na hamisha uzito hadi kwenye mguu wa kushoto, nyosha mguu wa kulia na kisigino kikandamizwe chini ardhini ili kuunda “hatua ya upinde” ya kushoto.Wakati unapogeuza mwili wako kidogo kuelekea kushoto. Inua polepole kigasha cha kushoto kimshazari hadi kwenye usawa wa macho na kiganja kikiangaliajuu kimshazari huku kisugudi kikiwa kimekunjwa kidogo ; shusha kitengele cha kulia hadi karibu na nyonga ya kulia huku kiganja kikiwa kinaangalia chini na vidole vikiwa vimenyoshwa mbele. Angalia kitengele cha kushoto.

3) Jifanye kama kwamba”unaketi”polepole---sogeza kiwiliwili nyuma kama kwamba unajitayarisha kuketi --- na hamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Inua kidogo vidole vya wayo wa kushoto na vigeuze kuelekea nje kabla wayo haujakanyaga chlni kabisa. Baadaye kunja mguu wa kushoto na geuza mwili kwa kushoto ( saa 11 ), huku ukihamisha uzito na kuupeleka nyuma tena kwenye mguu wa kushoto.

Fanya ishara ya kushika mpira mbele ya sehemu ya kushoto ya kifua , kitengele cha kushoto kiwe juu. Baadaye sogeza wayo wa kulia mbele hadi kando ya wayo wa kushoto na tuliza vidole chini. Angalia, kitengele cha kushoto.

4) Fanya hatua ya upinde ya kulia kwa wayo kwa kulia ukipiga hatua kuelekea kwenye saa 3—4 , huku ukinyoosha mguu wa kushoto na kisigino kikibonyeza chini na kupinda mguu wa kulia kwenye goti. Katika wakati huohuo, geuza mwili Kuelekea kulia (saa 2), polepole inua kitengele cha kulia kimshazari kuelekeajuu hadi kwenye usawa wa macho hali kiganja kikiwa kinangaliajuu kimshazari, na pinda visugudi kidogo, na elekeza kitengele cha kushoto chini mpaka kishuke na kuwa kando ya nyonga ya kushotojuu ya hayo kiganja kiwe kinatazama chini na vidole viwe vimenyooshwa mbele. Angalia kitengele cha kulia.

5) Rudi vitendo vilivyoelezwa katika 3) hapajuu, lakini pinda“kulia”na“kushoto”.

6) Rudi vitendo vilivyoelezwa katika 4) hapajuu, lakini pinda“kulia”na“kushoto”.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima na kifua kiwe kilegevu. Mikono lazima ijongee kwa kufuata njia ya kitao. Zuia mikono isinyooke vilivyo wakati wa kutenganisha vitengele. Wakati wa kugeuza mwili kiuno kiwe kama mhimili. Mwendo wa kitendo katika kufanya “hatua ya upinde” na katika kutenganisha vitengele unapaswa kuwa usiobadilika na uwe unalingana. Wakati unapopiga hatua kuelekea mbele, weka wayo wako polepole katika mahali pake, kisigino kitue chini kwanza. Goti la mguu ulioko mbele lisipite vidole vya mguuni ambavyo vinapaswa kuelekea mbele; mguu wa nyuma lazima unyooshwe kidogo, ukiunda pembe ya digrii 45 na ardhi. Visigino visiwe katika mstari ulionyooka. Umbali baina yao uwe sentimita 10-30. Tazama kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.



Mkao wa 3 Korongo Mweupe Anatanua Mbawa Zake

(白鹤亮翅)​

1) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto kwenye saa 2. Fanya ishara ya kushika mpira mbele ya sehemu ya kushoto ya kifua, kitengele cha kushoto kiwe juu. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Sogeza wayo wa kulia nusu-hatua kuelekea kwenye wayo wa kushoto na kisha jifanye kama kwamba”unaketi”. Geuza kiwiliwili kidogo kuelekea kulia ( saa 4) . Angalia kitengele cha kulia na uzito ukiwa kwenye mguu wa kulia, jongeza wayo wa kushoto kidogo kuelekea mbele na tuliza vidole polepolejuu ya ardhi. ( Sasa umefanya “hatua ya uwazi” ya kushoto.) Wakati huohuo, geuza kiwiliwili kidogo kuelekea kushoto ( saa 3), na inua kitengele cha kulia mpaka kiwe mbele ya panja la kulia, kiganja kigeuze kwa ndani, huku kitengele cha kushoto kikitelemke mpaka kisimame mbele ya nyonga ya kushoto, kiganja kigeuzwe kwa chini na vidole vielekee mbele. Angalia mbele moja kwa moja.

Mambo ya kukumbuka: Usibenue kifua mbele. Mikono inapaswa idumishwe katika umbo la nusu-duara wakati inapoinuliwa juu au kutelemshwa chini.Pinda mguu wa kushoto kidogo kwenye goti. Uhamishaji wa uzito kwa nyuma lazima ulingane na uinuaJi wa kitengele cha kulia na utelemkaji wa kitengele cha kushoto. Angalia kwenye saa 3.


Mkao wa 4: Piga Brashi Goti na Piga Hatua Kwenye Pande Mbili, Kushoto na Kulia

(左右搂膝拗步)​

1) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto ( saa 2 ) ; telemesha kitengele cha kulia huku ukipandisha kitengele cha kushoto. Geuza kiwiliwili kwa kulia ( saa 5), zungusha kitengele cha kulia kupitia kwenye tumbo na halafu kipandishe hadi kwenye usawa wa sikio, mkono ukiwa umepinda kidogona kiganja kiwe kinatazama juu kimshazari; wakati huohuo kitengele cha kushoto kwanza kiinulie juu na kisha kishushwe chini kwa kufuata njia ya kitao, na kusimama mbele ya sehemu ya kulia ya kifua, kiganja kitazame chini kimshazari. Angalia kltengele cha kulia.

2. Geuza kiviliuili kwa kushoto ( saa 3). wayo wa kushoto upige hatua mbele kuelekea kwenye saa 2 na kuunda ‘hatua ya upinde” ya kushoto. Katika wakati huo huo, sogeza kitengele cha kulia kwa kushoto kupitia kwenye sikio la kulia, na kikifuata geuko la mwili, kisukume kwa mbele mpaka kwenye usawa wa pua, na kiganja kiwe klnaangalia mbele, wakati huohuo kitengele cha kushoto kiwe kinashuka na kuzunguka goti la kushoto na kusimama kando ya nyonga ya kushoto na kiganja kitazame chini. Angalia vidole vya kitengele cha kulia.

3) Jifanye kama kwamba unakaa kitako huku ukipinda goti la kulia polepole, na kuhamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Inua vidole vya wayo wa kushoto na vigeuze kidogo kwa nje kabla ya kukanyaga ardhi . Halafu pinda mguu huo taratibu. Geuza mwili kwa kushoto (saa 1) na uzito uhamishwe kwenye mguu wa kushoto. Peleka wayo wa kulia mbele mpaka ufike kando ya wayo wa kushoto, na tuliza vidole juu ya ardhi. wakati huohuo, geuza kiganja cha kushoto kuelekea juu na pinda kidogo kisugudi cha mkono, peleka kitengele cha kushoto upande na kipandishe hadi kwenye usawa wa sikio, kiganja kikigeuka kimshazari kwa juu, huku kitengele cha kulia kikifuata geuko la mwili, kifanye tao kuelekea juu na halafu kuelekea chini kwa kusboto. Kikisimama mbele ya sehemu ya kushoto ya kifua, kiganja kiwe kinatazama chini kimshazari. Angalia kitengele cha kushoto.

4) Rudia vitendo vya 2) , uicLpYincla kulia na kusiioto” .

5) RudiI vitortdo vya 3) , ukipinda “kulia” na “kushoto “.

6) Rudia vitendo vya 2).

Mambo ya kukumbuka : Dumisha kiwiliwili wima huku ukisukuma vitengele kuelekea mbele. Kiuno na nyonga vinapaswa kulegea. Wakati. wa kukisukuma kiganja kwa mbele, shusha mabega na visugudi na dumisha kiuno katika hali ya kilegevu. Vitendo vya kiganja havina budi vilingane na vitendo vya kiuno na mguu. Umbali baina ya visigino usipungue sentimita 30, Tazama kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 5: Mkono Unapigapiga Pipa

(手挥琵琶)​

Peleka wayo wa kulia mbele nusu-hatua kuelekea kisigino cha kushoto. Jifanye kama kwamba unaketi na geuza kiwiliwili kidogo kwa kuiia (saa 4-5), huku ukihamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Inua wayo wa kushoto na kuweka mbele kidogo, kisigino kishuke chini na goti lipinde kidogo ili kuunda “hatua ya uwazi” ya kushoto. Wakati huohuo, inua kitengele cha kushoto kwa kufuata njia ya kitao mpaka kwenye usawa wa pua. kiganja kiangalie kulia na kisugudi kipinde kidogo. Shusha kitengele cha kulia hadi kifikie upande wa ndani wa kisugudi cha kushoto, kiganja kikabili kushoto. Angalia kidole cha shahada cha kitengele cha kushoto .

Mambo ya kukumbuka: Mwili unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na ya kiasili. Kifua kilegee, mabega na visugudi vya mikono vishushwe. Kitendo cha kuinua kitengele cha kushoto lazima kiwe cha umbo la tao kidogo. Wakati wa kusogeza wayo wa kulia mbele nusu-hatua, uweke polepole kwenye mahali pake, vidole vikitelemka kwanza. Uhamisho wa uzito unalazimika kulingana na uinukaji wa kitengele cha kushoto. Angalia kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 6 Kupiga Hatua kwa Nyuma na Kuzungusha.

Mikono Katika Pande Mbili, Kushoto na Kulia

(左右倒卷肱)​

1) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kulia ( saa 5-6). Mkono wa kulia ufanye nusu-duara kupitia tumbo na kuelekeajuu hadi kwenye usawa wa bega, kiganja kitazame juu na mkono upinde kidogo. Geuza kiganja cha kushoto juu na kuweka vidole vya wayo wa kushoto juu ya ardhi. Kwanza angalia kulia wakati mwili unapogeuka kuelekea upande huo wa kulia, halafu geuka kuangalia mkono wa kushoto ulioko mbele.

2) Pinda mkono wa kulia na sogeza mkono kupitia kwenye sikio kabla ya kuusukuma mbele na kiganja kikiwa kinaangalia mbele. Rudisha nyuma mkono wa kushoto mpaka uwe kando ya kiuno, kiganja kikielekea juu. Wakati huohuo, inua taratibu mguu wa kushoto na kupiga hatua kwa nyuma kuelekea kwenye saa 9-10, uweke polepole juu ya ardhi ukianza na vidole kwanza. Geuza mwili kwa kushoto ( saa 2) na hamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kushoto ili kuunda “hatua ya uwazi” ya kulia na wayo wa kulia ukizunguka kwa vidole mpaka wayo huo uelekee mbele. Angalia kitengele cha kulia.

Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto ( saa 12-1) . Wakati huohuo, peleka kitengele cha kushoto upande na kiinue juu mpaka kwenye usawa wa bega, kiganja kiwe kinatazama juu, huku kiganja cha kulia kikiwa kimegeuzwa juu. Kwanza macho yaangalie kushoto wakati mwili unapogeuka kuelekea kushoto, baadaye geuka na kutazama kitengele cha kulia kilichoko mbele.

3) Rudia vitendo vya 2), ukipinda “kulia” na “kushoto”.

4) Rudia vitendo vya 2) ,

5) Rudia vitendo vya 2 ) , ukipinda “kulia” na “kushoto”.

Mambo ya kukumbuka: Wakati wa kusukuma nje au kurudisha nyuma vitengele, inapasa vitengele visinyooke bali vitembee kwa kufuata njia ya kitao. Wakati wa kusukuma vitengele,dumisha kiuno na nyonga katika hali ya kulegea . Geuko la kiuno lazima lilingane na vitendo vya kitengele. Wakati ukipiga hatua kwa nyuma, kanyaga chini kwa vidole kwanza na halafu wayo mzima utue polepole juu ya ardhi. Mwili unapogeuka, geuza vidole vya wayo wa mbele mpaka viwe katika mstari mmoja na mwili. Sogeza mguu wa kushoto kidogo kuelekea kushoto ( au mguu wa kulia kidogo kuelekea kulia ) wakati unapopiga hatua kwa nyuma. Zingatia kuepa nyayo mbili kutua katika mstari mmoja. Kufuatana na mwelekeo wa geuko la mwili, kwanza tazama upande huo na halafu geuka kutazama kitengele kilichoko mbele . Angalia kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.



Marejeleo: anuwani ya mtandao https://www.baidu.com
Search: 24式简化太极拳视频 (VIDIO KUHUSU NGUMI TAIJI ILIYORAHISISHWA YA MIKAO 24)


SEHEMU B

第二部分


Mkao wa 7:Shika Mkia wa Shomoro, Kushoto

(左揽雀尾)​

1) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kulia ( saa 5-6). Wakati huohuo, peleka kitengele cha kulia upande na kukiinua juu mpaka kwenye usawa wa bega, Kiganja kitazame juu, huku kiganja cha kushoto kikikwa kimegeuzwa kuelekea chini. Angalia kitengele cha kushoto.

Geuza mwili kidogo kwa kulia ( saa 6). Fanya ishara ya kushika mpira mbele ya sehemu ya kulia ya kifua, kitengele cha kulia kiwe juu. wakati huohuo, uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia. Sogeza wayo wa kushoto kando ya wayo wa kulia na shusha chini vidole vya mguu huo. Angaiia kitengele cha kulia.

2) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto (saa 5). Wayo wa kushoto unapiga hatua kwa mbele kuelekea kwenye saa 2-3. Geuza kiwiliwili kwa kushoto zaidi (saa 4) , na kunja mguu wa kushoto ili kufanya “hatua ya upinde”, na mguu wa kulia unyooshwe katika hali ya kiasili . Wakati huohuo , sukuma kigasha cha kushoto kilichopinda kwenye usawa wa bega na kiganja kitazame ndani. Kitengele cha kulia kishuke polepole hadi kando ya nyonga ya kulia. na kiganja kiangalie chini na vidole vielekee mbele. Angalia kigasha cha kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha mikono miwili katika hali ya kupinda wakati wa kusogeza mkono mmoja wo wote. Ratibisha utengaji wa vitengele, ulegevu wa kiuno na ukunjaji wa magoti.

3) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto ( saa 3) huku ukinyoosha kitengele cha kushoto mbele na kiganja kikiwa kimegeuzwa chini. Inua kitengele cha kulia juu, huku kiganJa ukikipindua kiwe chini ya kigasha cha kushoto. Halafu geuza kiwiliwili kwa kulia ( saa 5) huku ukishusha vitengelee vyote viwili chini kama kwamba unapiga mstari wa kimzingo mbele ya tumbo, ukimaliza kwa kitengele cha kulia kikiwa kimenyooshwa upande kwenye usawa wa bega, kiganJa kikiwa juu, kigasha cha kushoto kikilala kwa kukata kifua na kiganja kikiwa kimegeuzwa kwa ndani. Wakati huohuo, hamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Angalia kitengele cha kulia.

Mambo ya kukumbuka: Wakati vitengele vinapotelemshwa chini, usiiname mbele au kubenua matako. Mikono inapaswa kufuata geuko la kiuno na sogea kwa kufuata njia ya duara.

4) Geuza kiwiliwili kidogo kwa kushoto ( saa 1). Pinda mkono wa kulia na kukiweka kitengele cha kulia ndani ya kiwiko cha kushoto (umbali wa sentimita 5). Geuza kiwiliwili zaidi kwa kushoto (saa 3). Sukuma vitengele viwili polepole kuelekea mbele, huku kiganja cha kulia kikitazama mbele na kiganja cha kushoto kuelekea ndani; dumisha mkono wa kushoto katika hali ya kujipinda. Hali kadhalika, hamisha uzito polepole na kuupeleka kwenye mguu wa kushoto ili kuunda “hatua ya upinde". Angalia kiwiko cha kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima wakati wa kusukuma vitengele kuelekea mbele; usogezaji wa vitengele lazima ulingane na ulegevu wa kiuno na ukunjaji wa mguu.

5) Geuza viganja viwili kwa chini wakati kitengele cha kulia kikipitia kwenye cha kushoto na kujongea mbele na halafu kuelekea kulia, hadi kwenye usawa wa kitengele cha kushoto. Tenganisha vitengele kwa upana wa mabega na kujifanya kama kwamba unaketi, hamisha uzito hadi kwenye mguu wa kulia uliokunjwa kidogo, na vidole vya wayo wa kushoto viinuliwe juu. Rudiisha nyuma vitengele viwili hadi mbele ya tumbo, viganja vitazame mbele lakini vielekee chini kidogo. Angalia mbele moja kwa moja.

6) Hamisha polepole uzito na kuupeleka mbele huku ukisukuma vitengele mbele na kuviinua juu kimshazari hali viganja vikiwa vinatazama mbele, mpaka viwiko vifikie usawa wa mabega. Wakati huohuo, kunja goti la kushoto katika “hatua ya upinde” . Angalia mbele. Tazama kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho .

Mambo ya kukumbuka: Wakati wa kusukuma vitengele mbele, vitengele hivyo vinapaswa kufuata mstari wa kitao. Viwiko vyote viwili viwe kwenye usawa wa mabega, na huku visugudi vikikunjwa kidogo.

Mkao wa 8:Shika Mkia wa Shomoro, Kulia

(右揽雀尾)​

1) Jifanye kama kwamba unaketi na geuza kiwiliwili kwa kulia ( saa 6), hamisha uzito kwenye wa kushoto na kuupeleka kwenye mguu wa kulia, na geuza vidole vya wayo wa kushoto kwa ndani. Kitengele cha kulia kichore tao lililolala sawasawa kwa kulia, baadaye kishushe kupitia kwenye tumbo na kipandishe hadi kwenye mbavu za kushoto, kiganja kiangalie juu, kikiunda ishara ya kushika mpira na kitengele cha kushoto kiwe juu. Wakati huohuo, uzito unahimishiwa nyuma kwenye mguu wa kushoto . Weka wayo wa kulia kando ya wayo wa kushoto na kisigino kiinuliwe. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Rudia vitendo vya 2) vya Mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kushoto .

3) Rudia vitendo vya 3) vya mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kushoto”.

4) Rudia vitendo vya 4) vya mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kushoto”.

5) Rudia vitendo vya 5) vya mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kushoto”.

6) Rudia vitendo vya 6) vya mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kshoto”.

Mambo ya kukumbuka: Sawa na yale ya mkao wa 7, ukipinda “kulia” na “kushoto”. Angalia kwenye saa 9 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 9:Mjeledi Mmoja, Kushoto

(左单鞭)​

1) Jifanye kama kwamba unaketi na hamisha polepole uzito kwenye mguu wa kulia na kuupeleka kwnye mguu wa kushoto huku ukigeuza vidole vya mguu wa kulia kuelekea ndani. Wakati huohuo, geuza mwili kuelekea kushoto ( saa 5). Sogeza vitengele vya mikono kwa kushoto huku kitengele cha kushoto kikiwa juu mpaka mkono wa kushoto unyooke na kufikia kwenye usawa wa bega, kiganja kitazame nje, na kitengele cha kulia kiwe mbele ya mbavu za kushoto, kiganja chake kitazame ndani kimshazari. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Geuza mwili kuelekea kulia ( saa 7), ukihamisha uzito polepole na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Sogeza wayo wa kushoto karibu na upande wa kulia na vidole vyake viguse chini. Katika wakati huohuo, kitengele cha kulia kifanye tao kwa juu na kuzunguka kwa kulia mpaka mkono ufike kwenye usawa wa bega. Kiganja cha kulia sasa kigeuziwe nje, bana ncha za vidole pamoja na vipinde kuelekea chini kutoka kwenye kiwiko ili kuunda “kitengele kilichopindamana “, huku kitengele cha kushoto kikiwa kinasogea katika umbo la tao kupitia kwenye tumbo na kusimama mbele ya bega la kulia na kiganja kiwe kinaangalia ndani. Angalia kitengele cha kushoto.

3) Geuza mwili kuelekea kushoto ( saa 4 ) na wayo wa kushoto upige hatua mbele kuelekea kwenye saa 2-3. Kunja goti la kushoto katika “hatua ya upinde “, Wakati ukihamishia uzito kwenye mguu wa kushoto, zungusha kiganja cha kushoto polepole na kukisukuma mbele pamoja na ncha za vidole hadi kwenye usawa wa macho na kisugudi kikunje kidogo. Angalia kitengele kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima na kiuno kilegezwe. Kisugudi cha kulia lazima kikunjwe kidogo kwa chini na kisugudi cha kushoto kiwekwe moja kwa moja juu ya goti la kushoto. Shusha mabega . Kiganja cha kushoto kigeuzwe kitengele cha kushoto kikiwa kinageuzwa kuelekea mbele; usikigeuze upesi sana au ghafla sana. Mabadiliko ya vitendo vyote yanapaswa yaandamane vizuri. Angalia kwenye saa 2 -3 katika kitendo.

Mkao wa 10: Punga Vitengele kama Mawingu, Kushoto na Kulia

(左右云手)​

1) Hamisha uzito kutoka kwenye mguu wa kushoto na kuupeleka kwenye mguu wa kulia na geuza mwili polepole kuelekea kulia ( saa 7-8 ) huku ukigeuza vidole vya wayo wa kushoto kuelekea ndani. Mkono wa kushoto ufanye tao kupitia tumhoni na kusimama mbele ya bega la kulia na kiganja kigeuzwe kimshazari kuelekea ndani. Wakati huohuo, fungua vidole vya kulia na geuza kiganja kuelekea nje. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Geuza kiwiliwili polepole kuelekea kushoto ( saa 4-5 ). Uzito ukiuhamishia kwenye mguu wa kushoto. Kitengele cha kushoto kipitie usoni kwa umbo la tao na huku kiganja kikigeuka polepole kuelekea nje. Kitengele cha kulia kifanye tao kwa kupitia tumboni na baadaye kielekee juu mpaka kwenye bega la kushoto na kiganja kigeuzwe kimshazari kwa ndani. Wakati huohuo, sogeza wayo wa kulia uwe sambamba na upande wa wayo wa kushoto na nyayo zitengane kwa sm. 10-20 hivi, Angalia kitengele cha kulia.

3) Geuza kiwiliwili polepole kuelekea kulia ( saa 1-2 ), uzito ukiuhamishia kwenye mguu wa kulia. Kitengele cha kulia kinaendelea kusogea kwa upande wa kulia kupitia kwenye uso, kiganja kigeuziwe nje, huku kitengele cha kushoto kikiwa kinaFanya tao kupitia kwenye tumbo na kuelekea juu mpaka kwenye usawa wa bega na kiganja kigeuzwe kimshazari kuelekea ndani. Halafu wayo wa kushoto upige hatua ya upande,, Angalia kitengele cha kushoto.

4) Rudia vitendo katika 2).

5) Rudia vitendo katika 3).

6) Rudia vitendo katika 2) .

Mambo ya kukumbuka: Uti wa mgongo uwe kama mhimili kwa ugeuzaji wa mwili. Legeza kiuno na nyonga na epuka kuinuka au kushuka ghafla kwa mwili. UsogeaJi wa mkono unapaswa uwe katika hali ya kiasili na ya kiduara na unapaswa kufuata ule wa kiuno. Mwendo lazima uwe wa tara tibu na wenye kulingana. Dumisha uwiano wakati wa kusogeza viungo vya chini. Macho yanapaswa kufuata vitengele wakati vinapopitia kwenye uso. Mwili uelekeo kwenye saa 4-5 katika kitendo cha mwisho.
Mkao wa 11: Mjeledi Mmoja,Kulia

(右单鞭)​

1) Geuza kiwiliwili kuelekea kulia ( saa 7 ). Katika wakatii huohuo, kitengele cha kulia kiende kulia na kuunda kitengele kilichopindamana juu kidogo ya usawa wa bega huku kitengele cha kushoto kikiwa kinafanya tao kupitia kwenye tumbo na baadaye kuelekea juu mpaka kwenye bega la kulia na kiganja kigeuzwe kuelckea ndani. Uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia, huku vidole vya wayo wa kushoto vikiwa vinagusa chini. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Vitendo ni sawa na vya 3) katika mkao wa 9.

Mambo ya kukumbuka: ni sawa na yale ya mkao wa 9. Angalia kwenye 2-3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 12 Mpapaso wa Juu Kwenye Farasi

(高探马)​

1) Wayo wa kulia upige nusu-hatua kwa mbele; uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia. Fungua kitengele cha kulia na geuza viganja vyote viwili kuelekea juu na visugudi vikunjwe kidogo, huku mwili ukigeukia kulia kidogo ( saa 4-5 ), kisigino cha kushoto kiinuliwe polepole ili kuunda “hatua ya uwazi”. Anga1ia mbele kwenye kitengele cha kushoto.

2) Geuza mwili kidogo kwa kushoto ( saa 3 ) ; Sogeza mbele kitengele cha kulia kwa kupitia kwenye sikio la kulia; kisukume mbele huku kiganja kikiwa kinatazama mbele na vldole viwe kwenye usawa wa macho yakionyesha mbele. Shusha kitengele cha kushoto mpaka kifike mbele ya nyonga ya kushoto, kiganja kikiwa bado kinakabili juu. Wakatt huohuo sogeza wayo wa kushoto kidogo kwa mbele na vidole viguse chini. Angalia kitengele cha kulia .

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima na kukilegeza. Shusha mabega na kunja kisugudi cha kulia kidogo kuelekea chini,, Usiinue mwili wala kuutelemsha wakati wa kuhamishia uzito kwenye mguu wa kulia. Kabili saa 3 katika hali ya mwisho.

SEHEMU C

第三部分


Mkao wa 13 Kupiga Teke kwa Kisigino,Kushoto na Kulia

(左右蹬腿)​

1) Kingamisha vitengele kwa kutanua kitengele cha kushoto, kiganja kikiwa kinaelekea juu, kwenye mgongo wa kiwiko cha kulia. Kisha tenganisha vitengele na visogeze kwa kutuata umbo la tao linaloelekea chini na viganja vigeuzwe kimshazari kuelekea chini. wakati huohuo, inua wayo wa kushoto na piga hatua kwa mbele kuelekea kwenye saa 2, ukiunda “hatua ya.upinde” ya kushoto na vidole vigeuke kidogo kuelekea nje. Angalia mbele moja kwa moja.

2) Vitengele viwili visogee kwa nje kiduara na halafu vielekee chini mpaka vikingamane mbele ya kifua, viganja yiwili vigeukie ndani, na mgongo wa kitengele cha kushoto uangalie upande wa ndani wa kiwiko cha kulia. Katika wakati huohuo, weka wayo wa kulia karibu na wayo wa kushoto na vidole viguse chini. Angalia mbele-kulia.

3) Panua vitengele, ukivipeleka upande hadi kwenye usawa wa mabega, kunja kidogo visugudi na geuza viganja kwa nje. Katika wakati huohuo, inua mguu wa kulia, kunja goti, na sogeza wayo mbele polepole kuelekea kwenye saa 4. Angalia kitengele cha kulia.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha utulivu wa mwili. Viwiko viwe katika usawa wa mabega, wakati vitengele vinapopanuliwa. Mguu wa kushoto ukunjwe kidogo wakati wayo wa kulia ukipiga teke kwa mbele, na nguvu ya kupiga teke inapaswa kuanzia kwenye kisigino, na vidole vielekee kidogo kwa ndani. Upanuaji wa vitengele lazima uandamane na upigaji teke. Mkono wa kulia uwe sambamba na mguu wa kulia. Angalia kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 14:Kupiga Masikio ya Mpinzani kwa Ngumi Mbili

双峰贯耳)​

1) Rudisha wayo wa kulia na uache ukining’inia kwa kukunja goti ili paja liwe katika hali ya usawa. Sogeza kitengele cha kushoto juu na kuelekea mbele, halafu kielekee chini karibu na kitengele cha kulia mbele ya kifua, ukigeuza viganja viwili juu. Vitcngele vyote viwili visogezwe kiduara kuelekea chini, na kutua kwenye pande mbili za goti la kulia. Angalia moja kwa moja mbele.

2) Wayo wa kulia unashuka chini pole pole na kukanyaga ardhi kwenye sehemu ya kulia kidogo mbele ya wayo wa kushoto, huku uztto ukiwa unahamishiwa kwenye mguu wa kulia na kuunda “hatua ya upinde”. Katika wakati huohuo, shusna vitengele vyote viwili na kidogo kidogo kunja ngumi. Halafu vitengele vifanye tao kuelekea juu na mbele kutoka pande mbili hadi mbele, vikiwa pamoja kwenye usawa wa masikio katika msogeo wa koleo,ngumi ziangale juu kimshazari.Umbali baina ya ngumi mbili

Uwe kiasi cha sm. 10-20. Angalia ngumi ya kulia,

Mambo ya kukumbuka: Kichwa na shingo viwe wima, kiuno na nyonga viwe vilegevu na ngumi zifumbwe bila ya kukazwa. Dumisha mabega chini na visugudi vining’inie katika hali ya kiasili na mikono ikunjwe kidogo. Tazama kwenye saa 4 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 15:Kugeuka na Kupiga Teke kwa Kisigino,Kushoto

(转身左蹬脚)​

1) Pinda mguu wa kushoto na kujifanya kuwa unaketi. Geuza mwili kwa kushoto ( saa 12 ) na vidole vya wayo wa kulia vielekee ndani. Fumbua ngumi kwa wakati mmoja na kupanua vitengele kwa pamoja katika msogeo wa kiduara ukivitanua upande kidogo juu ya usawa wa mabega, viganja vitazame mbele. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Uzito uharnishiwe kwenye mguu wa kulia. Sogeza wayo wa kushoto hadi kando ya wayo wa kulia na gusisha vidole chini. Katika wakati huohuo, zungusha vitengele viwili kuelekea chini hadi vifike kwenye pande mbili za mwili na kisha vielekee ndani na mbele mpaka vikingamane mbele ya kifua, na mgongo wa kitengele cha kulia utazame. kwenye upande wa ndani wa kiwiko cha kushoto, viganja vyote viwili viwe vikiangalia ndani, Angalia mbele kwenye kitengele cha kushoto

3) Panua vitengele na kuvinyoosha upande hadi kwenye usawa wa mabega, na viwiko vikunjwe. kidogo na viganja viangalie nje. Wakati huohuo, inua mguu wa kushoto na kunja goti na halafu sogeza wayo kidogokidogo mbele kuelekea kwenye saa 10. Angalia kitengele cha kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Sawa na yale ya Mkao wa 13, isipokuwa pinda “kulia” na “kushoto”. Angalia kweye saa 10 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 16 Kchutama na kusimama kwa Mguu Mmoja, Kushoto(左下势独立)​

1) Sogeza nyuma mguu wa kushoto na kuudumisha katika hali ya kuning’inia kwa kukunja goti ili paja liwe limelala sawa. Geuza kiwiliwili kwa kulia ( saa 1). Pinda kitengele cha kulia,huku kiganja cha kushoto kikiwa kinageuzwa juu na kufnya tao kwa juu na kulia mpaka kifike mbele ya bega la kulia na kutazama ndani kimshazari. Angalia kitengele cha kulia.

2) Chutama polepole kwa mguu wa kulia, huku ukinyoosha mguu wa kushoto kwa upande kuelekea kwenye saa 8-9. Kitengele cha kushoto kinyooshwe kwa upande kwa kufuata upande wa ndani wa mguu wa kushoto, kiganja kikikabili mbele. Angalia kwenye kitengele cha kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Wakati mguu wa kulia unapokuwa umekunjwa kikamilifu wakati wa kuchutama, geuza vidole kidogo kwa nje na nyoosha mguu wa kushoto na vidole vigeuziwe ndani; nyayo zote mbili zikanyage chini. Vidole vya wayo wa kushoto viwe katika mstari mmoja na kisigino cha mguu wa kulia. Usiinamishe sehemu ya juu ya mwili mbele kupita kiasi.

3) Ukitumia kisigino kama kiini. geuza vidole vya wayo wa mguu wa kushoto kidogo kwa nje ili viwe katika mstari mmoja na mguu ulionyooshwa; geuza vidole vya wayo wa mguu wa kulia kwenda ndani huku mguu wa kulia ukiwa unanyooka na mguu wa kushoto ukiwa unapindika. Uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kushoto. Kiwiliwili kigeuke kidogo kwa kushoto ( saa 10 ) na baadaye kiinue polepole kuelekea mbele. Katika wakati huohuo, mkono wa kushoto uendelee kunyooshwa kwa mbele, na kiganja kiwe kinaangalia kulia, huku kitengele cha kulia kikiwa kinatelemka nyuma ya mgongo, na ncha za vidole vilivyofungamana zikionyesha nyuma. Angalia kitengele cha kushoto.

4) Inua wayo wa kulia kidogo kidogo. Na kunja goti la kulia ili paja liwe limelala sawa sawa. Wakati huohuo fumbua kitengele cha kulia na kijongeshe kwa kupitia kwenye upande wa nje wa mguu wa kulia na halafu kuelekea juu hadi mbele mpaka kiwiko kilichokunjwa kiwe juu ya goti la kulia, vidole vikionyesha juu na kiganja kikitazarna upande wa kushoto. Shusha kitengele cha kushoto hadi kwenye nyonga ya kushuto, kiganja kiangalie chini. Angalia kitengele cha kulia.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima. Kunja kidogo mguu unaosimama. Vidole vinapaswa kuelekezwa chini katika hali ya kiasili, wakati wayo wa kulia unapoinuliwa. Angalia kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 17 Kuchutama na Kusimama kwa Mguu Mmoja, Kulia

(右下势独立)​

1) Weka wayo wa kuliachini mbele ya wayo wa kushoto (saa 6), ukitumia vidole vya kushoto kama kiegemeo. Wakati huohuo, kitengele cha kushoto kiinuliwe kiupandeupande na kuelekea juu mpaka kwenye usawa wa bega na kupindwa katika umbo la ndoana inayoangalia chini, huku kitengele cha kulia, kikifuata kiwiliwili,kinaongezwa kitao mpaka mbele ya bega la kushoto na vldole vikielekea juu. Angalia kitengele cha kushoto.

2) Rudia vitendo katika 2) vya mkao wa 16, ukipinda “kulia” na “kushoto”.

3) Rudia vitendo katika 3) vya mkao wa 16, ukipinda “kulia” na “kushoto”.

4) Rudia vitendo katika 4) vya mkao wa 16, ukipinda “kulia” na “kishoto”.

Mambo ya kukumbuka: Inua wayo wa kulia kidogo mbele kabla ya kuchutama na kunyoosha mguu wa kulia kwa upande. Mambo mengine madogomadogo ni sawa na yale yaliyotajwa katika mkao wa 16, isipokuwa vitendo vya “kulia” na “ushoto”vinapinduliwa. Angalia kwenye saa 9 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 18:Pisha Kashabu kwenye Pande Mbili, Kushoto na Kulia
(左右穿梭)​

1)Geuza mwili kwa kushoto (saa 7 ). Wekawayo wa kushoto chini mbele ya wayo wa kulia, vidole vikielekea nje. Na kisigino cha kulia kiinuliwe kidogo, kunja magoti yote mawili ili kuunda nusu “mkao wa miguu iliyopachikana”. Katika wakati huohuo, fanya ishara ya kushika mpira mbele ya sehemu ya kushoto ya kifua na kitengele cha kushoto kiwe juu. Kisha sogeza wayo wa kulia kando ya wayo wa kushoto na gusisha vidole vyake chini, Angalia kigasha cha kushoto.

2) Mwili ugeuziwe kulia ( saa 10 ) na wayo wa kulia upige hatua kuelekea mbele kwenye saa10-11 na kuunda “hatua ya upinde”. Wakati huohuo, kitengele cha kulia kiwe kinasogea .juu na ku8imsaajuu ya upande wa kulia wa kipaji na kiganja kiwe kinageuzwa juu kimshazari. Halafu kitengele cha kushoto kiende chini mpaka kwenye upande wa kushoto wa mwili na halafu kiende mbele na juu mpaka kwenye usawa wa pua, kiganja kiwe kinatazama mbele. Angalia kitengele cha kushoto.

3) Geuza mwili kidogo kwa kulia ( saa 11 ), uzito ukiuharnishia nyuma kidogo, na vidole vya wayo wa kulia viwe vinageuziwa nje kidogo. Halafu uzito uhamishiwe nyuma kwenye mguu wa kulia. Weka wayo wa kushoto karibu na wayo wa kulia na vidole viguse chini. Wakati huohuo, fanya ishara ya kushika mpira mbele ya sehemu ya kulia ya kifua na kitengele cha kulia kiwe juu, Angalia kigasha cha kulia.

4) Rudia vitendo vya 2), ukipinda “kulia” na “kushoto”.

Mambo ya kukumbuka: Usiiname mbele wakati wa kusukuma vitengele mbele, au kupandisha mabega wakati wa kuinua vitengele. Vitendo vya kitengele vinapaswa kuandamana na vile vya kiuno na miguu. Umbali baina ya visigino katika “harua ya upinde” uwe kiasi cha sm.30. Tazama kwenye saa 8 katika kitendo cha mwisho.

SEHEMU D

第四部分


Mkao wa 19:Sindano chini ya Bahari

(海底针)​

1) Wayo wa kulia upige nusu-hatua kwa mbele. Uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia wakati wayo wa kushoto unaposogea kwa mbele kidogo na vidole vikishuka chini na kuunda “hatua ya uwazi” ya kushoto. Katika wakati huohuo, geuza mwili kidogo kwa kulia ( saa 9-10 ). Shusha kitengele cha kulia mbele ya mwili, halafu kiinue mpaka kiwe kando ya sikio la kulia na mwili ugeuziwe kwenye saa 8-9, kisukumie chini kimshazari mbele ya mwili, na kiganja kiangalie kushoto na vidole vielekezwe chini kimshazari. Wakati huohuo, kitengele cha kushoto kiwe kiwe kinafanya tao kwa mbele na kwa chini mpaka kifike kando y nyonga ya kushoto na kiganja kiwe kinaangalia chini na vidole vielekee mbele. Angalia ardhi kwa mbele.

Mambo ya kukumbuka: Kwanza geuza mwili polepole kwa kulia na halafu kwa kushoto. Usiiname sana. Dumisha kichwa wima na matako yasibenuke . Mguu wa kushoto uwe umekunjwa kidogo. Kabili kwenye saa 9 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 20 Tupa Mkono

(闪通臂)​

1) Geuza mwili kidogo kwa kulia ( saa 4). Piga hatua kwa mbele na wayo wa kushoto ili kuunda “ hatua ya upinde” . Wakati huohuo, inua mkono wa kulia na kisugudi kikunje mpaka kitengele kisimame juu ya panja la kulia. Geuza kiganja kimshazari kuelekea juu, huku kidole gumba kikielekea chini. Inua kitengele cha kushoto kidogo na. kukirsukumia mbele mpaka kwenye usawa wa pua na kiganja kiangalie mbele. Angalia kitengele cha kushoto.

Mambo ya kukumbuka: Dumisha kiwiliwili wima na katika hali ya kiasili. Legeza kiuno na nyonga. Usinyooshe mkono wa kushoto. Dumisha musuli za mgongo katika hali ya kilegevu. Wakati wa kusukuma kiganja kwa mbele, kitendo lazima kiandamane na “hatua ya upinde”. Angalia kwenye saa 9 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 21 Geuka, Inama Chini, Kinga na Piga Ngumi

(转身搬拦槌)​

1) Jifanye kama kwamba unaketi na uzito uhamishiwe kwenye mguu wa kulia. Mwili ugeuziwe kulia ( saa. 12 ) , na vidole vya wayo wa kushoto ugeukie ndani, kisha uzito uhamishiwe tena kwenye mguu wa kushoto. Wakati wa kugeuza mwili, kitengele cha kulia kiwe kinakwenda kiduara kwa kulia na chini, na halafu vidole vikunjwe ili kuunda konde, huku kikiwa kinapitia tumboni kando ya mbavu za kushoto na fundo za mgongo wa ngumi zikiwa zinaelekea juu. Katika wakati huohuo, inua mkono wa kushoto mpaka juu ya kichwa na kiganja kiwe kinageuzwa kimshazari kuelekea juu, Angalia mbele.

2) Geuza mwili kwa kulia ( saa 2 ). Ngumi ya kulia ijongee juu na mbele kwenye sehemu ya mbele ya kifua na fundo za mgongo wa ngumi zigeuziwe chini. Kitengele cha kushoto kitelemke kwa upande wa nyonga ya kushoto na kiganja kigeuziwe chini na vidole vielekezwe mbele. Katika wakati huohuo, rudisha wayo wa kulia na, bila ya kusimama au kuufanya uguse chini, piga hatua moja kwa mbele na vidole viwe vinageukia nje. Angalia ngumi ya kulia.

3) Hamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia na wayo wa kushoto upige hatua kwa mbele. Wakati huohuo, jikinge kwa kitengele cha kushoto kwa kukifanya kiende juu na mbele kutoka upande wa kushoto katika msogeo wa kiduara, kiganja kigeuzwe kidogo kwa chini, na kurudisha nyuma ngumi ya kulia mpaka ubavuni mwa nyonga ya kulia na tumbo la ngumi litazame juu. Angalia kitengele cha kushoto.

4) Pinda mguu wa kushoto na kuunda “hatua ya upinde”. Wakati huo huo, ngumi ya kulia isukumwe mbele mpaka kwenye usawa wa kifua na mgongo wa kitengele hicho utazame upande.wa kulia. Rudisha nyuma kitengele cha kushoto mpaka kifike kando ya kigasha cha kulia. Angalia ngumi ya kulia.

Mamho ya kukumbuka: Ngumi ya kulia isiwe imekazwa. Wakati wa kurudisha ngumi nyuna. Kigasho kwanza kigeuziwe ndani na halafu kwa nje. Wakati ngumi inapsukumwa mbele, bega la kulia liwe linafuata kitendo hicho na linyooke kidogo kuelekca mbele. Telemsha mabega na visugudi. Mkono va kulia lazima upinde kidogo. Angalia kwenye saa 3.

Mkao wa 22:Kuonekana Kufungika

(如封似闭)​

1) Nyoosha kitengele cha kushoto kwa mbele kutoka chini ya kiwiko cha kulia; fumbua ngurmi ya kulia. Viganja vigeuzie juu, panua vitengele na kuvisogeza nyuma polepole. Jifanye kama kwamba unaketi na vidole vya wayo wa kushoto viinuliwe huku uzito ukiwa unahamishiwa kwenye mguu wa kulia. Angalia mbele.

2) Ukiwa unavigeuzia chini viganja mbele ya kifua, visukumie chini kupitia tumhoni na halafu mbele, na kisha kuelekea juu. Kitendo hiki kinapomalizika viwiko viwe usawa wa mabega,viganja viwe vinatazama mbele. Katika wakati huohuo, pinda mguu wa kushoto ili kuunda “hatua ya upinde”. Angalia mbele.

Mambo ya kukumbuka: Usiiname nyuma wakati unapojifanya karna kwamba unaketi. Usibenue matako. Legeza mabega na geuza visugudi kwa nje kidogo wakati mikono inaporudishwa nyuma kwa kuandamana na kitendo cha mwili. Usirudishe mikono nyuma moja kwa moja. baina ya vitengele viwili usipite upana wa mabega. Angalia kwenye saa 3 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 23: Vitengele vya Msalaba

(十字手)​

1) Kunja goti la kulia na kujifanya kama kwamba unaketi, ukihamisha uzito na kuupeleka kwenye mguu wa kulia. Geuza mwili kwa kulia ( saa 7 ) huku vidole vya wayo wa kushoto vikigeukia ndani. Vikifuata geuko la mwili, vitengele vyote viwili viwe vinasogea kiupande na kiduara kwenye usawa wa mabega, na viganja viangalie mbele na visugudi vikunjwe kidogo. Wakati huohuo, vidole vya wayo wa kulia viwe vinageukia n.je kidogo na uzito uwe unahamishiwa kwenye mguu wa kulia ili kuunda “hatua ya upinde” ya kulia. Angalia kitengele cha kulia.

2) Uzito unahamishiwa polepole kwenye mguu wa kushoto na vidole vya wayo wa kulia vinageukia ndani. Halafu sogeza wayo wa kulia kuelekea kwenye wayo wa kushoto kusudi nyayo zote mbili ziwe sambamba na upana wa mabega; nyuosha miguu pole pole. Katika wakati huohuo, telemsha vitengele vyote viwili na kuvikingamanisha mbele ya tumbo, kisha inua vitengele vilivyokingamana hadi kwenye usawa wa kifua na viwiko vikiwa kwenye usawa wa mabega, kitengele cha kulia kiwe nje na viganja vikabili ndani, Angalia mbele moja kwa moja.

Mambo ya kukumbuka: Usiiname mbele wakati wa kupanua vitengele au kuvikingamanisha. Wakati unapokuwa katika mkao wa kisambamba dumisha mwili wima katika hali ya kiasili, na Kichwa kisimame na kidevu kipelekwe ndani kidogo. Dumisha mikono iliyokunjwa katika hali ya starehe, mabega na visugudi vishushwe chini. Angalia kwenye saa 6 katika kitendo cha mwisho.

Mkao wa 24: Hatua ya Kufunga

(收势)​

1) Geuza viganja mbele na chini huku ukitelemsha vitengele vyote viwili polepole hadi kwenye nyonga, Angalia mbele moja kwa moja
Mambo ya kukumbuka: Dumisha mwili mzima katika hali ya ulegevu na vuta pumzi ndefu na kwa polepole wakati vitengele vinaposhuka. Weka wayo wa kushoto kando ya wayo wa kulia baada ya pumzi kubadilika na kuwa sawa sawa.
中国一瞥1984/46







Angalia:

Inafaa kuumaliza vitendo vya seti nzima kwa dakika3-5 ; haifai kuharakisha sana wala kuvifaya pole pole sana.

Katika maelezo ya maneno, “wakati huo huo” kila yanapotokea haidhuru yawe yameandikwa kwanza au baadaye, vitendo vya sehemu fulani za mwili, huhitajiwa kutendwa kwa pamoja, usivitenge katika sehemu mbili, yaani cha kufanywa kwanza na cha kufanywa baadaye.

Mielekeo ya vitendo ni ya mbele, nyuma, kushoto na kulia. Haidhuru ugeuke namna gani, mwelekeo lazima uwe wa mbele, nyuma, kushoto na kuiia.

Mstari wa kuelekeza (→ ) uliochorwa kwenye picha unamaanisha njia na nafasi zinazofuatwa na kitendo kimoja mpaka kitendo kingine.

Nambari zilizoandikwa kwenye picha za vitendo zilizofungwa ndani ya alama ya kifungo zinamaanisha mkao wa mwili baada ya kumaliza kufanya kitendo fulani.



——————————————————————————————————


Wayo wa vistari alivyoachana ni wayo wa kushoto; wayo wa mstari halisi, yaani wa mfululizo , ni wayo wa kulia. Nambari zisizo na alama ya kifungo zilizomo ndani ya unyayo zinamaanisha utaratibu wa vitendo; nambbari zilizofungwa ndani alama ya kifungo (brackets) zinamaanisha mtindo wa kushoto na wa kulia wa kitendo fulani au marudio ya kitendo fulani, unyayo mtupu unamaanisha kitendo cha kupita.

http://album.sina.com.cn/pic/001fSgHjzy7Ccq07EeIb8
Alama hii inamaanisha nafasi ya vidole vya wayo vinavyotua chini katika kitendo cha kupita。
http://album.sina.com.cn/pic/001fSgHjzy7Ccq07EeIb8
Alama hii inamaanisha kuwa sehemu ya mbele ya wayo inakanyaga chini.
Alama hii inamaanisha kuwa kisigino kinakanyaga chini.
Alama hii inamaanisha kitendo cha kuinua goti na kulining'iniza angani cha mtindo wa kusimama kwa mguu mmoja.
Alama hii inamaaanisha kitendo cha mguu cha kuning'inia angani cha kupiga teke kwa kushoto (kulia)
————————————————————————————

Anuwani ya mtandao: https://www.baidu.com

Search: 24式简化太极拳视频 (VIDEO KUHUSU NGUMI TAIJI ILIYORAHISISHWA YA MIKAO 24)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom